hawana maana ...sasa kama Vick kamata eti mbunge sasa anaoingea nini bungeni kama sio kwenye kujipaka mapoda tu na kujibinua binua
Wengi ni mashangingi tu hawana la maana kule mjengoni zaidi ya kuliletea taifa mzigo wa gharama zisizo za lazima.Wafutwe ama kupunguzwa, ni wengi mno hawana mchango wowote, angalia bunge la sasa viti maalum ni upupu mtupu.
Ni kweli huyu mkubwa amenena, wanawake tunapaswa tupiganie nafasi zetu za heshimu, ukimshinda mwanamume na uwakilishi pia unaheshimiwa. siyo huu ambao kila mmoja anaona tumependelewa na wakubwa ndiyo wanataka kila wakiwaona vitimaalum wanaota ngono tu. Tutapigania kina mama mbona wanaume wengi sasa wanaelewa uwezo wetu!!!!
Tushalisema sana hili jambo hapa. Huyu Katibu baada ya kuona hilo ametumiaje mamlaka yake ku influence mabadiliko zaidi ya kusema tu (which is appreciated, coming from the corridors of power and with the risk of alienating a whole lotta bigwigs)
Wabunge wa VITU MAALUM sio Viti maalum
Kigogo Kigogo hapo kwenye red kaka du umenivunja mbavu kwi kwi kwiiiiiiiiiiiii,kujibinua binua ili amurushe roho mzeehawana maana ...sasa kama Vick kamata eti mbunge sasa anaoingea nini bungeni kama sio kwenye kujipaka mapoda tu na kujibinua binua
Wabunge wa VITU MAALUM sio Viti maalum
Dk. Kashilila aliwaponda wabunge wa viti maalumu akisema kundi hilo ni mzigo kwa taifa kwa kuwa hawana kazi wanayoifanya zaidi ya kukidhi maslahi ya kisiasa.
Dk. Kashilila alisema ni Tanzania pekee ndiyo yenye wabunge wa aina hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine zinazofuata mfumo wa mabunge ya jumuiya ya madola (Commonwealth).
Mtendaji huyo wa Bunge alihoji sababu za kuwepo kwa kundi hilo la wabunge, wakati wabunge wa majimbo wapo. Wabunge 102 kati ya wabunge 350 waliopo bungeni hivi sasa ni wabunge wa viti maalumu.
Wabunge wa majimbo wapo 239, ndiyo kusema kwamba katika eneo lote la Tanzania hakuna eneo lisilokuwa na uwakilishi bungeni. Ukisema kila mbunge wa jimbo aende jimboni kwake, utakuta nchi yote ipo covered (ina wabunge).
Sasa unajiuliza kama hivyo ndivyo hawa wabunge wa viti maalumu wa kazi gani? Wanafanya kazi ipi special (maalumu) ambayo haifanywi na mbunge wa jimbo? alihoji.
Alipoulizwa iwapo hoja yake hiyo inalenga kushauri wabunge wa viti maalumu wafutwe, Dk Kashilila alisema: Mimi siwezi kushauri moja kwa moja kwamba wabunge hawa wafutwe, ila tunaweza kufanya marekebisho tukaiga affirmative policy ya Uingereza.
Tukatenga maeneo, kwamba katika kila majimbo kumi ya uchaguzi majimbo manne yawe kwa ajili ya wanawake kama hoja ni kuwa na wanawake bungeni. Hapo vyama visisimamishe wagombea wanaume katika majimbo hayo.
Kwa kufanya hivyo tutajikuta tumewaondoa hawa wabunge wa viti maalumu ambao kimsingi mimi sioni kazi wanayofanya na badala yake tutakuwa na wanawake bungeni, lakini wanaotokana na majimbo, alisema.
Wakizungumza na Mtanzania kwa nyakati tofauti, baadhi ya wabunge walitoa maoni tofauti kuhusiana na kauli hiyo, huku baadhi yao wakiipinga wazi wazi kauli hiyo.Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) alimshangaa Dk. Kashilila kwa kutoa mashambulizi makali dhidi ya wabunge wa viti maalumu, huku akisema wabunge hao ni watu wenye mchango mkubwa kwa jamii.
Hayo ni maoni yake, lakini kusema wabunge wa viti maalumu ni mzigo kwa taifa mimi nadhani siyo sahihi. Wabunge wa viti maalumu wana mchango mkubwa kwa jamii na hata hao walioweka mfumo huu walijua wabunge wa viti maalumu wana mchango.
Tunafanya shughuli nyingi za kijamii, tumekuwa tukisaidiana na wabunge wa majimbo katika mambo mbalimbali. Pale ambapo wabunge wa majimbo hawatimizi sisi tumekuwa tukiziba mapengo. Kwa hiyo si kweli kusema wabunge wa viti maalumu hawana kazi ya kufanya, alisema
Maoni yangu: tunapoteza zaidi ya bilioni 50 kwa miaka mitano kughalimia hawa wabunge wasio na tija kwa taifa wala kwa hao wanawake wanao wawakilisha nadhani tukifuata mfumo wa kiingereza kwa sababu tunafuta huo itakuwa makini zaidi, au kama vipi tuwe na utaratibu ambao wabunge wanatoka kajimboni tu na uwakilishi na ushawishi wao utaoneka wazi wazi, hizo pesa tunaweza kuzitumia kuleta maendeleo makubwa sana, na hawa wakuu wa mikoa na wilaya watolewe pia hakuna kitu cha maana wanachofanya.
SOURCE: MTANZANIA (Wabunge kikaongoni)
Wabunge wa viti maalum hawatakiwi kabisa, ni kulitwisha mzigo Taifa. Inashangaza mtu kama Ana Abdala amekuwa ni Mbunge kwa zaidi ya miaka 30 bungeni lakini mpaka leo ndiyo kusema hana uwezo wa kusimama jimboni na kuomba kura?
Wafutwe. Dk kashirima ameshaona watu wanateua mademu zao kuwaleta Bungeni, haina maana.
Nadhani hapo umekosea mkuu! Ni Dr. Kashililah au sio mangi?