Ushauri: Ununuaji wa magari

Ushauri: Ununuaji wa magari

Wadau naomba kuuliza, TRA hutoa bei elekezi kwa ajili ya kodi, lakini unaweza nunua gari kwa bei ndogo kuliko hiyo elekezi ukiagiza nje ya nchi, je TRA wanaweza tumia document ulizonunulia kukokotoa kodi?

Natanguliza shukrani.
 
Nunua Gari iliyo exactly ten year after manufacturing. Utasave dumping fee name depression itakuwa maximum yaani 80%. Hiyo ndo utalipa hela kidogo tra. Alafu angalia bei elekezi tra kwa Gari husika
Mkuu inakuwaje mbona nasikia dumping fee inaanzia na miaka 8? Au huu ni uwongo?
 
Nunua Gari iliyo exactly ten year after manufacturing. Utasave dumping fee name depression itakuwa maximum yaani 80%. Hiyo ndo utalipa hela kidogo tra. Alafu angalia bei elekezi tra kwa Gari husika

mimi sina hakika kama unauhakika na unachosema kama ni cha uhakika. Depreciation kwa sasa inaanzia miaka 8+ after manufacturing na sio 10+ kama zamani.
 
codes, Pamoja na ushauri mwingi unaoendelea kupewa, mi nakushauri kitu kimoja. Nunua online toka kampuni yoyote Japan utakayoipenda ila hakikisha gari linafanyiwa inspection na kampuni ya EAA (East Africa Automobiles). Wambie wauzaji wakaguliwe na kampuni hiyo kwani ndio pekee inayoamika kwa kukagua gari na kuhakiki ubora wake.

Nina uzoefu na nina hakika na ninachikisema.
 
Pamoja na ushauri mwingi unaoendelea kupewa, mi nakushauri kitu kimoja. Nunua online toka kampuni yoyote Japan utakayoipenda ila hakikisha gari linafanyiwa inspection na kampuni ya EAA (East Africa Automobiles). Wambie wauzaji wakaguliwe na kampuni hiyo kwani ndio pekee inayoamika kwa kukagua gari na kuhakiki ubora wake. Nina uzoefu na nina hakika na ninachikisema.

Ahsante kwa ushauri wako mkuu.
 
Umedhurumiwa gari ? Ndena na payment slip yako na copy za TT ubalozi wa Japan.
 
Kama ulikuwa unawasiliana kwa email imelala kwako, but kama through tradecarview account do as I tell you. Maelezo yapo on tradecarview never negotiate with a seller through private email.ndio maana unalipa pay trade .
 
Libaba OPAL siyo mchezo, inachagua vituo vya mafuta (wewe utakuwa na undugu wa karibu na BP tu). kuhusu spare sijajua sana ila nilishawahi kusikia watu wanasema eti vifaa vyake ni aghali.

Subiri watu wengine wachangie pia. yangu ni hayo tu
Amekwambia OPA wewe umekurupukia OPAL au ulitaka kumaanisha OPEL? OPA ni NZT vvti cc 1760 injini zipo katika magari mengi hadi katika Rav4

Production 2000-2005
Body and chassis
Body style 5-door CUV
Layout Front engine, front-wheel drive / Four-wheel drive
Powertrain
Engine 1.8 L I4 1ZZ-FE
2.0 L I4 1AZ-FSE
Dimensions
Length 4,250 mm (167 in)
Width 1,695 mm (66.7 in)
Height 1,525 mm (60.0 in)
Curb weight 1,310 kg (2,890 lb)
Hapo kuna ya 2.0 L14 1AZ-FSE
 
Jamani kwa mwenye kujua ni wapi nitaweza pata gari used ya kununua!aina ni Rav4, Escudo milango 5 (auto/manual) Noah old model na nyinginezo. Karibuni!
 
God Baba, Jamani! usihangaike na zilizowachosha wabongo, agiza Japan tu! kwan kusubiri mwez mmoja na nusu unashindwa? Au kama huwezi waambie mawakala wakuagizie na malipo yao ni kidogo tu.
 
Habari,

Kwa yeyote anayetaka magari kwa jumla au rejareja kutoka japani moja kwa moja njoo pm nikusaidie au nitafute katika simu tajwa hapo chini. Pia unaweza kujipatia gari kwa bei ndogo zaidi ukilinganisha na tanzania kutoka katika yard/garage zetu za South Africa (tokyo car mesina) au Gaborone Botswana.

Pia utapewa ushauri wa kuku wezesha kupata gari lako kwa bei nafuu zaidi.

Mimi ni muwakilishi wa kampuni ya K.K AUTOWORD(pvt) Ltd yenye makao makuu katika jiji la nagoya nchini Japan. Pia tuna matawi katika nchi mbalimbali za Africa. Karibu tufanye biashara.

Ahsante.
 
Mnaotaka kununua magari kwa sasa kama huna haraka subirini uchaguzi mkuu upite kwanza maana dollar ya Marekani imepanda mno. Mtanunua kwa bei kubwa mno kwa sasa.

Uchaguzi ukiisha shilingi yaweza pata nguvu kidogo. Hivi sasa mafisadi wenye pesa nyingi wanageuza shilingi zao kuwa dollar ili ikiwezekana wazitoroshee nje ya nchi na wao kukimbia kama rais ajaye atawabana sana. Ni ushauri tu.
 
Mwenye uzoefu na gari za mazda demio anipatie. Nataka kujua spare zake na je ukubwa wake ni kama ist au vitz au swift
 
Ukiacha na beforward mtandao gani nao mzuri kununua magari
 
Wakuu nashukuru sana kwa elimu nzuri kuhusu aina ya magari yanayofaa kwa mazingira ya Tanzania. Naomba ushauri kuhusu matumizi ya mafuta, ubora, upatikanaji na gharama za vipuri kwa gari aina ya Toyota Kruger la 2005 cc 2400. Asante.
 
Back
Top Bottom