USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Mapenzi mabaya sasa hawa wabunge viti maalumu wa Chadema wana kazi gani bungeni?

Ebu nitajie mchango hwa Mbunge Rose Kamili, Ester Matiku, Cristiana Lissu, Regia Mtema, yule mtoto wa Ndesamburo na mtoto wa Mashishanga..

wapo wengi hawafai, hakuna mbunge makini viti maalum sio CCM wala Chadema, CUF wote ni pumba tu..

Viti maalum vifutwe vyote ni mzigo kwa taifa

Leo imenibidi nikubaliane na wewe
 
Kumbe mambo ndo hayo! Labda ndo maana kuna siku bwana mkubwa alisema "ukitaka kula nawe uliwe kidogo". Kweli Tz ni mwisho wa matatizo.
 
Mapenzi mabaya sasa hawa wabunge viti maalumu wa Chadema wana kazi gani bungeni?

Ebu nitajie mchango hwa Mbunge Rose Kamili, Ester Matiku, Cristiana Lissu, Regia Mtema, yule mtoto wa Ndesamburo na mtoto wa Mashishanga..

wapo wengi hawafai, hakuna mbunge makini viti maalum sio CCM wala Chadema, CUF wote ni pumba tu..

Viti maalum vifutwe vyote ni mzigo kwa taifa

Ipo siku nitakufuata ulipo kaa unafikiri atukujui,mwanaume mzima huna aibu,changia hoja au anzisha yako.
 
wanakula kodi zetu bure, hawana maana kwa mfano wabunge wa mikoa mipya ambayo mpaka sasa haipo ipo kwenye makaratasi tu wanamuwakilisha nani kama sio wizi wa mchana? hata mawaziri tulio nao pia hawatusaidii ushahidi ziara za kikwete wakati antembelea wizara namnukuu eti waziri aningia ofisini saa 5 akifika anaangalia machafuko misri kupitia aljazira tv ikifika saa 7 anaenda kula harudi tena mpaka kesho ,mfano wa pili waziri anashtaki kwa rausi eti kunawafanya kazi hewa kibao du tutafika kweli hasa ukizingatia tunataka kuanza kununua used item ccm hoyeee
 
viti maalum hasa wa CCM ACHENI TAARABU BUNGENI , igeni mfano wa ,

  1. HALIMA MDEE
  2. ANNE KILANGO
  3. NAOMI KAIHULA
  4. MAGDALENA SAKAYA
  5. JENESTA MHAGAMA
  6. CHIKU.........
 
Huu ni ukweli usiopingika kabisa kwamba hizi ofa wanazopewa hawa kina mama wa CCM kuingia bungeni wanazitumia vibaya.

Mara nyingi nimekuwa nikuatilia vikao vya bunge,na kwa umakini niliougundua ni kwamba, wabunge hao wa CCM hawako mle ndani kwa ajili ya kutetea maslahi ya watanzania bali kwa ajili ya kulinda chama chao na wale waliowapa ofa..

Wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha kuvuruga amani bungeni,huku spika wao akiwakingia kifua.
Kutetea hoja zisizokuwa na kichwa wala mguu..
Hakuna wanachojua zaidi ya umbea tu.

Mkuu maelezo yako ni ya kweli kabisa. Wabunge wa kuteuliwa kimsingi ni watu waliobebwa na watu binafsi wakishirikiana na vigogo wa CCM. Ndiyo maana unawakuta wengi ni wake, watoto, nyumba dogo za watu vigogo fulani ndani ya CCM. Ni wazi katika mazingira kama haya mbunge huyu atakuwa na vipaumbele tofauti sana na mbunge wa jimbo. Wajibu wake wa kwanza ni uaminifu kwa mtu aliyembeba na matokeo ndiyo kama ulivyohitimisha.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia michango ya wabunge mbalimbali hasa wa viti maalum.Jamani sifurahi jinsi wabunge hawa hasa wa CCM wanavyowakilisha watanzania!!!!!.Ni taarabu mwanzo mwisho BUNGENI,hawajui kilichowapeleka pale,..Inaonesha wazi kuwa wamelewa na ule msemo usemao.NIKISHIBA NINAJALI NINI.badilikeni waheshimiwa ,TETEENI MASLAHI YA NCHI YENU,JENGA HESHIMA KWAKO NA JAMII NZIMA YA TANZANIA KWA kuzungumza vitu vya kueleweka.SIYO KILA KITU -VE .MAKOFI,+VE, MAKOFI.Hatupo enzi za mipasho,kama mmeingia BUNGENI KWA KUWA ASSIGNED SPECIAL TASK tujue ili nasi tujipange jinsi ya kuwakabili...

........BADILIKENI............

WANA JF ENDELEENI KUTOA DUKUDUKU.....

NAWASILISHA
 
Hizo ndio habari tunazotakiwa kujuulishwa. tarabu sanaa. stori za kina ngeleja kwenda kununua machangudoa china. Lakini ukigusia tu shida za mtanzania we!
 
- Ni matumaini yangu makubwa sana kwamba kwenye katiba mpya, Tanzania TUTAONDOKANA NA Wabunge wa Bure na Viti maalum, I am sick na Bunge kujaa vimada wa Viongozi wa vyama vyetu vya siasa vyote kuanzia CCM mpaka Upinzani, ENOUGH! Wabunge wote wawe wa Majimbo tu Only Mwanasheria Mkuu ndiye aruhusiwe kuingia Bungeni na Cabinet bila kugombea jimbo!

- Taifa letu linapoteza Shillingi Billioni 90 kila miaka mitano on hawa Wabunge wa bure, that is insane kwa taifa masikini kama letu.

Much Respect People!

William @ NYC, USA: Le Mutuz Baharia!
 
Wabunge wa viti maalum ni kero kero kero. Na kipindi hiki wale wa viti maalum - CCM wanatisha. They look/behave kama vile wametoka red-district. It is sickening na historia itawakumbuka.

Kuhusu mwanasheria mkuu, nadhani kazi yake ibakie kuishauri serikali, na kwa vyovyote vile ASIRUHUSIWE ku-debate bungeni. Kazi yake itaishia kwenye baraza la mawaziri na sio hii ya kujibizana na wawakilishi wa wananchi. Kama wabunge wanataka ufafanuzi basi aitwe kwa utaratibu maalum lakini mwanasheria abaki ofisini kwake. Bunge ni kwa ajili ya wabunge na yeyote anayekwenda bungeni lazima apitie sanduku la kura. No exemption. Yule Mama albino kasaidiaje maalbino wengine kwa kuwepo kwake bungeni? Sanduku la kura. basi.
 
Kuna mmoja wa viti maalumu namuona hapa amejipara kama anaenda kwenye kitchen party, mbaya zaid anasinzia hapa nadhani baada ya lunch yake leo aliteremshia na shots kadhaa za whisky.
 
- Ni matumaini yangu makubwa sana kwamba kwenye katiba mpya, Tanzania TUTAONDOKANA NA Wabunge wa Bure na Viti maalum, I am sick na Bunge kujaa vimada wa Viongozi wa vyama vyetu vya siasa vyote kuanzia CCM mpaka Upinzani, ENOUGH! Wabunge wote wawe wa Majimbo tu Only Mwanasheria Mkuu ndiye aruhusiwe kuingia Bungeni na Cabinet bila kugombea jimbo!

- Taifa letu linapoteza Shillingi Billioni 90 kila miaka mitano on hawa Wabunge wa bure, that is insane kwa taifa masikini kama letu.

Much Respect People!

William @ NYC, USA: Le Mutuz Baharia!

Uko sahihi sana mkuu, na nadhani ndio ugonvi ulioko kati ya CDM na CCM/serikali. kwani Rais ana madaraka makubwa mno, na kama serikali ina kataa ushoga basi ikatae na hili la Viti maalum maana sioni wanafanya nini mfano mbunre kama Mch. Rwakatare anasign tu posho na haieleweki anamwakilisha nani.

badala yakwe tunakuwa na wabunge wengi wasio wawakilishi wa wananchi wanamwakilisha mtu bisafsi, waziri fulania au Rais. Huu ni upumbavu usiokubalika.
 
mara nyingi nilikuwa najiuliza ilikuwaje hadi kuwepo na wabunge viti maalum.......viti maalum vipi hivyo.......au hao ***** ndio viti vyenyewe hawana lolote iondolewa kabisa
 
PKatika vitu vilivyonifanya nione ubunge kuwa wa level ya chini ni hii kitu viti maalumu. Yule aliyechaguliwa na wana nchi anawakilisha sauti ya watu (wanawake kwa waume). Hawa wenzetu sijui huwa wanawakilisha sauti ya nani. Maana hata wanawake wenzao huwa hawawafagilii kabisa, shida za wa mama zimebaki pale pale; watoto wao wanakaa chini ya miti kusoma huku kukiwa na hatari ya nyoka kuwa ng'ata vitu vizito kuwaangukia, jua kali kuwa piga na kuharibu macho yao wakiangalia karatasi nyeupe; wanawake wajawazito ndiyo hao wanabebwa kwa bajaj kwenda kujifungua na wao wanapiga makofi ya kupitisha haya bungeni; wengine wamelazwa chini huko mahospitalini; watoto wa hao wanawake ambao tuna uhakika ni damu yao wanakufa kwa utapia mlo na malaria ambayo kwakuwa na makazi bora tu ingepungua by 50%.

Hawa kina mama wanafanya nini Bungeni? Katika watu wanaochelewesha demokrasia ya nchi yetu kukua ni hawa mamluki wa viti maalumu; maana wengi wanalinda interest za hao hao wanaume wenzetu maarufu kwa ufisadi.

Polygamisim imeingia kwa aina yake kwenye Bunge letu. Watu wana rahisisha shughuliz za ukusanyaji mali kwakutumia nguvu kazi ya mwanamke kama ilivyokuwa enzi za mababu. Walioa wake wengi ili kuongeza nguvu kazi. Chaaaaa laana gani hii jamani?
 
- Ni matumaini yangu makubwa sana kwamba kwenye katiba mpya, Tanzania TUTAONDOKANA NA Wabunge wa Bure na Viti maalum, I am sick na Bunge kujaa vimada wa Viongozi wa vyama vyetu vya siasa vyote kuanzia CCM mpaka Upinzani, ENOUGH! Wabunge wote wawe wa Majimbo tu Only Mwanasheria Mkuu ndiye aruhusiwe kuingia Bungeni na Cabinet bila kugombea jimbo!

- Taifa letu linapoteza Shillingi Billioni 90 kila miaka mitano on hawa Wabunge wa bure, that is insane kwa taifa masikini kama letu.

Much Respect People!

William @ NYC, USA: Le Mutuz Baharia!

Unachosema ni kweli mkuu. Lakini magamba hawataki kabisa kulisikia hilo. Ndio maana sasa hivi tunataka katiba iwe mali ya Watanzania wote na sio ya magamba. Magamba wana ibaka haki ya msingi ya mtanzania ambayo ni katiba
 
viti maalum mie naona vina faida kwa wachache na tungeweza kupunguza hadi kufikia viti 10 tu nchi mzima... pia tungehitaji mid term review ya performance ya wabunge

wengine ni zero kabisa
 
Back
Top Bottom