Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Mkuu umenena kweli
 
Umeomba msaada lakini hujatufungukia vizuri hivo itakuwa ngumu mtu kukushauri nini ufanye ili upate kuwa mpya 2018

Inatakiwa ueleze how much you have so itakuwa vyepesi mtu kuku shauri nini ufanye kutokana na kiasi ulichonacho vinginevyo utapewa pole tu.
 
Naomba niongezeee kidogo,hakuna ndugu anayetaka Ndugu yake afanikiwe kimaisha bora mtu baki anaweza kukusadia ukatoka kimasha sio Ndugu.
Hili Mi nakataa inategemea na malezi yenu tokea udogoni km mlilelewa kwa upendo Wa kupendana nyinyi kwa nyinyi mtasaidiana tu! Ni mifano kbao ya ndugu walioshikana mikono mpk wakatusua
 
30miaka bado hujachelewa anza hata na mtaji wa laki moja,usichague kazi mwaka mmoja tu ukitulia mabadiliko utayaona ila uvumilivu ndio siraha namba moja
 
Umesema unafanya shughuli ndogo ndogo zinazokusaidia kulipa kodi, ni shughuli zipi hizo na mtaji wake ni kiasi gani? Tunaweza kushauriana namna ya kupanua hizo hizo shughuli zako ndogo na zikawa kubwa
Naomba unisaidie Mimi mawazo mkuu
 
Pole sana ndugu yangu, ila kanuni ya waliowengi iliyopelekea wakafanikiwa ni mbili tu
1. Spend less, save more
2. Invest wat u ar willing to lose
Nilijarib and it works
 
Acha kuifikiria degree yako, kufanya hivyo inakuZuwia kujitoa kwa hicho kidogo unacho kifanya kwa kuwa unafanya kwa kungojea matunda ya degree. Wapo wasio na degree lakini kuna sehem nao walikosea na kupotea muda na pesa. Umri wako sio mkubwa na unabahati ya kuwa na degree ambayo inakupa kiburi cha kujilipua kwa ku take risk kibiashara kwakua unajia unapo pa kuegemea. weka vyeti kabatini wala hakuna anye kujua kama wewe ni msomi, jichanganye na hao std IV fanya nao kaZi huku ukitumia upe wa Degree. Sikupi pole bali nakutia Moyo, bado mapema usivute shuka, bado mapema fungua macho .
 
Kati ya watu usiotakiwa tegemea ni
Ndugu (Tumbo Moja au W Mbali)
Familia
Marafiki

Ukiwategemea Hawa utakufa masikini, hata wawe nacho hawawezi kukusaidia zaidi watapenda uwe hivyo ili uwaheshimu
ni kama umenigusa na mm yaani ndugu wanataka uwatetemekee wao hawakusaidii kitu
 
Maneno yako yamenigusa sana kiongozi.

Pole sana.
 
Aika mleu oko
 
Mwanangu amka acha kulialia kunja roho kunjua sura tafuta network mjini wanaojua kusoma ramani, kuna maboya town wanamiliki hela nyingi tunawachukuliaga tu kwani nn? Umasikini unatesa sana usikubari kuishi kinyonge ni bora kuishi muda mfupi wenye raha kuliko miaka mingi ya shida na dharau, kila mtu mjini ni hustler hata yule pastor wako anakuthamini kutokana na kiwango chako cha sadaka.
 
kuni unauzia wapi mkuu?? nna shamba langu maeneo ya vigwaza nlitaka kukata miti nichome mkaa ila mlolongo nlopewa huko maliasili ilibid niweke pause kwanza,,vibali ulipataje??
 
Ni ukweli usiopingika kuwa ukisoma saana unapishana na hela.
 
Nakushauri, ufanye kazi hapo kwa malengo. Hao hawatakuja kukulipa vizuri kama unavyotaka, na kwamba wanafanya hivo ili uendelee kupiga kazi kwao huku ukipiga kiaina.

Kuna usemi unasema kwamba "ili uweze kupiga hatua/kufanikiwa haijarishi unapata Shilingi ngapi bali unaweka akiba Shilingi ngapi".

Nakushauri, uanzishe vijimradi vidogo vidogo vidogo vidogo kama vile kutengeneza na kuuza "ice cream" na ubuyu, Mpesa, kuuza vocha za jumla, nakadhalika. Vijimradi hivi vitakujengea uwezo wa kutokuwa mtumwa/tegemezi kwa hao hajamaa 100%. Naukisha simama unasepa ili kujipa muda wa kutosha kusimamia mijimradi vyako.

Nikutowe wasiwasi, kwanza hujachelewa kutusua, pili siyo kweli kwamba ili uanzishe biashara lazima uwe na mtaji mkubwa kama unavyodhani. Wengi waliotusua walianza na mitaji kiduchu muno ila walikuwa na malengo ya kufika mbali na walisimamia vema biashara zao.

Nakushauri uanze na hicho kidogo unachopata kwa kuanza na kijimradi kulingana kipato/uwezo wako. Cha msingi hakikisha unasimamia mwenyewe kwani ndiyo siri ya mafanikio ktk biashara yoyote iwe kubwa/ndogo.

Ni hayo tu....
 
Pole sana bro unanikumbusha mbaaaaali na huwa nasema cku zote km mm nimefanikiwa kupata jpo pakupunguzia ukali wa jua bc naamini hata ninyi mnaosota ss hv ipo cku yenu hakuna kukata tamaa ktk watu walikuwa na nyota ngumu ni mm 5 years nazurula tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…