Ushauri unahitajika: Je, nimueleze kama Mama yake Kafariki?

Ushauri unahitajika: Je, nimueleze kama Mama yake Kafariki?

Hajawi kuniuliza ndio maana nikataka ushauri nifanyeje.

Kwa kuwa hajawahi kukuuliza, na kule kwa babake hawajawahi kuja kuuliza mtoto wao, na sidhani kama ana urithi wowote kule kwao, basi huyo ni mtoto wako wa kuzaa kabisaa kihalali japo hukuenda leba kujifungua.
Mwache mtoto wako usimpe kidonda cha moyo. Tulia tu, akishapata cheo serekalini, akiwa waziri wa view wonders utaona kidudu mtu akija kukuambia huyo ni mwanangu. Wewe usibishane naye, mwache huyo mtoto amjibu wala usimjibu. Ka mtoto akikuuliza muulize kuwa ameona upungufu gani kwako hata akaona kuwa wewe sio mamake.
 
hakuna haja yoyote ya kumwambia, mdau kwenye post namba 8 amemaliza kila kitu, na endapo akija kujua huko mbele utamwambia ww hujaona tofauti ya mamaake mzaz na ww mana wote ni wazazi tu
 
Usimueleze chochote,huyo nimwanao ambae mungu kakupa mwenyewe,kufa na hiyo siri,utampa mawazo sana, na kumsumbua kisaikologia kutafuta sura ya mama mzazi,na kwanza haina faida yoyote,ataanza kukuona mbaya kwa mapungufu yaliyojitokeza kwenye malezi yake,

Sent from my CAM-L21 using JamiiForums mobile app
 
Hajawi kuniuliza ndio maana nikataka ushauri nifanyeje.
Sioni sababu kwa nn umwambie hakuna anayekudai umwambie, unatafuta umsababishie huzuni isiyo na sababu, ikitokea akajua mwenyewe kazi yako itakuwa ni kuthibitisha tu ukweli. Lakini kuanza tu kumwambia tu from nowhere haifai. Unamwabia ili iweje,?

Sent from my Galaxy A 9(2017) using JamiiForums mobile app
 
Akija kusikia kwa watu atakuchukia sana,believe me!!.......ni heri umwambie sasa hivi!!

Sent from my Armor using JamiiForums mobile app
Amchukie kwa kutomwambia kuwa yy hakuwa mzazi wake, hakuna kitu kama hicho. Labda kama wazazi wake wangekuwa hai halafu asimwabie hapo ingekuwa tatizo. Lakini wazazi hawapo na baba ndo alikimbia toka hajazaliwa atamchukia kwa lipi?

Sent from my Galaxy A 9(2017) using JamiiForums mobile app
 
Subili afikishe angalau 20 na kama anasoma subiri kwanza na inabidi uweke mazingira yakumwambia na kama una watoto wengine usiwambie mwambiye yeye tu ili asije baguliwa

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Hongera kwa malezi mn ungekuwa na malezi ya kibaguzi naamini angeshajua ukweli. By then huenda alishaambiwa na watu ila hajakushirikisha tu.

Nakushauri nikiwa na akili timamu isiyo na shaka kuwa usimwambie kabisaaa mwache ajue wewe ndie mamake, nasema hivi kwa sababu ukimwambia huenda kuna siku ulimpiga akiwa hajui kosa hivyo ukimwambia atarudi nyuma na kusema ndo maana naonewa au nilionewa kumbe sio mamangu.

Usimwambie na endelee kumlea katika njia zimpendezazo mungu watu

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app

Weweeee lazima ukweli ubaki palepale na mtoto anapaswa kujua....
 
Haina haja ya mtu kuujua kila ukweli... We muache muache kwanza siku muafaka ikifika atajua tu...
 
Hatujui baba ake alipo alitelekezwa tangu yupo tumboni. Na marehemu mama yale tulimsihi amtaje baba wa mtoto hata kama kaikataa mimba Jibu lilikuwa Baba ake amefariki.
Pole sana ila acha akue zaidi ya hapo ndo umwambie ila muombe Mungu sana isije ikatokea watu wakamwambia hilo mana ataumia sanaa
 
Me ningekushauri umwache kwanza angalau afikishe miaka 20, ilo swala linaweza kumwathiri kuliko watu wanavyoweza kudhani.
what if akijua ukweli kwa watu baki kabla ya miaka 20?? si ndio itakuwa balaa zaidi
 
what if akijua ukweli kwa watu baki kabla ya miaka 20?? si ndio itakuwa balaa zaidi
Sidhani kama itakuwa rahisi uamini watu baki kuliko mama yako.
Kwanza mimi sioni umuhimu wa yeye kumwambia angeacha tu. Haina haja.

Sent from my head using brain
 
Kuna mtoto mmoja wa kaka mpaka leo anajua dada yangu ( Shangazi ake) ndio mama.. Sijui itakuaje akikua akapata ufahamu yani

Cc Smart911


Cc
 
Kuna mdogo wangu alifariki akaacha mtoto wa miezi 3 mwaka 2000 yule mtoto akalelewa na Mama alipofikisha miez 8 akachukuliwa na Mdogo wangu wa mwisho akaishi nae alipofikisha mwakana nusu yule mdogo wangu nae akafariki , nikamchukua mimi kumlea mpaka sasa anajua mimi ndiye mama yake wa kumzaa , Mpaka sasa ana umri wa miaka 17, hajui kama mama yake amefariki. Je nimuache au nimueleze ukweli kwamba yeye ni Yatima hana wazazi.
Usimwambie lolote mwache based on ur story ataumia sana ukicheki umri pia bado vigumu kuhandle habari kama hiyo. Kama una muhudumia vizuri hana tatizo lolote acha maisha ya endlee tu.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Subiri utamwambiaga siku ya harusi yake after hustling za maisha
 
Kuna mdogo wangu alifariki akaacha mtoto wa miezi 3 mwaka 2000 yule mtoto akalelewa na Mama alipofikisha miez 8 akachukuliwa na Mdogo wangu wa mwisho akaishi nae alipofikisha mwakana nusu yule mdogo wangu nae akafariki , nikamchukua mimi kumlea mpaka sasa anajua mimi ndiye mama yake wa kumzaa , Mpaka sasa ana umri wa miaka 17, hajui kama mama yake amefariki. Je nimuache au nimueleze ukweli kwamba yeye ni Yatima hana wazazi.


Nimependa kitu kimoja tu, umekuwa mama kwake, hadi anahisi hilo. Jambo la pili, kama hakuna event ya kufanya umuambie ukweli mwache tu... Kuna siku utakuja kumuambia, after all bado yupo chini ya miaka 18.
 
Back
Top Bottom