USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

HIVI NDIVYO VITU AMBAVYO VINATAKIWA VIINGIZWE KWENYE KATIBA ,ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi
 
Hakuna asiyefahamu kuwa hakuna value addition whatsover kwa kuwa na wabunge wa viti maalumu...zaidi ya hasara kwa taifa ya kuwamaintaini wabunge 102.

Swala la kupiga makofi, mipasho, kuzomea au kuwa na idadi ya wapiga kura ndani ya bunge nk si mambo yenye tija na wala watz hatuyahitaji ktk bunge letu.
 
Jamani wakati wa mchakato wa kuunda katiba mpya tutapendekeza vifutwe kwani havina tija
 
Now you are talking
 
Sehemu kubwa ya wabunge viti maalumu ni vibaraka wa wagodfather waliohakikisha wana teuliwa. kwa sehemu kubwa wabunge hawa uwajibikaji ni mdogo kwa sasbubu hawako acountable majimboni... wanaongeza uwingi bungeni bila tija kwa taifa, wanalipwa pesa nyingi bila kutika jasho.

Wabunge hawa haswa wale kumi ambao raisi anamalaka wa kuwateua kikatiba,, hawana mtu wanaemwakilisha bungeni wapo wapo tu kazi yao ni kuongeza idadi ya kura bungeni kupitisha miswada inayoliangamiza taifa..... wabunge hawa tuwakatae.... ikishindikana ni heri tukabaki na hawa viti maalumu kwa makundi maalum, sio hawa wanaoteuliwa na rais bila kuzingatia wanamwakilisha nani bungeni.....

Kwa mfano, nini tija ya mchungaji mama Rwakatale au mzee Makamba,, Kingunge? Hili janga kwa taifa
 
huu ni ufisadi kwa hawa wabunge wa viti maalum bungeni ni kaaina ya ufisadi
 
wamejazana bungeni lakini no output badala yake ni posho na rushwa kwishney
 
jamani mi naomba kuuliza wabunge wa viti maalum wanamuwakilisha nani bungeni?
 
Mdahalo wa katiba uliofanyika ubungo plaza leo umekuwa tofauti na midahalo ya hapo kabla ile iliyotawaliwa na hisia za vyama vya siasa, enzi hizo hakuna kilichofanikiwa zaidi ya watu kuzomeana na kusodoana tu.
Leo hali ilikuwa tofauti sana kwani washiriki walikuwa watulivu na walipeana nafasi za kila aliyebahatika kupata nasafi ya kuchangia alitoa mawazo yake kwa uhuru tofauti na awali ilivyokuwa.

MAWAZO YALIYONIGUSA NA MAPYA KWANGU NA NINAYOYAUNGA MKONO NI HAYA YAFUATAYO:-

1. Dada anaeitwa Agnes alitoa mawazo yake kuhusu VITI maalum, alisema viti maalum vinarahisisha wanawake kutawaliwa na hata wanapofika bungeni hawana jeuri ya kutoa mawazo huru, kwani ni lazima waendelee kujipendekeza na kuwaabudu waliowawezesha (waliowazawadia)kupata nafasi hizo
MY TAKE.
Hii ni dhahili sana kwani hata mifano ipo wazi, sio wazo zuri kuwapata wabunge hawa kwa mfumo unaotumiwa na viongozi wa vyama vya siasa kuwaweka watu wao, hata pengine ikatamkwa kuwa ni mademu zao, wake zao, dada zao na ndio sababu hata leo utamsikia VITI maalum akijitambulisha kuwa ni mbunge kivuli wa jimbo fulani analoliota, na sio mbunge wa viti maalum wanaona aibu na hawana uhuru kwa kuhofia kuwakera waliowawezesha (waliowazawadia) nafasi hizo n.k.
Ushauri wangu kwenye katiba mpya hizi nafasi za makundi maalum, zisipatikane kupitia vyama vya siasa, ili makundi haya ya wanawake na walemavu, yawakilishwe bila itikadi za kisiasa, hebu jiulize wabunge wa ccm wakiwa wengi na wapo kwa ajili ya wanawake, je watakua sauti ya nani kama sio sauti ya wanawake wa ccm, na hata kwa wle wa cdm na cuf na nccr nao wataishi kiitikadi vilevile hapa makundi maalum hayawakilishwi bali ni unafiki tu wa kisiasa na huu mfumo wao wa kuwapata viti maalum.

2. BABU ALIYETOA MFANO WA KINYONGA.
Babu mzee sana alitoa unabii kama uliwahi kutolewa na Nabii samweli kuwa hatakufa mpaka atakapomuona Yesu, na mzee huyu leo ametoa unabii huo kwa kusema kuwa hatakufa kabla ccm haijafa, akatoa mifano mingi ya kuwataka viongozi wawe waadilifu na akashangiliwa sana.
Mfano alioutoa Babu wa kinyonga kufa akiwa tayari amefikia term(yaani miezi ya kujifungua)ni mfano dhahili akilenga ccm ni lazima ife ili mfumo wa vyama vingi uwe huru na wa haki, hapa sio tu kwa ccm bali hata vyama vya siasa vina jukumu la kufa kiitikadi kiimani na kimienendo na hata kisera/kiorganisation, ili viweze kuwa na mitazamo imara na ya haki ya dhati, na ili viweze kudumu mioyoni mwa wananchi na viweke misingi ya kudumu ya kujiendesha kimgawanyiko wa kiutendaji, ndio tafasiri ya kufa na kufufuka upya, kufa pia kuna maana ya kuwaweka watendaji wenye sifa katika ngazi husika na sio kama ilivyo kwa vyama vyetu hapa tz, vyenye viongozi wanaotumia nafasi zao kuwateua watu kwa vigezo wajuavyo wenyewe na sio uwezo wala sifa dhahili, hapa bila kukubali kuliwa na kufa ili vifufuke upya, hatutaona kipya i swear!!
NIWATAKIE MAATAZMIIO MEMA YA KATIBA MPYA...
 
jinsi mambo yanavyoelekea kubadilika kuna dalili kwamba viti maalum mwisho wake ni 2014. Je itakuwa jambo la mbolea iwapo tanzania itabakia na wabunge wa kuchaguliwa tu!!!!!
 
jinsi mambo yanavyoelekea kubadilika kuna dalili kwamba viti maalum mwisho wake ni 2014. Je itakuwa jambo la mbolea iwapo tanzania itabakia na wabunge wa kuchaguliwa tu!!!!!

Wabunge wa viti maalumu nao pia ni ufisadi....huko bungeni wanawakilisha interest za mabosi wao and not citizen

narudia tena to me viti maalumu ni mzigo kwa taifa.
 
Viti maalumu ni kwa ajili ya wachumba,ma girlfriends,wake wa wanene wa vyama vya siasa,ukiangalia kwa undani utakuta wengi wa wabunge wa viti maalumu wana jamaa zao humo humo mjengoni.hakika sijui wanachokifanya humo mjengoni zaidi ya kujibinua binua na kuombana dili za vimiradi au vitenda
 
Mkuu hiyo writting colour yako haipo sawa, change! Viti maalum visitishwe kwani ni gharama kwa taifa!
 
Ngoja waje wenyewe hapa muone povu lao!
 
Hivi nao huwa wanalamba ile Millioni Tano ya Mbunge kwa maendeleo ya Jimbo?
 


Not true at all, hiyo ni negativity ya wabongo. Ni udhalilishaji mkubwa kuwa eti wanajibinuabinua, hivi kweli hamuoni kazi wanayofanya? na je hao wawakilishi wa majimbo are they working properly kwa maslahi ya wananchi? au ndo mfumo dume mlionao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…