USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!


Naungana na wajumbe wengine kuendelea kushangaa kuwa haya maneno unayaandika wewe kweli au ni mtu mwingine anayetumia jina lako humu jamvini.

Binafsi nilishawahi kuwahoji wabunge wa viti maalum nilipopata nafasi ya kukutana nao ana kwa ana, na kuwauliza wanafanya nini bungeni, wanamwakilisha nani, na nini faida ya wao kuwepo bungeni kwa wananchi. Hawakulipenda swali langu. Kwa kifupi niliwaambia ya kuwa binafsi sioni kazi wanayoifanya na ningekuwa nina uwezo wa kubadilisha katiba hivyo viti maalum ningeviondoa. Kwa kuwa sasa tuko kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya (?) ni vizuri hilo wazo ulilolitoa likatiliwa mkazo.

Ingawa sina hakika kama kwa mwendo tulionao na kwa kuburuzwa tunakokuona tutafikia mahali pa kusema tunaandika katiba mpya! Labda kwa maandamano na migomo, lakini siyo kwa bunge la vijembe!
 

toka zamani viti vya upendeleo kwa wamama wetu nilikuwa siviafiki. utafutwe utaratibu mwingine wa kuwaingiza wamama wetu bungeni. najua wengi ni viburudisho vya waheshimiwa sana lakini tutafute njia muafaka ili kupunguza kujaza viti maalum ambao wengi wao ni vilaza.
 

Mkuu katiba gani hiyo unayoingelea?. Huu mchakato wa sasa wa Katiba ya serikali ya CCM?. Hatuwezi kujadili katiba ya CCM, tunataka kujadili katiba ya Tanzania. Ila ukiwa kama mwana CCM una haki ya kujadili katiba ya chama serikali ya chama chako. Wapinzani nao wakishika nchi kwa nguvu ya umma kupitia kura zao halali zitakazodharauliwa na CCM watatutengenezea katiba yao. Huu Mchakato mzima ni FLAWED
 

FJM Uko right. AG akae tu ofisini awe anaitwa siku maalum ili kujibu hoja mbali mbali zenye kuhitaji kufafanuliwa kisheria. sasa hivi AG nae ni mbunge. hii si sawa. tujifunze toka kwa wenzetu. huyo mbunge anaewakilisha walemavu wa ngozi hamna halilofanya zaidi ya kujiangalia yeye tu.
 
Tulipokuwa tunawaomba mfute viti maalum kuna watu walikuja jamvini na mapovu ya hasira na kusema tuna wivu na choyo. Mantiki ya viti maalum ni siasa za kizamani sasa hivi wanawake wakagombee ubunge. Vile vile watu wengine wagombee majimbo isipokuwa watu kama Mwanasheria mkuu, Rais wa zanzibar (kama huo muungano utaendelea) basi.

Mawaziri tunaomba waombe kazi na wasiwe wabunge kwani mgongano wa kimaslahi haifai. vile vile wabunge kuwemo katika mabodi ni mgongano wa kimaslahi. Rais asiwe na mamlaka ya kuteua viongozi wa mashirika ya umma na gavana bali wapendekezwe na wizara na kupigiwa kura na bunge ili wawe accountable bungeni na sisi tuwawajibishe wabunge wetu wakipoteza mwelekeo.

Vyenginevyo this system is full of corrupt bureaucrat!!!!
 
NYC unakwenda kinyume na lengo la mwenyekiti wako la kuongeza sketi mpaka kufikia 70% mjengoni ! na wewe NYC unatakiwa uvuliwe gamba nimekuona kuanzia mchakato wa katiba mpya
 
Wanadhalilisha bunge letu tu!Hawa ndio wanaofanya bunge letu lionekane kama ukumbi wa TAARAB.
 

Magodoro ya wakubwa hayo, Mtikila pamoja na wehu wake sometime huwa anaongea mambo ya msingi sana yule jamaa.
 
Katiba Mpya pia izuie Wabunge kuoana Kama ilivyotokea kwa Wazazi wako na Ubunge uwe na Kikomo kama Urais sio mpaka mtu anazeekea Bungeni kama Mzee Malecela.
Ungeanza na fair disclosure, kwamba wewe mwenyewe ni mbunge wa kupewa, ili tujue na kupima kwamba chochote utakachosema kinaweza kuwa na mgongano wa kimaslahi wa kutetea kitumbua chako.

Anyhow, binafsi sijui kama ni kweli wabunge wa kupewa bure ni vimada wa power brokers wa nchi, sina uhakika huo. Kwa mfano, sijui kama Shamsi Vuai Nahodha anananiliwa na Kikwete! Na tatizo langu sio whether wanaongea sense bungeni au ni watupu. Tatizo kubwa ni gharama, Bunge la nchi masikini inayopewa misaada kwa masharti ya ushoga haiihitaji wabunge 100 wa viti vya bure.

Kingine, wengi wa hawa huwa wanakuwa ni reject tayari mbele ya jamii. Regia wewe, kwa mfano,
wananchi wa Kilombero walikukataa halafu CHADEMA wakaku ram down our throats japo hatukutaki. Tuwafuteni.
 
Katiba Mpya pia izuie Wabunge kuoana Kama ilivyotokea kwa Wazazi wako na Ubunge uwe na Kikomo kama Urais sio mpaka mtu anazeekea Bungeni kama Mzee Malecela.

Mhhhhhhh! Madam Mtema I have respect for you and the people of Kilombero respect you. On this issue, i think you have gone astray. May be u need to say i am sorry to the guy, don't you think so? it could be you have your own reservation for the father of the guy, but attacking him in the way you have done, it does not show the positive side of your thinking and respect for private lives of others.

You have to say something on this to soothe the matter!
 
Katiba Mpya pia izuie Wabunge kuoana Kama ilivyotokea kwa Wazazi wako na Ubunge uwe na Kikomo kama Urais sio mpaka mtu anazeekea Bungeni kama Mzee Malecela.

Regia hii message yako naona kama haijakaa vizuri, ni rahisi sana mtu kuitafsiri kinyume na hasa ukizingatia kuwa swala la kuoa liko kwenye haki za binadamu zaidi.

Hata hivyo niseme tukiwa na katiba mpya yenye kumpa wananchi nguvu zaidi katima safu nzima ya uongozi/utawala basi hatuhitaji viti maalum. Kwa mfano kama wakuu wa mikoa, wilaya watachaguliwa na wananchi basi watawajibika kwa wananchi tofauti na ilivyo sasa ambavyo wanawajibika kwa rais aliyewapa kazi. Vivyo hivyo mkuu wa polisi, judge mkuu, mwanasheria mkuu wote n.k wote hawa ni wateule wa mtu mmoja - rais.

Tatizo la mfumo huu ni kwamba wakati wa uchaguzi viongozi wote hawa ambao wameteuliwa na rais wanafanya kazi ya kuchakachua kura ili mradi bosi arudi kazini vinginevyo hawana kazi. Lakini kama tungekuwa na mfumo wa kuwachagua watu hawa kwa vyovyote vile wasingefanya hayo ambayo wamekuwa wanafanya, na wewe mwenyewe Regia ni muhanga wa huu mkorogo. Hukutaka kuja bungeni kwa viti maalum na ndio maana ulipambana vikali lakini kwa bahati mbaya mfumo ulikuwa mbovu. Turekeshe yote hayo.
 
Katiba Mpya pia izuie Wabunge kuoana Kama ilivyotokea kwa Wazazi wako na Ubunge uwe na Kikomo kama Urais sio mpaka mtu anazeekea Bungeni kama Mzee Malecela.
NO wonder siasa za tz ni rotten,wewe public figure unakuja na rotten sweeping statements kama hizi. If i had been in PAWS place ungekula ban so that u regain your senses by knowing what to say in public
 

Zamani kabisa hawakuwepo ila walianza pale mambo ya beijing yalipoanza.Sasa sijui hii katiba ya zamani kama iliongezewa au ndo madaraka ya rais kuwa makubwa zaidi...
 
Katiba Mpya pia izuie Wabunge kuoana Kama ilivyotokea kwa Wazazi wako na Ubunge uwe na Kikomo kama Urais sio mpaka mtu anazeekea Bungeni kama Mzee Malecela.

Dada nimeshawahi kukuambia kwamba kwa staili unakua huna tofauti na watu wa CCM! Mara nyingi nimekuona hupendi kupewa chagamoto.

Ni kweli ubunge wa viti maalumu ni mzigo kwa taifa! Wewe ni viti maalumu kwa ajili ya nini na nani? Kwani Kilombero hawana mbunge? Ni kitu gani unachoweza kufanya mbunge wa jimbo Kilombero hasiweze kufanya kisheria na kitaratibu?

W.J. Malecela yupo sahihi katika hili (pengine suala la uhawara linaweza likawa si kweli!)
 
Unaweza ukawa sahihi. Viti maalumu viondolewe maana imekuwa kero machoni kwa watu na eti tunadai hatuoni kazi zao, moja kubwa ninaloomba tuwaunge mkono wakijitokeza kwenye uchaguzi maana tunatabia ya kuwadharau na kuwaona hawafai la sivyo, tutakuwa na wabunge wachache sana sana bungeni wanawake na sijui kama italeta picha nzuri.
 
NO wonder siasa za tz ni rotten,wewe public figure unakuja na rotten sweeping statements kama hizi. If i had been in PAWS place ungekula ban so that u regain your senses by knowing what to say in public

Huyu dada hapendi kupewa changamoto kabisa. Mara zote akipewa changamoto anatoa majibu ya namna hiyo. Anakua hana tofauti na serikali ya CCM ambayo inamwona yeyote anaikosoa na kuisema vibaya ni mwanachama au mfuasi wa CHADEMA.
Kama mpenda mabadiliko wa kweli, anapaswa kupokea changamoto zote kutoka upande wowote!
Au kwa kuwa maslahi yake yameguswa?!
 
no wonderkwenye ubunge wa kilombero alishindwa na of all people pedeshee MTEKETA
 
Reactions: Nzi

Picha nzuri kivipi? Kwa vile wao ni wanawake?! Ufike wakati watu (wanawake kwa wanaume) waingie bungeni kwa merits aisee. Kwaiyo kama ana uwezo wa kusimama jimboni na kuweza kuwashawishi wananchi kwamba anaweza, basi hakuna shida. Lakini hili la kutaka eti bunge lilete picha nzuri kwa kujaza wanawake ambao wanakua hawako worthy kuingia bungeni, haliko sawa hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…