Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Tatizo limeanzia pale kwenye kitu wanaita " mindset". Kwakweli tuwapo huko mashuleni pamoja na hamasa za wazazi, ndugu na jamaa, wote walituaminisha nasi tukajiaminisha kuwa kusoma ndio kufanikiwa. Lakini kumbe kusoma na kufanikiwa ni vitu viwili vinavyotegemeana ila visivyofanana.

Kama ujuavyo kuwa tunatumia muda mwingi wa kusoma yaani tangu "vidudu" hadi Chuo ambapo si chini ya miaka 15 mpaka kuhitimu.

Sasa hawa ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wakitupa moyo wa kukazana kusoma kwa miaka zaidi ya 15, walisahau kama tunatakiwa kupewa pia moyo huo huo wa kuyatafuta mafanikio kwa kujipa miaka mingine kadhaa, mana mafanikio si lelemama.

Ushauri wangu ni kuwa, umemaliza hatua ya kwanza ya kuelekea mafanikio ambayo ni kusoma, hivyo unaelekea hatua nyingine isiyokuwa na uhakika wa lini utaikamilisha, hivyo jipe moyo kuwa bado unaendelea na mapambano.

Ukishajipa matumaini wewe mwenyewe, mimi nakushauri haya yafuatayo.

Kwanza kabisa ondoa kichwani mwako kinachoitwa Degree wala Postgraduate, kisha fanya chochote kinachoweza kukuingizia kipato huku ukitumia elimu yako kuweka malengo mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu. Jenga akilini mwako kuwa mafanikio ni mchakato wa muda mrefu na si muda mfupi, huku ukiendelea kusimamia malengo yako ya muda mfupi na muda mrefu.

Anza na hata mtaji wa 50,000. Fanya chochote iwe kubrush viatu, kuchoma mahindi mtaani, kuosha magari, kuuza matunda n.k. Hizi kazi huonekana kama za watu waliokata tamaa na maisha lakini nikuhakikishie kuwa endapo utakuwa na malengo ya muda mrefu na muda mfupi haitakuchukua zaidi ya mwaka mmoja kupiga hatu. Kuliko kubaki na degree yako mfukoni na kubakia ukilia lia, nakushauri uanze kuchukua hatua sasa.Huu ni ushauri wangu si lazima uukubali kwani ushauri hukubalika au kukataliwa kulingana na mpokeaji. Ahsante.

Ukiona ushauri huu ni muhimu kwako na ukahitaji kuutekeleza ila changamoto ikawa ni mazingira unayoishi, nakushauri uondoke katika mazingira hayo uliyozoea kuishi na kwenda mahala kwingine utakakoweza kitekeleza bila kuwa na fikra za flani na flani watanionaje..
 
Umenena vyema.

Anachokipitia jamaa, watu wengi wanapitia ikiwemo mimi.


Alichokisema, nimekipitia.


Nilidharauliwa kwa umasikini wangu japo ni digrii, ila sasa ninaheshimika eti kwa pesa zangu, na sasa wananipiga mizinga, japo sina pesa kihivyo.


Ndugu, marafiki, wengi ni wanafiki tu.
Mbinu gani ulitumia kutoka kimaisha brother??
Tugusie kidogo tu ulianzaje ili na wengine wajipange kuwa muwazi maana nimesoma hizo post nikawasikitika sana watanzania wenzangu
 
I feel you brother. Umejizungumzia wewe kama umenizungumzia mimi na hii BAEd yangu inanifanya najichukia na kujutia muda niliopoteza chuoni. Naelekea kukata tamaa kabisa .Eee mola nisaidie [emoji24] [emoji24]
....The biggest mistake in life is to give up, don't you ever give up...pambana mpaka unaingia kaburini
 
Yaan mkuu una akil sna , hakika halio ndo hali halisi haswa

Nina kaka angu yupo uk hapa bongo ana majumba hayana idadi
Ma eka ya mashamba had mengine hayajui

Ila kumseidia mtu shida yaan kukupa kamtaj hawez labda sh 10000 ili sku yapili umuombe tena aone huwezi ishi bila yeye nikaona. Bora nijiongeze saiv sina habar nae kabisa japo km ni kaka baba mmoja ma mmoja ila sina mawasiliano nae tena nafanya yangu

Jaman chonde chonde msitegemee vya ndugu mtakufa masikini
Safi kabisa..ndugu sio wa kutegemewa
bora hata anayepewa elf 10..mwingine anakununulia bia kunywa tani yako lakin kitu cha kukusaidia maisha yako thubutu
 
Yaan mkuu una akil sna , hakika halio ndo hali halisi haswa

Nina kaka angu yupo uk hapa bongo ana majumba hayana idadi
Ma eka ya mashamba had mengine hayajui

Ila kumseidia mtu shida yaan kukupa kamtaj hawez labda sh 10000 ili sku yapili umuombe tena aone huwezi ishi bila yeye nikaona. Bora nijiongeze saiv sina habar nae kabisa japo km ni kaka baba mmoja ma mmoja ila sina mawasiliano nae tena nafanya yangu

Jaman chonde chonde msitegemee vya ndugu mtakufa masikini
Safi kabisa..ndugu sio wa kutegemewa
bora hata anayepewa elf 10..mwingine anakununulia bia kunywa tani yako lakin kitu cha kukusaidia maisha yako thubutu
 
Salaam wanajamvi,

Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.

Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.

Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.

Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.

Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.

Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.

Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.

Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.

Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.

Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.

Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.

Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.

NAWASILISHA
Me nakushaur ujikite ktk bsness ...me n former teacher nmefundsha English medium kadhaa hapa dar Nina miaka 24 nmeacha kaz mapema mwaka huu na nmejiajir Nina vibal toka maliasili ninauza kuni znalipa sana ......ila ka hauna mtaj kabisa nakushaue ebu hangaika upate jpo lak nne ...uanze kwenda kwa wakulima wa Mihogo ununue kwa kuanzia robo eka then unaenda kuuza sokon ...aidha mwenyew au kuptia madalali .......au unawzann cha kufanya ....jipange jiamin kuwa jasir ur the best mambo yanawezekana
 
Mbinu gani ulitumia kutoka kimaisha brother??
Tugusie kidogo tu ulianzaje ili na wengine wajipange kuwa muwazi maana nimesoma hizo post nikawasikitika sana watanzania wenzangu


Siri ni kupambana, usichague kazi...Baada ya digrii niliwahi kulima mboga kwa mtaji wa jero tu, pia niliwahi kuchimba msingi wa nyumba, kuhamisha kifusi, na kupalilia mashamba, ni kutokana na hulka hiyo, nimeweza kupanda juu na sasa ninapumua kwa furaha.

Kifupi ndiyo hivyo.


mwakani nimepanga kununua ardhi na nianze kujenga....


Nilichekwa, kudhalilika, kuzodolewa ila sikujali maana nilijua lengo langu ni nini, ninataka nitoke, na ndiyo hivyo ninatoka tu
 
Pole sana mkuu ila usisikitike sana na nikupe angalizo moja: ni kweli kuna vijana wana assets kama magari na nyumba ila thamani halisi (net assets) ni ndogo au negative maana wana mikopo balaa.

Changamoto yako iwe chachu ya kutafuta wazo la biashara au ujasiriamali alafu washirikishe watu wa karibu akiwemo mzazi mwenzio siku za usoni utafanikiwa na kuwazidi masharobaro wa mjini.
 
Back
Top Bottom