USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

"Makengeza" akikudinya tu ubunge maalum unaupata kupitia chama chao cha kifamilia.
 
wewe viti maalum hawateuliwa na rais . wabunge viti maalum wanachaguliwa na wajumbe wa uwt mkoa mzima. kila kata inatoa wajumbe watano : mwenyekiti uwt kata, katibu uwt kata,mjumbe wa mkutano mkuu uwt mkoa. katibu mhasishaji . kila kata wajumbe hao hukutana mkoani wanapiga kura kupata mbunge. hiyo ni hatua ya kwanza , lakinj hatua ya pili inaangaliwa idadi ya wabunge wa majimbo ambao chama kimepata inatafutwa asilimia ndipo tume wanapokuja na jibu la idadi ya wabunge kwa kila chama. halafu baadae ikishatoka idadi ya wabunge kwa kila chama ndipo wale walio shinda mikoani wanaitwa na kuambiwa . Kwa mfano kama wabunge walio chaguliwa ni wengi na chama kimepata nafasi chache chama kinaandaa utaratibu wa kupunguzana wenyewe ili kupata idadi sahihi inayohitajika na tume ya taifa ya uchaguzi . mfano kwa ccm katika uchaguzi wa 2005 ccm walikuwa na wabunge wengi wa majimbo hivyo wakapata wabunge wengi wa viti maalum lakini 2010 walipoteza majimbo mengi hivyo ikabidi idadi ya wabunge wa ccm wa viti maalum ipungue toka 92 hadi 60 , na wakati wao ccm waliandaa wabunge 92 wa viti maalum wakijua watapata majimbo mengi , matokeo yake ikabidi chama kiwapunguze hadi 60. na utaratibu ulio tumika ulikuwa ni kuandika namba vikaratas hadi 92 na kuvitupa chini na kila mbunge akitakiwa kuokota na aliyeokota 1-60 ndiye aliyepita na aliyeokota 61-92 aliondolewa . kwa hiyo nafas 22 za wabunge viti maalum wakapewa chadema . huo ni utaratibu ndanj ya ccm , kila chama kina utaratibu wake , wao chadema kila mbunge mwanamke aliyegombea kwenye jimbo na akashindwa ndio walio pewa nafasi za viti maalumu. kwa chadema sharti ugombee jimboni ukishindwa unapewa viti maalum . kigezo cha ushindan wao ni idadi ya kura ulizopata jimboni kwako. na uchaguzi wao ni tarehe 2/8 kama sikosei
kwa nilivokuelewa mkiwa na majimbo mengi ndvyo na vti maalum vnavozdi kuwa vingi na kwamba idadi ya majimbo mlopata ndo inalimit idad ya vt maalum... Mkuu em fafanua uwt ni nn??
 
Ballac

Kitega Uchumi Chako Cha Asili Na Ulichojaaliwa Na Mwenyezi Mungu Ambacho Hakihamishiki Tokea Unazaliwa Unaoa / Kuolewa Hadi Kufa!
 
Last edited by a moderator:
Wana JF,

Ubunge wa Viti maalum unatakiwa uongezewe vigezo vya kutosha kuchagua mtu sahihi bila upendeleo wa zawadi kutoka kwa wanaochagua, kumbuka viti hivi vya upendeleo vinatugharimu sana, na ukiangalia azima ya kuwepo ni kwa ajiri ya huruma ya upendeleo kwa kina mama ambao kwa kufikiria tanzania tuna mfumo dume ambao wanawake hawawezi kupenya wenyewe bila kuwezeshwa.

Viti hivi sana sana vinaendena na dhama ya kiukoo kwa vyama vyote yaani vya upinzani na chama tawala, kupitia viti hivi huwa kuna mihemuko mingi sana na ushabiki wa hovyo hovyo bungeni kwa kuwa jamii ya watu hawa waliopendelewa hawana cha kupoteza, inatakiwa wawe na mvuto wa kutosha waliouonyesha jamii kuwa ni watetezi wakweli, sio wale wanaotetea matumbo ya viongozi wao ndio wanapeta kwa kuwa kazi yao ni kujikomba kwa viongozi mwanzo mwisho.
 
Salaam wadau,

Naombeni kufahamishwa ni namna gani wabunge wa viti maalum kwa kila chama wanavyopatikana.Pia na vigezo wanavyovitumia,asante.
 
Kura alizopata rais zinachangia kwa asilimia nyingi upatikanaji wa wabunge wa viti maalumu. Hilo ndilo ninalojua
 
Usiwe mvivu wa kufikiri, jinga weee!!! Hata ku-google huwezi!!!
 
Humu ndani mijitu mingine haipitii thread nyingine yanaibuka tu na miswali yao
 
Salaam wadau,

Naombeni kufahamishwa ni namna gani wabunge wa viti maalum kwa kila chama wanavyopatikana.Pia na vigezo wanavyovitumia,asante.

Najua Tu Kuhusu Wa CCM Ambao Kwanza Wanatakiwa Wawe Na GPA Kubwa, Masters Degree au PhD, Akili ZILIZOTUKUKA, Ushawishi, Wasio Wanafiki Na Wagomaji Bila Kusahau Wawe Na Mvuto Mkubwa Sana Machoni Mwa Watu Huku Bila Kusahau AFYA Zao Zisiwe Na Mgogoro. Kwa Ndugu Zetu Wa UPANDE Wa Pili " WAGOMAJI, WASANII Na WASUSAJI Camp " Ni Kinyume Za SIFA Hizo Za CCM Mkuu. Nadhani Kidogo Sasa Nitakuwa Nimekufumbua Macho Na Karibu Ujiunge Na CCM Ili Ukaribie Paradiso.
 
Kura za rais lkn pia idadi ya wabunge mpendwa tupo kwa ajili ya kulijenga taifa letu la Tanzania
 
Nachukua nafasi hii kukishauri Chama cha Mapinduzi CCM Kwa kuwa Mwenyekiti wake anajinadi kuwa CCM ni ya Wanyonge Chama hicho kipendekeze Viti Maalumu vya Wabunge Na Madiwani VIFUTWE ili fedha zipelekwe Kwa Wanyonge ambao CCM imekuwa inawapigania miaka nenda miaka rudi wananchi wake bado Na wanazidi kuwa Wanyonge.
 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa nafasi za Wabunge wa Viti Maalum wanaoteuliwa zipo kwa mujibu wa Sheria na zimeainishwa katika Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amesema kuwa Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba inaeleza utaratibu mzima wa kuwapata Wabunge wanawake wa Viti maalum.

Amesema kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu na kupata angalau asilimia 5 ya Kura zote halali za wabunge kitapata Wabunge wa Viti Maalum kulingana na Kura kilizopata

Amefafanua kuwa Chama kinachopata asilimia 5 ya Kura zote halali za Wabunge katika Uchaguzi Mkuu kinatakiwa kuwasilisha orodha ya majina ya wanachama kinaowapendekeza kuwa wagombea wa Viti Maalum katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Aidha, ameeleza kuwa endapo inatokea nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu mbalimbali, Spika wa Bunge humtaarifu Mwenyekiti wa Tume juu ya uwepo wa nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343

Amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume hukiandikia barua chama husika kukitaarifu juu ya uwepo wa nafasi wazi ya viti maalum ili kiweze kuwasilisha pendekezo la jina katika orodha kiliyowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015, ikiambatanishwa na Fomu namba 8 D ya kuomba jina lililopendekezwa liteuliwe na Tume katika nafasi ya Ubunge kulingana na vigezo vilivyoainishwa.
 
Back
Top Bottom