Ushauri: Uwekezaji katika maeneo ya kambi za Jeshi utazamwe kwa jicho la 3

Ushauri: Uwekezaji katika maeneo ya kambi za Jeshi utazamwe kwa jicho la 3

Majeshi yetu ya Ulinzi na usalama ni vyombo nyeti mno katika mustakabali wa usalama wa nchi yetu (Kisiasa,Kiuchumi na Kijamii). Maeneo ya kambi za Jeshi ni maeneo adhimu na yanapaswa kutochangamana na maeneo ya kiraia kwa namna moja au nyingine.

Miaka michache iliopita tulipata janga la mabomu kulipuka ktk kambi kadhaa za jeshi na kusababisha maafa na utaabishaji mkubwa.Nadhani yatupasa kujifunza na kuepuka ukaribu na maeneo ya kiraia au kuchangamanisha maeneo haya na mambo ya biashara kwa ujumla.

Kwasasa kumekuwa na wimbi kubwa la wafanyabiashara kuwekeza maduka, yards,ofisi,kumbi, showrooms n.k. Inawezekana kabisa nia na lengo ni zuri (Kwa mujibu wa tathmini) kabisa ila kwa unyenyekevu mkubwa nadhani yatupasa kutazama kwa mapana athali zake kiusalama sasa na baadae.
Acha kujipa umuhimu usio stahili nani huo unyeti umeuona wewe

Walio panga hivo hawakujua kwani
Ushaur wako ni utopolo umetupiliwa mbali
 
Wanakusanya fedha na mapato....unataka wategemee tu serikali kuu ?!? [emoji44][emoji44]
Zile pesa wala hazina msaada kwenye kupunguza mzigo kwa serikali.
Serikali hii kwa woga wake wameongeza mshahara na posho za wanajeshi halafu watumishi wengine wanaambiwa wasubiri kauli ya Rais
 
Pole.
Eneo la mbele nafikiri wameshachukua lote, sijajua kwa eneo la nyuma yake kama limekwisha.
Pole.
Eneo la mbele nafikiri wameshachukua lote, sijajua kwa eneo la nyuma yake kama limekwisha.
Hivi mkataba wao ukoje?
Unajenga then unalipa kodi au unatoa pesa unajenga halafu hulipi kodi mpaka muda husika?
Halafu mbona ilikuwa kimyakimya tumeshituka watu wanaanza kujenga.
Kigoma welding ndio walinishitua huku tayari plot zimeisha. Sijamwoji sana
 
Unapatiwa eneo unajenga. Unaendesha biashara yako mpaka muda wa mkataba ukiisha ndo unaanza kulipa kodi, kama hautahitaji kuendelea unawapisha wengine wanaingia.
 
Wajitahidi kuhifadhi mabomu yao vizuri yasije kutokea ya Mbagara na G/mboto
 
Back
Top Bottom