JF Igolya!
Ndugu zangu Ibara ya 66 (1) na Ibara ya 78 ya Katiba ya JMT, 1977 na kifungu Cha 86A Cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343, vinatambua uwepo wa Wabunge Wanawake wa Viti Maalum wasiopungua asilimia 30 ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, Serikali iliamua kufanya uamzi wa kuongeza idadi hiyo kutoka asilimia 30 hadi kufikia asilimia 40 ya Wabunge wote wa Bunge la JMT.
Ni jambo zuri, kwani linakusudia kuongeza nafasi na fursa kwa wanawake katika vyombo vya maamzi.
Asilimia 40, kwa Sasa ni sawa na Wabunge Wanawake wa Viti Maalum 113, ambapo CCM ina Wabunge 66, CHADEMA 37, CUF 10.
Vyama vingine havikubahatika kupata baada ya kukosa walau asilimia 5 ya kura zote halali kwa mujibu wa ibara 78 (1) ya Katiba ya JMT, 1977.
*Swali langu*
Hivi viti ni kwa ajili kuongeza ufanisi pale bungeni, au just utekelezaji wa dhana ya usawa wa kijinsia?
Hizi hela wanazopewa bure bure hizi haziwezi kusaidia kuwatoa Wanafunzi kuandikia chini, na hatimae wapate madawati?
Kuna mjumbe mmoja humu JF alilalamika kuwa alikuwa anarubuniwa kuwa atapewa nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum, kama Chama kitapata fursa hiyo pale atakapokuwa ameondoa chupi yake mwilini? Hapa inaonyesha kuwa Kuna wabunge wanaingia bungeni kwa kutumia mbinu hii!- Siwafahamu lakini pia inawez kuwa ni dhana tu.
Lakn swali langu linabaki palepale, hawa ndugu zetu hawa 113, Wana tija yoyote kwa Taifa, au ndo tunaongeza tu matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa Taifa? Kwa nn watu wasichuane majimboni, maana uwanja uko huru, haubagui mwanamke Wala mwanume.
Akisinzia bungeni akahojiwe, lkn huyu kiti Maalum hawajibiki kwa mwananchi yeyote.
Nawasilisha kwa mjadala.
Lugumya.
Sent using
Jamii Forums mobile app