wewe viti maalum hawateuliwa na rais . wabunge viti maalum wanachaguliwa na wajumbe wa uwt mkoa mzima. kila kata inatoa wajumbe watano : mwenyekiti uwt kata, katibu uwt kata,mjumbe wa mkutano mkuu uwt mkoa. katibu mhasishaji . kila kata wajumbe hao hukutana mkoani wanapiga kura kupata mbunge. hiyo ni hatua ya kwanza , lakinj hatua ya pili inaangaliwa idadi ya wabunge wa majimbo ambao chama kimepata inatafutwa asilimia ndipo tume wanapokuja na jibu la idadi ya wabunge kwa kila chama. halafu baadae ikishatoka idadi ya wabunge kwa kila chama ndipo wale walio shinda mikoani wanaitwa na kuambiwa . Kwa mfano kama wabunge walio chaguliwa ni wengi na chama kimepata nafasi chache chama kinaandaa utaratibu wa kupunguzana wenyewe ili kupata idadi sahihi inayohitajika na tume ya taifa ya uchaguzi . mfano kwa ccm katika uchaguzi wa 2005 ccm walikuwa na wabunge wengi wa majimbo hivyo wakapata wabunge wengi wa viti maalum lakini 2010 walipoteza majimbo mengi hivyo ikabidi idadi ya wabunge wa ccm wa viti maalum ipungue toka 92 hadi 60 , na wakati wao ccm waliandaa wabunge 92 wa viti maalum wakijua watapata majimbo mengi , matokeo yake ikabidi chama kiwapunguze hadi 60. na utaratibu ulio tumika ulikuwa ni kuandika namba vikaratas hadi 92 na kuvitupa chini na kila mbunge akitakiwa kuokota na aliyeokota 1-60 ndiye aliyepita na aliyeokota 61-92 aliondolewa . kwa hiyo nafas 22 za wabunge viti maalum wakapewa chadema . huo ni utaratibu ndanj ya ccm , kila chama kina utaratibu wake , wao chadema kila mbunge mwanamke aliyegombea kwenye jimbo na akashindwa ndio walio pewa nafasi za viti maalumu. kwa chadema sharti ugombee jimboni ukishindwa unapewa viti maalum . kigezo cha ushindan wao ni idadi ya kura ulizopata jimboni kwako. na uchaguzi wao ni tarehe 2/8 kama sikosei