Ushauri wa bure: Ally Kiba nenda ukasainishwe WCB ili mziki wako upae

Ushauri wa bure: Ally Kiba nenda ukasainishwe WCB ili mziki wako upae

brigedia mafia

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2016
Posts
2,260
Reaction score
2,279
Napenda kumpa ushauri mdogo wangu Ally Salehe Kiba aende akaombe kusainishwa WCB kiroho safi ili akuze mziki wake bila ya hivyo natabiri baada ya miaka miwili ijayo hatoweza tena kumkaribia Diamond level zake bali atakuwa level za Rayvanny na Harmonize

Hawa madogo tangu waingie WCB mafanikio wameyapata mapema sana kulinganishwa na wenzao waliotoka pamoja kama vile Neddy Music na madogo wengine

Hata Rich Mavoko tulikuwa tushamsahau ila tangu aingie WCB show zimekuwa za kucheba na thamani yake imepanda maradufu
Si Mavoko tu hata Khadija Kopa alivyoshirikishwa kwenye wimbo wa Nasema nawe jina lake lilitajwa kwenye tuzo za Afrimma ingawaje hakuweza kuibuka kidedea

Ommy Dimpoz ,Yamoto band ,V money walllivyokuwa karibu na Dai majina yao yaling'aa sana ila tazama sasa ukaribu umepungua wapo wapi?
Huu ni ushauri tu najua utamfikia tu taka asitake akipuuzia shauri zake kwa maana ataenda na maji

Mimi ya kwangu ndio hayo kwa siku ya leo akiweza apokee ushauri wangu akijifanya mjuaji na kichwa ngumu shauri zake ila baadaye asije akasema hakushauriwa.
 
microphone.png
yooooooooooo
 
Mimi sio team kiba wala team diamond...wote ni wasanii wazuri.mwanzoni nilikua nahisi bifu zao zinaletwa Na media au ushabiki wa watu...lakini nimekua nikifutilia kauli za alikiba..mara karuka ukuta kwenye tamasha kwasababu Getini aliwekewa uchawi, mara anamuhisi manager wa diamond alimzimia mziki, lakini pia akihojiwa anadai diamond ni mtoto wa juzi tu kwenye game hamuwezi kwa chochote lakini wakati huhuo diamond akihojiwa Anasema alikiba amemkuta kwenye game Na anamuheshimu sana. Kauli hizi zinatosha sana kujua nani ana hekima Na nani mpumbavu.
 
Ushauri ni mzuri.
Sema sasa mafahari wawili hawawezi kukaa zizi moja.
Vmoney still yupo juu na anaendelea kufanya vizuri zaidi kwa Africa.
ndipo hapo anapokosea Ally K kujiona yupo juu kuliko mwenzake

Rich Mavoko naye pia alikuwa hivyo hivyo mwanzoni alikuwa anaongea maneno ya shombo sana kwa Dai kama neno hili" Wa Tz wengi hawajui kutofautisha almasi na kipande cha chupa mimi ni almasi ila huyo mnayemfagilia ni kichupa ila ipo siku mtajua thamani yangu" huu ni mfano tu ila alikuwa akimdiss mara kwa mara Diamond kwamba anaiba nyimbo za watu na shutuma nyingine nyingi ila leo kiko wapi si kasainishwa na huyo huyo aliyemtusi? Lakini si haba thamani yake si sawa na Rich wa zamani ambaye hakuwa chini ya WCB


Wengi walimponda dhamani alivyosainishwa WCB ila leo wanamuonea wivu mafanikio yake



Hii ni sawa na Juma Mwambusi alivyokuwa anaenda Yanga wengi walimponda na kusema mafahari wawili hawakai zizi moja na amejishusha kuwa kocha msaidizi lakini jaribu kufikiria Juma Mwambusi huyu ni sawa na yule wa Mbeya city??


Bila shaka jibu unalo ,na huu ni mfano tosha unaotufunza kuwa muda mwingine yatupasa tujishushe ili tupate mafanikio zaidi
 
Hiz bangi ulizofuta usrudie tena maaana ukirudia tena utakuja kuandika na mazaako huko ukimshaur,,,,
 
Back
Top Bottom