Mdahalo wa katiba uliofanyika ubungo plaza leo umekuwa tofauti na midahalo ya hapo kabla ile iliyotawaliwa na hisia za vyama vya siasa, enzi hizo hakuna kilichofanikiwa zaidi ya watu kuzomeana na kusodoana tu.
Leo hali ilikuwa tofauti sana kwani washiriki walikuwa watulivu na walipeana nafasi za kila aliyebahatika kupata nasafi ya kuchangia alitoa mawazo yake kwa uhuru tofauti na awali ilivyokuwa.
MAWAZO YALIYONIGUSA NA MAPYA KWANGU NA NINAYOYAUNGA MKONO NI HAYA YAFUATAYO:-
1. Dada anaeitwa Agnes alitoa mawazo yake kuhusu VITI maalum, alisema viti maalum vinarahisisha wanawake kutawaliwa na hata wanapofika bungeni hawana jeuri ya kutoa mawazo huru, kwani ni lazima waendelee kujipendekeza na kuwaabudu waliowawezesha (waliowazawadia)kupata nafasi hizo
MY TAKE.
Hii ni dhahili sana kwani hata mifano ipo wazi, sio wazo zuri kuwapata wabunge hawa kwa mfumo unaotumiwa na viongozi wa vyama vya siasa kuwaweka watu wao, hata pengine ikatamkwa kuwa ni mademu zao, wake zao, dada zao na ndio sababu hata leo utamsikia VITI maalum akijitambulisha kuwa ni mbunge kivuli wa jimbo fulani analoliota, na sio mbunge wa viti maalum wanaona aibu na hawana uhuru kwa kuhofia kuwakera waliowawezesha (waliowazawadia) nafasi hizo n.k.
Ushauri wangu kwenye katiba mpya hizi nafasi za makundi maalum, zisipatikane kupitia vyama vya siasa, ili makundi haya ya wanawake na walemavu, yawakilishwe bila itikadi za kisiasa, hebu jiulize wabunge wa ccm wakiwa wengi na wapo kwa ajili ya wanawake, je watakua sauti ya nani kama sio sauti ya wanawake wa ccm, na hata kwa wle wa cdm na cuf na nccr nao wataishi kiitikadi vilevile hapa makundi maalum hayawakilishwi bali ni unafiki tu wa kisiasa na huu mfumo wao wa kuwapata viti maalum.
2. BABU ALIYETOA MFANO WA KINYONGA.
Babu mzee sana alitoa unabii kama uliwahi kutolewa na Nabii samweli kuwa hatakufa mpaka atakapomuona Yesu, na mzee huyu leo ametoa unabii huo kwa kusema kuwa hatakufa kabla ccm haijafa, akatoa mifano mingi ya kuwataka viongozi wawe waadilifu na akashangiliwa sana.
Mfano alioutoa Babu wa kinyonga kufa akiwa tayari amefikia term(yaani miezi ya kujifungua)ni mfano dhahili akilenga ccm ni lazima ife ili mfumo wa vyama vingi uwe huru na wa haki, hapa sio tu kwa ccm bali hata vyama vya siasa vina jukumu la kufa kiitikadi kiimani na kimienendo na hata kisera/kiorganisation, ili viweze kuwa na mitazamo imara na ya haki ya dhati, na ili viweze kudumu mioyoni mwa wananchi na viweke misingi ya kudumu ya kujiendesha kimgawanyiko wa kiutendaji, ndio tafasiri ya kufa na kufufuka upya, kufa pia kuna maana ya kuwaweka watendaji wenye sifa katika ngazi husika na sio kama ilivyo kwa vyama vyetu hapa tz, vyenye viongozi wanaotumia nafasi zao kuwateua watu kwa vigezo wajuavyo wenyewe na sio uwezo wala sifa dhahili, hapa bila kukubali kuliwa na kufa ili vifufuke upya, hatutaona kipya i swear!!
NIWATAKIE MAATAZMIIO MEMA YA KATIBA MPYA...