Ushauri: Vijana wanaochangishana kumsaidia Sabaya wafuatiliwe, wana nia ovu ya kuzuia haki isitendeke(obstruction of justice), pia wanatukana Serikali

Ushauri: Vijana wanaochangishana kumsaidia Sabaya wafuatiliwe, wana nia ovu ya kuzuia haki isitendeke(obstruction of justice), pia wanatukana Serikali

Hawa ni lile kundi ambalo mimi nimelichana hapa JF hivi karibuni, lina mambo ya hovyo sana. Hili kundi linachangishana pesa huku likitoa maneno ya kashfa kwa mkuu wetu. Nina wasiwasi wana lengo la kuzuia haki isitendeke.

Vyombo vya kisheria na vya kidola viwakamate,viwahoji na ikibidi wapelekwe mahakamani. Kukamatwa kwao hakutawashangaza kwa kuwa hata wao walikuwa wanachongea watu wengine wakamatwe.
Mbona wakina mbowe walichangiwa ??!!

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Mbona kina Mbowe na viongozi wengne wa Chadema tuliwachangia pale walipopatikana na hatia mahakamani na walikuwa wakikejeli na kudhihaki Serikali, kwann kwa Sabaya iwe nongwa!???

Pili, michango kwa huyó Sabaya kunaathirije mwenendo wa kesi mpaka vyombo vya dola viwakamate!??

Kwani kuchangia mtu pesa ni uvunjifu wa sheria!??
Mnachanga ili isaidie kwenye nn??

Hapa kuna makundi mawili kundi la kwanza na linalohangaika hivi sasa ni lile linaloratibiwa na Watendaji au waliowahi kuwa Watendaji Serikalini. Hawa ni wale wenye tabia zilizolandana na za Saa Mbaya. Hawafanyi hivyo kwakuwa wanamkubali Saa Mbaya hapana. Bali wanajaribu kujijengea ukuta ili wasiweze kufikiwa/kukamatwa na kufikishwa Mahalamani. Jambo ambalo nalo lita fail.

Kundi la pili ni kakijikikundi cha Wachache waliokuwa wanafaika wa zile harakati uchwara za Saa Mbaya wakiwemo Wanasiasa. Nalo litaangukia pua.
 
Ni swala la muda tu mkuu, ila nakwambia wazi Maza anajua beat anayopiga kapata dancers wa kutosha

Hvyo baada ya muda hii ishu ya huyu dogo itakuwa haina kiki tena kisha baadae utasikia 'DPP hana nia ya kuendelea na kesi..'
Sabaya lazima aozee jela,hatatoka milele
 
Wanachangia kupitia namba ipi na Mimi nimchangie ..... Haiwezekani sabaya awe mbuzi wa kafara dhidi ya serikali ya CCM , sabaya aliwakilisha kile mwenyekiti wa CCM na CCM walimwagiza kufanya ,kama ni kuwajibishana inabd tuwajibike wote kuanzia Raisi aliyeko madarakani mpak serikali yote ya CCM
 
Wanachangishana kumsaidia Sabaya kufanya nini? kama kesi tayari ipo mahakamani na ushahidi pia naamimi upo tayari, au unataka kusema wanachangishana ili wawahonge mahakimu?
 
Mbona kina Mbowe na viongozi wengne wa Chadema tuliwachangia pale walipopatikana na hatia mahakamani na walikuwa wakikejeli na kudhihaki Serikali, kwann kwa Sabaya iwe nongwa!???

Pili, michango kwa huyó Sabaya kunaathirije mwenendo wa kesi mpaka vyombo vya dola viwakamate!??

Kwani kuchangia mtu pesa ni uvunjifu wa sheria!??
You must be mad.

Unaweza vipi kulinganisha waliobambikiwa kesi kwa amri za mjuaji mmoja, na hilo jambazi lililopora vinywaji na vyakula mahotelini, nguo madukani, na wake za watu?
 
Pale mleta mada anaposahau kuwa kna UHURU wa kuchagua ilihali yeye ana upande alio uchagua
 
Mbona kina Mbowe na viongozi wengne wa Chadema tuliwachangia pale walipopatikana na hatia mahakamani na walikuwa wakikejeli na kudhihaki Serikali, kwann kwa Sabaya iwe nongwa!???

Pili, michango kwa huyó Sabaya kunaathirije mwenendo wa kesi mpaka vyombo vya dola viwakamate!??

Kwani kuchangia mtu pesa ni uvunjifu wa sheria!??
Jambaz lenzie hili
 
Back
Top Bottom