Ushauri unahitajika: Je, nimueleze kama Mama yake Kafariki?

Ushauri unahitajika: Je, nimueleze kama Mama yake Kafariki?

Usimwambie kwa sasa wacha afikishe maisha ya kuanza kujitegemea miala 17 bado ni mdogo sana ..
Mwache asikie kwa watu lakini si kwamwambia wewe..
Watu kama hao wakifanikiwa huwa wanakumbuka sana walezi wao kuliko hata watoto wako wakuzaa mwenyewe..


Sent from my SHV-E250S using JamiiForums mobile app
 
NO!, wewe ndio mzazi, kama umebeba miaka yote hiyo, usimwambie atakua na amani sana kuliko ukimwambia

Sent from my LG-H635 using JamiiForums mobile app
 
Labda marudio lkn tiar ukweli anaujua.... Miaka 17 si mchezo, labda km huishi na majirani

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Kama kinakusumbua ndani ya moyo wako na unaamini ukimwambia utapata amani mwambie. Otherwise hakuna ulazima.
 
Swali la kujiuliza ni hili; Kwa nini unataka kumueleza?? Amekuwa akikuuliza kuwa je wewe ni mama yangu au?? Na kama kakuuliza, ni kitu gani kilimfanya akakuuliza hilo swali??
Angalia, kama ungelikuwa unamfanyia hiana asingelifikia umri huu bila kujua ukweli. Yeye amekujua kama mama yake imetosha. Humdai malipo ya kumtunza, humkatai katika uzee wake, sasa kinachokufanya umwambie kuwa weye sio mamake ni kitu gani??
Kama wakiitwa wazazi wake tangu akiwa mdogo si ni wewe ulienda?? Mbona unakuja kataa mtoto wako uzeeni? Acha kabisa hayo maneno unayotaka kumhuzunisha nayo. Sio mazuri
Nimependa huu ushauri
 
Swali la kujiuliza ni hili; Kwa nini unataka kumueleza?? Amekuwa akikuuliza kuwa je wewe ni mama yangu au?? Na kama kakuuliza, ni kitu gani kilimfanya akakuuliza hilo swali??
Angalia, kama ungelikuwa unamfanyia hiana asingelifikia umri huu bila kujua ukweli. Yeye amekujua kama mama yake imetosha. Humdai malipo ya kumtunza, humkatai katika uzee wake, sasa kinachokufanya umwambie kuwa weye sio mamake ni kitu gani??
Kama wakiitwa wazazi wake tangu akiwa mdogo si ni wewe ulienda?? Mbona unakuja kataa mtoto wako uzeeni? Acha kabisa hayo maneno unayotaka kumhuzunisha nayo. Sio mazuri
Hajawi kuniuliza ndio maana nikataka ushauri nifanyeje.
 
Me kabla ya ushauri naswali
Je babake yuko wapi?
Hilo swali na mtoto ndo atakaloanza kukuliza kwa kuwa anajua wewe ndo mamake

Sent from my Infinix-X600 using JamiiForums mobile app
Hatujui baba ake alipo alitelekezwa tangu yupo tumboni. Na marehemu mama yale tulimsihi amtaje baba wa mtoto hata kama kaikataa mimba Jibu lilikuwa Baba ake amefariki.
 
Ni Ngumu kumwambia ukweli na kama kuna mapenzi mema kati yenu hata akisikia huko nje atajua ni kwanini ulifanya vile.
 
Kuna msemo unasema hakuna siri duniani,
Hii yaweza ikawa ni kweli lakini kwa ushauri mzuri mimi nafikiri ungemuacha kwa miaka kadhaa akifikia umri wa kujielewa na kuamua kufanya maamuzi sahihi, endelea kuwa naye kwa upendo na mlee vyema nafikiri akifikisha umri wa miaka 23 mpala 25 ndio inaweza kumuambia ukweli ili hali naamini atakuwa anajitegemea na kufanya maamuzi sahihi katika maisha yake, kwa sasa bado ni mdogo kiakili itaweza muathiri kisaikolojia, mwambie ukweli na sababu tofauti tofauti kwa lugha nyepesi tulivu. Hakika atakuelewa na kukushukuru kwa mchango wake mkubwa wa kumlea, kwa wewe atakuwa ni zaidi ya mama kwake, atakuthamini na kukupenda kukuzidishia upendo maradufu kwako.
Mungu akubariki pia na wewe kwa kujitolea kulea mtoto wa mwenzio hakika sio jambo jepesi lakini Mungu amekusaidia umeweza kufanya hayo yote. Ni baraka tosha kwa Mwenyezi Mungu.
 
Nakuomba usubirii muda muafaka

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kuna mdogo wangu alifariki akaacha mtoto wa miezi 3 mwaka 2000 yule mtoto akalelewa na Mama alipofikisha miez 8 akachukuliwa na Mdogo wangu wa mwisho akaishi nae alipofikisha mwakana nusu yule mdogo wangu nae akafariki , nikamchukua mimi kumlea mpaka sasa anajua mimi ndiye mama yake wa kumzaa , Mpaka sasa ana umri wa miaka 17, hajui kama mama yake amefariki. Je nimuache au nimueleze ukweli kwamba yeye ni Yatima hana wazazi.

wanaambiawaga wakifika miaka 15 - 18 .... huu ndo mda wa kumwambia, wala sio ngumu, ni rahisi tu, muwe kwenye mazingira mazuri tu na awe na moody nzuri.
 
Akija kusikia kwa watu atakuchukia sana,believe me!!.......ni heri umwambie sasa hivi!!

Sent from my Armor using JamiiForums mobile app
 
Piga kimya, usimwambie maisha yaendelee... ukimwambia athari zake 1. Kuishi maisha ya upweke na simanzi maishani mwake. Na kusema bola na yeye angefariki, n.k

Usimwambie kabsa na hakuna jirani au mtu mwingne ataweza kwambia na bint akaamini.

Sent from my EVA-L19 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom