Ushauri: Uwekezaji katika maeneo ya kambi za Jeshi utazamwe kwa jicho la 3

Ushauri: Uwekezaji katika maeneo ya kambi za Jeshi utazamwe kwa jicho la 3

Jeshi utaliweza Kaka ?

Jeshi letu ni taasisi kubwa,Heshima yake na Uzalendo wake ni jambo la kutukuka ktk ukanda wa Afrika ya kati na kusini mwa Afrika..

Nidhamu na uadirifu mkubwa wa Jeshi letu ni jambo la kujivunia na sote twajivunia..

Kwa unyeyekevu mkubwa tuna nafasi ya kushauri kwa heshima na hekima.
 
Lugalo ipo hapo miaka dahari Mkuu, na mpaka watu wapo hapo maana yake wameshafanya CBA kama kuna risk jeshi huwa ni amri wanatolewa mara moja.
Wewe huzioni risk..mbona ziko wazi wala hazihitaji CBA..hata km ipo hapo karne, kwa sasa haina sifa kuwa barrack.
 
Majeshi yetu ya Ulinzi na usalama ni vyombo nyeti mno katika mustakabali wa usalama wa nchi yetu (Kisiasa,Kiuchumi na Kijamii). Maeneo ya kambi za Jeshi ni maeneo adhimu na yanapaswa kutochangamana na maeneo ya kiraia kwa namna moja au nyingine.

Miaka michache iliopita tulipata janga la mabomu kulipuka ktk kambi kadhaa za jeshi na kusababisha maafa na utaabishaji mkubwa.Nadhani yatupasa kujifunza na kuepuka ukaribu na maeneo ya kiraia au kuchangamanisha maeneo haya na mambo ya biashara kwa ujumla.

Kwasasa kumekuwa na wimbi kubwa la wafanyabiashara kuwekeza maduka, yards,ofisi,kumbi, showrooms n.k. Inawezekana kabisa nia na lengo ni zuri (Kwa mujibu wa tathmini) kabisa ila kwa unyenyekevu mkubwa nadhani yatupasa kutazama kwa mapana athali zake kiusalama sasa na baadae.
Wewe ndio unajua sana kuliko wale Ma generals na mabrigadia waliobobea pale?
 
Ikiwa ushauri una tija ufanyiwe kazi

La hasha ikiwa hauna tija upuuzwe

Mungu ibariki Tanzania
 
Fremu zote unazoona zote kuzunguka kambi zote ni za wanajeshi kupitia vyama vyao vya Saccos
Kazi zingine ukikubali kufanya zinakufunga usifanye vile wanaokulipa wanafanya..
Wananchi wanalipa kodi ambazo zinatumiwa kulipa mishahara na kutunza wanajeshi, inakuwaje tena wao kutamani kufanya biashara kushindana na wanaogharimia mishahara yao?
 
Nchi iko kwenye uchumi wa maframe mzee

Ova
Hapo Gongolamboto jeshi wameuza ardhi ya mbele watu wanajenga fremu.
Uchumi wa fremu
Hiyo project ya fremuz waliianza tangu mwaka 2020, kuanzia kule KIUT naona sasa sababu ya uwepo wa Kituo cha mwendokasi wameamua kuwekeza kwa mtindo wa kuwauzia wafanyabiashara eneo wanajenga fremu wenyewe kwa mkataba wa muda wa miaka kadhaa, baada ya muda wa mkataba kuisha fremu zitarudi kuwa mali ya Jeshi na kuanza kukodishwa kwa wahusika.
 
Akili za Sa100 na Lucas Mwashambwa zitaigharimu hii nchi.
 
Kwa kuongezea

Ipo siku Mr. Slim atapenyezea watu wake humohumo kuja kusoma mwenendo wa majeshi yetu kisha awatume M23 watusumbue
Hata Sasa amepenyeza.hujui kuwa Saamiamoja ni mnyarwaanda?
 
Kituo cha Polisi cha wilaya ya Arumeru pale Usa River kimezungukwa na frem ambapo zamani hazikuwepo!! Nilipita mwezi uliopita nimeshangaa
 
Majeshi yetu ya Ulinzi na usalama ni vyombo nyeti mno katika mustakabali wa usalama wa nchi yetu (Kisiasa,Kiuchumi na Kijamii). Maeneo ya kambi za Jeshi ni maeneo adhimu na yanapaswa kutochangamana na maeneo ya kiraia kwa namna moja au nyingine.

Miaka michache iliopita tulipata janga la mabomu kulipuka ktk kambi kadhaa za jeshi na kusababisha maafa na utaabishaji mkubwa.Nadhani yatupasa kujifunza na kuepuka ukaribu na maeneo ya kiraia au kuchangamanisha maeneo haya na mambo ya biashara kwa ujumla.

Kwasasa kumekuwa na wimbi kubwa la wafanyabiashara kuwekeza maduka, yards,ofisi,kumbi, showrooms n.k. Inawezekana kabisa nia na lengo ni zuri (Kwa mujibu wa tathmini) kabisa ila kwa unyenyekevu mkubwa nadhani yatupasa kutazama kwa mapana athali zake kiusalama sasa na baadae.
Tanzania si Kongo ama Burundi....
 
Ni uzuzu wa hali ya Juu ,siku kikiwaka tunashikika kirahisi kwelii
 
Hiyo project ya fremuz waliianza tangu mwaka 2020, kuanzia kule KIUT naona sasa sababu ya uwepo wa Kituo cha mwendokasi wameamua kuwekeza kwa mtindo wa kuwauzia wafanyabiashara eneo wanajenga fremu wenyewe kwa mkataba wa muda wa miaka kadhaa, baada ya muda wa mkataba kuisha fremu zitarudi kuwa mali ya Jeshi na kuanza kukodishwa kwa wahusika.
Mimi ilinipita. Ningepata plot pale
 
Back
Top Bottom