<br />Wabunge wa viti maalumu nao pia ni ufisadi....huko bungeni wanawakilisha interest za mabosi wao and not citizen<br />
<br />
narudia tena to me viti maalumu ni mzigo kwa taifa.
kwani mdee ni special seat................uko wapy weye hebu kawaamshe special seats bungeniAnd Mdee bana... naona niache tu.... One thing is for sure... she is way great ukifananisha na the speacial seats wengine...
Sielewi alosema mwanamke akiwezeshwa anaweza ...manake kwangu inamaanisha dharau kuwa mwanamke hawezi mpaka awezeshwe!
...Sijui hii mantiki ya tukiwezeshwa tunaweza hivi ni nani aliye ianzisha? ni wanawake au?
kwani mdee ni special seat................uko wapy weye hebu kawaamshe special seats bungeni
Yes, ni kauli rasmi ya wanawake kiserikali.
Margaret Sitta, akiwa Waziri wa Jinsia, alisoma hotuba ya Wizara siku ya Wanawake duniani mwaka jana Tabora mbele ya Rais (siku ile Kikwete aliposema vitoto vya shule vinavyotiwa mimba vinapenda vyenyewe kuchakachuliwa) akasisitiza kauli hiyo mara kibao "Tukiwezeshwa tunaweza...Tukiwezeshwa tunaweza"! Nilishangaa mno. Ukiwezeshwa na nani, kivipi, akufadhili na akufanyie na akumiliki na akutunze halafu akutumie kama nyama ya kujifurahishia? Yani mnajidharaulisha na kuonyesha wazi kwamba gender perspectives za wanawake wa Tanzania bado ni finyu mno.
Ni kauli rasmi ya muelekeo wa sera ya maendeleo ya jinsia iliyotengenezwa na wanawake wenyewe, vinginevyo Wizara isingeiweka kwenye hotuba ya Waziri.
Kimey, hata hilo pendekezo lako la "tukiamua tunaweza" is no better. Ukiamua unaweza, ni ile ile kitchen floor mentality ya mwanamke kutokuwa na maamuzi, subiri kwenye vigoda vya uani na mazuria ya ukili, sio kwenye meza ya maamuzi mbele mjengoni. Kuja mbele kuamua na kuweza subiri sisi tukuwezeshe.
i wonder nani ali-design hili lipya. Limekaa ki-stage zaidi ya a debating chamber...
na chalila kibuda
balozi wa finland nchini tanzania, sinikka antilla, amewaasa wanawake kugombea nafasi za uongozi ili waachane na mfumo wa kuteuliwa kwenye viti maalum kwa kuwa unawanyima sauti kwenye maamzi.
antilla aliyasema hayo juzi wakati wa maadhimisho ya siku ya demokrasia duniani kwa wanawake, yaliyofanyika katika ukumbi wa karimjee, jijini dar es salaam ambalo liliratibiwa na umoja wa wanawake wenye uwakilishi bungeni (t-wcp).
alisema kupigania nafasi za uongozi kwa kusimama wenyewe kutawejengea kuwa na maamzi mazuri katika masuala yao na kutetea wanawake wenzao.
antilla alisema juhudi za wanawake tanzania bado si za kutosha, hivyo akawataka washiriki kikamilifu katika siasa kwa kogombea na kuacha nafasi za kuteuliwa ambazo zinawafanya wasiwe na sauti.
alisema wanawake wa rwanda wameweza kuwa katika maamzi kutokana na kushiriki kikamilifu katika siasa na kuweza kufikia asilimia 51 katika nchi za afrika.
antilla alisema kuwa wanawake wakifikia asilimia 50 wanaweza kushinikiza serikali kuweka bajeti ya wanawake ambayo itashughulikia masuala yao ambayo yamekuwa kikwazo.