Mkuu kwanza kabisa anza kuangalia mazingira mazuri ya soko ya mboga mboga hasa eneo ulipo jaribu kupitia kwenye masoko ya wakulima yale kama yapo pia jaribu kupitia kwa wanaouza mboga waulize huwa wanachukua aidha kwa (tenga) au (mfuko) moja Shilling ngapi ukipata ABC za soko sasa njoo tuingie shambani.
Umesema una nusu eka si ndio master? Sasa na uzuri umesema eneo lina fensi na kisima kipo,, sasa basi angalia uwezekano wa kupata mbolea ya samadi kwanza, na ujue udongo wa eneo lako husika kama ni kichanga, tifutifu, mfinyanzi au wa aina gani,, kama ni tifutifu au mfinyanzi itakupa urahisi zaidi katika umwagiliaji sababu kichanga itahitaji wastani kila siku umwagilie ( pia uwe na lile bomba la kumwagilia, au mashine pia unaweza kumwagilia kwa njia ya kawaida tu ya kubeba maji kwa ndoo). Kingine hakikisha uwe na bomba la kupuliza dawa hasa kwenye chainiz sabb kuna kaugonjw flan baadhi ya maeneo huwa majini kama yanakua na ukungu au kunyauka flani hivi.
Sasa basi uwe na jembe pamoja na leki tengeneza vitalu, ( nikipata picha ntatuma mfano wake) tengeneza kitalu cha mfano wa tuta hiyo ni nzuri sababu ukimwagia maji yatakua yanaingia vizuri kwenye ardhi.
Tafuta mbegu nzuri kwenye maduka maalumu ya Chinese pamoja na mchicha,, Chinese anza kutia kwnyw kitalu ikitoka ikifika walau inch4 pandikiza kwenye vitalu vyako ulivoandaa kwa kusia miche, pia kuna option ya wauzaji wa miche unaweza kwenda kununua miche iliyo tayari kwa kupandwa hasa kwa wale jamaa wanaouza miche ya maua na miti wanaweza kuwa nazo.
Lakini epuka kuku maeneo hayo maana ni waharibifu sana wa mboga mboga hasa Chinese,
Kwa maelezo zaidi tembelea duka lolote la pembejeo za kilimo utapata maelezo zaidi kuhus mbolea nzuri, pia viuatilifu bora pamoja na mda wa kupanda pamoja na kuanza kuvuna mboga zako,, usiogope ingia duka lolote wapige maswali ya kutosha hata kama hununui chchte Mkuu