Ushauri: Utumishi waache siasa kwenye kazi

Ushauri: Utumishi waache siasa kwenye kazi

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,973
Reaction score
6,750
Habari za wakti huu;

Naandika uzi huu kwa nia nzuri kabisa ambayo najua Ndugu XAVIER DAUDI pamoja na Waziri anayehusika na UTUMISHI pia wanayo. Utumishi wa serikali/umma ni heshima kubwa sana kwa yeyote anayepata fursa ya kuajiriwa huko. Hata ni ukweli usiopingika kwamba sio kila mtu ana sifa ya kuwa mtumishi wa umma iwe wa kisiasa au kitaaluma. Hivyo basi ni muhimu sana umakini ukawepo katika mfumo mzima wa ajira serikalini.

Binafsi naona ni ujinga kuita watu 10,000 kwa ajili ya usahili wa kazi za watu mia. Ni uhuni,ni ushenzi na ni ushamba usiokuwa na maana.Unakuwa mbaya zaidi pale unapowaita hao watu sehemu moja tena kipindi ambacho kuna maambukizi ya COVID ilhali watu wakitaka kukusanyika kwa masuala ambayo hamuyapendi mnawakatalia. Inakera zaidi pale ambapo unagundua kwamba haya yote yanafanyika sio kwa sababu mnataka kupata watumishi bora bali mnataka kujitoa lawama na kujikosha na kumbe mnajidhalilisha na kuchosha watu. Sasa niwape ushauri

Teknolojia imekuwa na dunia imebadilika kuna nmna nyingi sana za kufanya mchujo kwa kutumia machine learning au kwa kupita aptitude tests, Career events n.k. Kwa mfano, Mnaweza kuwa na Career events kwenye vyuo na shule za upili ambako mnaselect watu wenye sifa za kipekee na kuwaweka katika database ya watu wangependa kufanya kazi serikalini. Tena hii database wanaweza share watu wa TISS, TPDF, TPF, Magereza Tanzania, na Taasisi zote za Uma ambapo mtu ambaye anapenda kufanya kazi serikalini anajisajili kwenye hio database bure an kuweka CV yake pamoja na kuonesha interest yake ni fani gani au eneo gani mfano Military, Police, Health ETC. Mkimsajili mnapatia namba ya ufuatiliaji ambapo yeye atakuwa anahuisha akaunti yake kama ulivo mfumo wenu wa sasa.

Pili kila mwaka mnaweza kufanya USAILI wa wazi katika mikoa(Unaweza kuwa restrictive PIA) ambapo watu ambao hawana ajira kabisa au wana ajira ila wanataka kuingia serikalini kubadili fani wanajitokeza kwa wiki nzima mnakaa kwenye maeneo ya maonesho tena pamoja taasisi nyingine mnfanya Government Career week.

Inapofika wakati wa Ajira,Mnatangaza nafasi na mnawafanyia waombaji USAILI wa njia ya mtanda, kwa kutumia Aptitude test, phone interview, video conferences, Case examination, reference check na kisha kama mkipata watu wenye vigezo mnawaita kwa ajili ya written kisha oral na kisha mnawapa mkataba.

Katika kila hatua mnarekodi score za msahiliwa na kumjulisha performance yake kwa vigezo vilivyo wazi. Rekodi zake zinakuwa valid kwa mwaka mzima kwa wale ambao wamefaulu ila kwa wale ambao hawajafaulu inabidi warudia tena wakiomba nafasi nyingine ila kwa mtu ambae alifikia pass atarudia written na oral interview.

Kwani nilichoshauri hapa ni kitu kigumu?Kinawezekana kiteknolojia na kinawezekana kiundeshaji.LAKINI kinawezekana kwa watu wenye NIA NJEMA

Swali JE Mna NIA NJEMA?

Endeleeni kupenyeza watu kwenye utumishi wa umma bila kuzingatia weledi na kuna siku si mbali sana mtalipia makosa hayo.

Kumbukeni SIO kila mtu anaweza kuwa mtumishi wa umma.Kuwa mtumishi wa umma kuna hitaji uelewe viziuri uafanyaji kazi wa serikali,uwe mzalendo,uwe muwazi na zaidi uwe na hari ya kutumikia umma na kuona taifa lako kusonga mbele.Ukiruhusu watu waingie serikali kwa maslahi binafsi job security na kutaka kuula,Basi Rushwa itaendelea kuwepo,Kukosekana weledi serikalini kutaendelea kuwepo na wananchi wataendelea kteseka na kutozwa TOZO za ajabu kama hii ya MIAMALA kisa tu viongozi walishindwa kufanya mipango thabiti ya maendeleo na kulazimisha MAMIRADI yenye gharama kubwa ndani ya muda mfupi bila kuzingatia uwezo wao wa kiuchumi na faida za miradi hio

NImeandika mengi nasisitiza vijembe nilivoweka humu havihusiani na itikadi yangu kisiasa na wala havilengi kuondoa umuhimu wa ushauri wangu kwenu

Nawatakie kila la HERI.

Kama mkishindwa kufanyia kazi huu ushauri basi mtakuwa ni BURE kabisa.

Pole kwa waombaji kazi serikalini mnaozungushwa na kupewa stress. TUMAINI BADO LIPO.
 
Back
Top Bottom