Ushauri: Ununuaji wa magari

Ushauri: Ununuaji wa magari

Hizi gari ni kama Baby walker, ni kwenye lami tu, kwenye rough road lazima ung'oe bampa la mbele. Nishawahi kuwa nayo hiyo ila ni very comfortable.
 
Naombeni msaada kwa mwenye uzoefu kuagiza gari kupitia tradecarview. Nataka kulipia ila nitakwepa gharama za paytrade (USD 300). Je hawa jamaa ni waaminifu? Najua autorec huwa hawana shida, ila hawa tradecarview sijawahi kuwatumia. Nipeni uzoefu.
 
Naombeni msaada kwa mwenye uzoefu kuagiza gari kupitia trade car view. Nataka kulipia ila nitakwepa gharama za paytrade (USD 300). Je hawa jamaa ni waaminifu? Najuwa autorec howa hawana shida, ila hawa tradecarview sijawahi kuwatumia. Nipeni uzoefu.

Kwa usalama zaidi wa gari yako, wape tu hiyo $300. Waweza kuikwepa hiyo, then ukaja kulizwa zaidi
 
Kuna kampuni inaitwa Japan Cars And Trucks Co., Ltd wamekubali kuniuzia spacio ya 2004 kwa USD 2000 CIF. Nahisi ni bei ndogo kulinganisha na kampuni zingine je niwaamini hawa? au changa la macho? Nikitaka kujua kama kampuni si ya uwongo nitumie mbinu gani?
 
Kwa wale waliochangia ushauri juu ya kununua gari cartrade view nawashukuru. Nililipa kwa paytrade. Tayari shipping documents zimetumwa na gari lipo baharini. Hii ina maana gari inakuja, ila sina uhakika katika hali gani. Sababu ya kununua gari hili lilikuwa ni bei rahisi kulingana na mitandao mingine hadi nikawa na wasiwasi.

So fingers crossed hadi likifika, ingawa nimeongea na muuzaji kwa simu akanihakikishia kuwa gari lipo katika hali nzuri. Ni vizuri watu wakaufanyia kazi ushauri unaotolewa hapa. Vilevile hakuna sababu ya kulizwa wakati kila swali lina jibu hapa JF.

All the best
 
Libaba OPAL siyo mchezo, inachagua vituo vya mafuta (wewe utakuwa na undugu wa karibu na BP tu). kuhusu spare sijajua sana ila nilishawahi kusikia watu wanasema eti vifaa vyake ni aghali.

Subiri watu wengine wachangie pia. yangu ni hayo tu
Mbona BP imefunga vituo vyake Bongo na bado OPAL zipo barabarani?
 
MwanaHaki, Kaka naona ni mnunuzi mzuri sana. Na inaonesha pia una kauzoefu cha ku purchase goods from abroad nimependa sana mchanganuo wako
 
Ushauri kwa watumiaji wa gari aina ya landrover freelander je utumiaji wake wa mafuta ukoje? Na upatikanaje wa spare ukoje?
 
Toyota Altezza GXE10(2000) / ALLOY WHEEL

FOB US$1,200
Year 2000

Naombeni mnisaidie kukokotoa gharama hadi mikononi kwangu
 
Mkuu si kweli unayosema. Kwenye tradecarview magari yaliyopopale tayari makampuni yake yameonyeshwa na baei za magari yao pia na si kwamba magari yanauzwa na tradecarview, wao ni mkusanyiko tu wa makampuni mengi yanayouza magari. Uzuri wa kwenye tradecarview kuna wigo mkubwa wa kuchagua magari tofauti na hiyo beforward.jp maana nimeangalia ni wachovu kwelikweli hawana Harrier ya kuanzia mwaka 2001 hata moja, Suzuki escudo ya kuanzia mwaka 2001 hakuna hata moja na pia hawaonyeshi mileage ya magari yao kitu ambacho ni hatari maana unaweza kununua gari lililokongoroka hasa. Kuna watu kadha wa kadha niliokaribu nao wamenunua kupitia tradecarview magari mazuri kabisa kwa bei nzuri.

Ni zamani na naona ulikuwa umeiponda saana Be Forward, labda wakati huo, alichosema mwenzetu ni sawa maana Trade Car view wanakupeleka kwa dealer na Be Forward wana deal wenyewe. Na mie nimenunua kweli Be Forward, ni wazuri na magari yao mazuri na bei zao very competetive. Wala si wachovu kama unavyofikiria. Usijali kutoonekana unalolitaka leo haipiti wiki hujalipata maana wana-upload kila wakati.
 
mkuu vp kuhusu car junction? wapo vizuri?
 
Ni zamani na naona ulikuwa umeiponda saana Be Forward, labda wakati huo, alichosema mwenzetu ni sawa maana Trade Car view wanakupeleka kwa dealer na Be Forward wana deal wenyewe. Na mie nimenunua kweli Be Forward, ni wazuri na magari yao mazuri na bei zao very competetive. Wala si wachovu kama unavyofikiria. Usijali kutoonekana unalolitaka leo haipiti wiki hujalipata maana wana-upload kila wakati.

Ni kweli mkuu kwa wakati huo walikuwa kama nilivyoeleza hapo awali. Kwa sasa nimeingia kwenye web yao wako vizuri na bei zao ni nzuri zinavutia kwa kweli japo magari yao yamekwenda mwendo kidogo. Tupe experience ya gari yako wewe vipi ubora wake hata kama imetembea km zaidi ya 100,000?
 
Ni kweli limetembea zaidi ya km 100,000 but that is what I could have afforded, ila gari liko vizuri, unalipokea kama unavyoliona kwenye mtandao, literally haukutani na uporaji hata kama gari linakaa muda kidogo. Ila kuna baadhi ya wafanyakazi wao sio wazuri ki-hivyo ila wengine ni very helpful. In a nutshell gari nililochukua liko katika hali nzuri na baadhi ya vitumiaji kama matairi (including spare) na vinginevyo ni vizuri na nadhani wameweka vipya mfano tyres na jack.

Ningeulizwa ningewafagilia, maana mpaka gari limeingia nililipa around 12M hapo ni turn key, ambapo pengine aina ile ile mode ile ile ilikuwa mpaka kufika ni about 17M turn key. That is all I can say
 
Nilipata gari aina ya gaia 2002 cc2000 kwa USD 650 FOB nikalipa usd 2150 CIF na nikalitoa kwa jumla ya USD 2830. Total USD 4980
 
Back
Top Bottom