Mtoa mada ana wazo na jicho zuri sana, hebu tumia akili yako ya ndani kuitafakari kauli yake, ukilizoom vizuri hilo wazo lake la kununua nyumba kwa 1M najua hamaanishi hivyo kama wengi mlivyoichukulia moja kwa moja.
Mfano mzuri ameutoa hapo kwamba kipindi cha nyuma alitumia akili zaidi ya kuona mbele kuhusiana na kwenda chuo au ajira na hatimaye leo amekaa pazuri, mi naona kikubwa anachomaanisha ni kwamba baada ya korona kuisha kuna watu watakua na hela nyingii kuliko kawaida (hapo tumia akili sasa) na kuna wengine ambao watakua makapuku kabisa kuliko mwanzo kitendo kitachopelekea kuweza kupata vitu vizuri na vikubwa kwa bei chee than before.
Imagine una nyumba na ni mtumishi sekta binafsi, baada ya msoto wa korona ulipunguzwa kazini au uliambiwa kwa kipindi hichi chote hutolipwa (kama ndugu zetu wa tusiime wale) na korona imetupiga kwa miezi nane mpk tisa, baada ya korona kuisha hukurudishwa kazin, michongo yoote inaanza upya from default setting hapo akilini kichwani ndugu utatuuzia tu hiyo nyumba kwa bei yetu.
Kuna wale wakulungwa waliochukua mkopo akanunua passo akampa mwana aendeshe uba, due to lock down hamna wateja gari wamekurudishia, kodi walikuambia utalipa afta lock down na kazini ulipunguzwa, mpwa tutanunua tu kwa laki tano hicho kipaso chetu..
Kuna wale pangu pakavu, ambao forever and always hawanaga tu mambo ya akiba iwe from mshahara au kipato chochote, wewe ni ''pata tumia mpk mwisho'', leo hatujaanza vizuri lockdown huna hata mia unasubiri Alhamis hapo ukasubiri pale atm za nmb, je Sponsor mwenye Nchi yake akitia neno kamili kwamba wote tujifungie.... sijui utatuuzia nini hapo baadae.
Kwahyo ni kipindi flani hivi ambacho mawimbi yake sio ya kitoto, tumia akili yako kabisa ile ya ndani kuhakikisha during this corona season and even afta hata kama hautakua jabali ila umake sure unatoboa katika hii natural selection.
Mtoa mada 0yee✊