Kiwi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 1,054
- 991
- Ni matumaini yangu makubwa sana kwamba kwenye katiba mpya, Tanzania TUTAONDOKANA NA Wabunge wa Bure na Viti maalum, I am sick na Bunge kujaa vimada wa Viongozi wa vyama vyetu vya siasa vyote kuanzia CCM mpaka Upinzani, ENOUGH! Wabunge wote wawe wa Majimbo tu Only Mwanasheria Mkuu ndiye aruhusiwe kuingia Bungeni na Cabinet bila kugombea jimbo!
- Taifa letu linapoteza Shillingi Billioni 90 kila miaka mitano on hawa Wabunge wa bure, that is insane kwa taifa masikini kama letu.
Much Respect People!
William @ NYC, USA: Le Mutuz Baharia!
Naungana na wajumbe wengine kuendelea kushangaa kuwa haya maneno unayaandika wewe kweli au ni mtu mwingine anayetumia jina lako humu jamvini.
Binafsi nilishawahi kuwahoji wabunge wa viti maalum nilipopata nafasi ya kukutana nao ana kwa ana, na kuwauliza wanafanya nini bungeni, wanamwakilisha nani, na nini faida ya wao kuwepo bungeni kwa wananchi. Hawakulipenda swali langu. Kwa kifupi niliwaambia ya kuwa binafsi sioni kazi wanayoifanya na ningekuwa nina uwezo wa kubadilisha katiba hivyo viti maalum ningeviondoa. Kwa kuwa sasa tuko kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya (?) ni vizuri hilo wazo ulilolitoa likatiliwa mkazo.
Ingawa sina hakika kama kwa mwendo tulionao na kwa kuburuzwa tunakokuona tutafikia mahali pa kusema tunaandika katiba mpya! Labda kwa maandamano na migomo, lakini siyo kwa bunge la vijembe!