USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

hawana maana ...sasa kama Vick kamata eti mbunge sasa anaoingea nini bungeni kama sio kwenye kujipaka mapoda tu na kujibinua binua

Afadhali huyu anae jipaka poda na kujibinua binua kama unavyosema, maana yuko active, je wanaosinzia, kujamba na kukoroma?
 
Wafutwe ama kupunguzwa, ni wengi mno hawana mchango wowote, angalia bunge la sasa viti maalum ni upupu mtupu.
Wengi ni mashangingi tu hawana la maana kule mjengoni zaidi ya kuliletea taifa mzigo wa gharama zisizo za lazima.
 
System yetu inatudanganya kwamba wanawawakilisha akina mama zetu ni wizi mtupu. Hiyo cost ya representation is just high kuwalipa 100 plus kama wawakilishi wasiochanguliwa na wawakilishwa. Affirmative yes wenzetu wanataka kuwezeshwa lakini iwe kwa kuwapa opportunity ya kugombea na sio kwa kupewa kama ilivyo kwa sasa...sina mfano mzuri lakini najua ipo mifano mingi tu ya kuigwa na sisi :frusty:
 
Tatizo hilo zigo linatokana na masharti ya wafadhili; sasa sijui cost benefit analysis inasemaje? Je, hiyo cost inakuwa covered na wafadhili tu au na sehemu ya kodi ninayolipa? Au ni kodi yangu tu? Je, tuna - benefit nini kama Taifa?
 
Siku zote huwa najiuliza sana hawa wabunge wa viti maalumu ni wa nini??? Hawatakiwi kbisa kuwepo. nadhani ni jambo muhimu liingizwe kwenye katiba mpya kuondoa kabisa.

Hili liendane na wabunge wa kuteuliwa na Rais, hawa pia hawatakiwi sana sana rais anatumia nafasi hii kutoa rushwa kwa watu...mfano Rais Mpaka kumteua Dr. Lamwai, marehemu chief fundikira, Rashid H. Rashid, makongoro Nyerere; rais Kikwete kumteua Thomasi mwang'onda, Zakia Megji. Kamna ni uwaziri basi katiba mpya tuingize kipengele wabunge wasitokane na wabunge ili raisi awe na wigo mpana wa kuchangua kama ni muhimu kwake
 
Ni kweli huyu mkubwa amenena, wanawake tunapaswa tupiganie nafasi zetu za heshimu, ukimshinda mwanamume na uwakilishi pia unaheshimiwa. siyo huu ambao kila mmoja anaona tumependelewa na wakubwa ndiyo wanataka kila wakiwaona vitimaalum wanaota ngono tu. Tutapigania kina mama mbona wanaume wengi sasa wanaelewa uwezo wetu!!!!
 
Tushalisema sana hili jambo hapa. Huyu Katibu baada ya kuona hilo ametumiaje mamlaka yake ku influence mabadiliko zaidi ya kusema tu (which is appreciated, coming from the corridors of power and with the risk of alienating a whole lotta bigwigs)
 
mbaya ni hasara tunayopata kwa ili suhala lisilo na tija kwa wataifa wala kina mama
wanawake wanazidi kutaabika tu, hii imewekwa kujiosha kwenye mashirika ya kimataifa ili kupata misaada
na anayeumia zaidi ni sisi wananchi wa kawaida kwa kutozwa kodi kulipa mishahara ya hawa viti maalumu

Ni kweli huyu mkubwa amenena, wanawake tunapaswa tupiganie nafasi zetu za heshimu, ukimshinda mwanamume na uwakilishi pia unaheshimiwa. siyo huu ambao kila mmoja anaona tumependelewa na wakubwa ndiyo wanataka kila wakiwaona vitimaalum wanaota ngono tu. Tutapigania kina mama mbona wanaume wengi sasa wanaelewa uwezo wetu!!!!

Tushalisema sana hili jambo hapa. Huyu Katibu baada ya kuona hilo ametumiaje mamlaka yake ku influence mabadiliko zaidi ya kusema tu (which is appreciated, coming from the corridors of power and with the risk of alienating a whole lotta bigwigs)
 
Ni mzigo kwa taifa na kuongeza idadi ya kura za ndiyooooo!!!! kwa chama chenye wabunge wengi, mwishowe ni kupitisha maamuzi na sheria mbumbumbu, tunazojutia hapo mbeleni, kwani wengi tu ni rubber stamp ya ruling elite. (Umaalum unamwakilisha nani maalum, anyway?)
 
hawana maana ...sasa kama Vick kamata eti mbunge sasa anaoingea nini bungeni kama sio kwenye kujipaka mapoda tu na kujibinua binua
Kigogo Kigogo hapo kwenye red kaka du umenivunja mbavu kwi kwi kwiiiiiiiiiiiii,kujibinua binua ili amurushe roho mzee
 
Wabunge wa viti maalum hawatakiwi kabisa, ni kulitwisha mzigo Taifa. Inashangaza mtu kama Ana Abdala amekuwa ni Mbunge kwa zaidi ya miaka 30 bungeni lakini mpaka leo ndiyo kusema hana uwezo wa kusimama jimboni na kuomba kura?
 
Hata kesho vifutwee na sio kwamba tunawaonea wivu hapana hawana tija na hawafanyi kitu chochote!! Kuhusu uroda tuwaulize wao wathibitishe. Lakini kuna ushaidi wa kimazingira!!!!!
 
Huu ni ufisadi mwingine ambao wananchi wa Tanzania wamebebeshwa!Mpaka lini mali zetu zitafujwa namna hii kwa maslahi ya watu wachache?
Dk. Kashilila aliwaponda wabunge wa viti maalumu akisema kundi hilo ni mzigo kwa taifa kwa kuwa hawana kazi wanayoifanya zaidi ya kukidhi maslahi ya kisiasa.
Dk. Kashilila alisema ni Tanzania pekee ndiyo yenye wabunge wa aina hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine zinazofuata mfumo wa mabunge ya jumuiya ya madola (Commonwealth).

Mtendaji huyo wa Bunge alihoji sababu za kuwepo kwa kundi hilo la wabunge, wakati wabunge wa majimbo wapo. Wabunge 102 kati ya wabunge 350 waliopo bungeni hivi sasa ni wabunge wa viti maalumu.

“Wabunge wa majimbo wapo 239, ndiyo kusema kwamba katika eneo lote la Tanzania hakuna eneo lisilokuwa na uwakilishi bungeni. Ukisema kila mbunge wa jimbo aende jimboni kwake, utakuta nchi yote ipo covered (ina wabunge).
“Sasa unajiuliza kama hivyo ndivyo hawa wabunge wa viti maalumu wa kazi gani? Wanafanya kazi ipi special (maalumu) ambayo haifanywi na mbunge wa jimbo?” alihoji.
Alipoulizwa iwapo hoja yake hiyo inalenga kushauri wabunge wa viti maalumu wafutwe, Dk Kashilila alisema: “ Mimi siwezi kushauri moja kwa moja kwamba wabunge hawa wafutwe, ila tunaweza kufanya marekebisho tukaiga affirmative policy ya Uingereza.

“Tukatenga maeneo, kwamba katika kila majimbo kumi ya uchaguzi majimbo manne yawe kwa ajili ya wanawake kama hoja ni kuwa na wanawake bungeni. Hapo vyama visisimamishe wagombea wanaume katika majimbo hayo.
“Kwa kufanya hivyo tutajikuta tumewaondoa hawa wabunge wa viti maalumu ambao kimsingi mimi sioni kazi wanayofanya na badala yake tutakuwa na wanawake bungeni, lakini wanaotokana na majimbo,” alisema.

Wakizungumza na Mtanzania kwa nyakati tofauti, baadhi ya wabunge walitoa maoni tofauti kuhusiana na kauli hiyo, huku baadhi yao wakiipinga wazi wazi kauli hiyo.Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) alimshangaa Dk. Kashilila kwa kutoa mashambulizi makali dhidi ya wabunge wa viti maalumu, huku akisema wabunge hao ni watu wenye mchango mkubwa kwa jamii.

“Hayo ni maoni yake, lakini kusema wabunge wa viti maalumu ni mzigo kwa taifa mimi nadhani siyo sahihi. Wabunge wa viti maalumu wana mchango mkubwa kwa jamii na hata hao walioweka mfumo huu walijua wabunge wa viti maalumu wana mchango.
“Tunafanya shughuli nyingi za kijamii, tumekuwa tukisaidiana na wabunge wa majimbo katika mambo mbalimbali. Pale ambapo wabunge wa majimbo hawatimizi sisi tumekuwa tukiziba mapengo. Kwa hiyo si kweli kusema wabunge wa viti maalumu hawana kazi ya kufanya,” alisema


Maoni yangu:
tunapoteza zaidi ya bilioni 50 kwa miaka mitano kughalimia hawa wabunge wasio na tija kwa taifa wala kwa hao wanawake wanao wawakilisha nadhani tukifuata mfumo wa kiingereza kwa sababu tunafuta huo itakuwa makini zaidi, au kama vipi tuwe na utaratibu ambao wabunge wanatoka kajimboni tu na uwakilishi na ushawishi wao utaoneka wazi wazi, hizo pesa tunaweza kuzitumia kuleta maendeleo makubwa sana, na hawa wakuu wa mikoa na wilaya watolewe pia hakuna kitu cha maana wanachofanya.

SOURCE: MTANZANIA (
Wabunge kikaongoni)
 
mkuu umeona, sasa hiyo ni kuwezesha au kubaka nafasi, bora hata wangekuwa wanapewa miaka mitano tu hakuna kurudia KITI MAALUMU na sio 102 ni vingi mno, vifutwe hayo ndio maoni yangu
ni mzigo mkubwa kwa bibi yangu kijijini
na shangazi yangu pia kwa kulipia kodi watu walemaisha bora
huu ni wakati wananchi kushika hatamu

Wabunge wa viti maalum hawatakiwi kabisa, ni kulitwisha mzigo Taifa. Inashangaza mtu kama Ana Abdala amekuwa ni Mbunge kwa zaidi ya miaka 30 bungeni lakini mpaka leo ndiyo kusema hana uwezo wa kusimama jimboni na kuomba kura?
 
Nimelipigia kelele hili muda mrefu tu humu. Tunaigharamia sana SIASA huku huduma muhimu kwa WATANZANIA ikidorora vibaya.
 
Back
Top Bottom