Yes, ni kauli rasmi ya wanawake kiserikali.
Margaret Sitta, akiwa Waziri wa Jinsia, alisoma hotuba ya Wizara siku ya Wanawake duniani mwaka jana Tabora mbele ya Rais (siku ile Kikwete aliposema vitoto vya shule vinavyotiwa mimba vinapenda vyenyewe kuchakachuliwa) akasisitiza kauli hiyo mara kibao "Tukiwezeshwa tunaweza...Tukiwezeshwa tunaweza"! Nilishangaa mno. Ukiwezeshwa na nani, kivipi, akufadhili na akufanyie na akumiliki na akutunze halafu akutumie kama nyama ya kujifurahishia? Yani mnajidharaulisha na kuonyesha wazi kwamba gender perspectives za wanawake wa Tanzania bado ni finyu mno.
Ni kauli rasmi ya muelekeo wa sera ya maendeleo ya jinsia iliyotengenezwa na wanawake wenyewe, vinginevyo Wizara isingeiweka kwenye hotuba ya Waziri.
Kimey, hata hilo pendekezo lako la "tukiamua tunaweza" is no better. Ukiamua unaweza, ni ile ile kitchen floor mentality ya mwanamke kutokuwa na maamuzi, subiri kwenye vigoda vya uani na mazuria ya ukili, sio kwenye meza ya maamuzi mbele mjengoni. Kuja mbele kuamua na kuweza subiri sisi tukuwezeshe.