Ushauri wa bure: Ally Kiba nenda ukasainishwe WCB ili mziki wako upae

Ushauri wa bure: Ally Kiba nenda ukasainishwe WCB ili mziki wako upae

Acheni ujinga diamond hawezi miliki mziki wa bongo. Akili ndogo haiwezi kuongoza kubwa. Diamond sio mwanamuziki ni mdandiaji chini ya redio fulan inayo tumiwa na kiongoz fulan kuongoza jiji. Kiba vumilia siku zinakuja wasafi itakuwa wachafu....
Pole tena hauna pole kaka hauna(in manfongo's voice)
 
Tuzo za kill nazo mpaka team wema na team jokate sasa hivi wema hana team si alizitukana utaona kama atapata uwiiiiiii huu mwaka wa kiba aisee
Kuna jamaa jana nilimwambia kuwa, sku hizi Wema ndio kwanza yuko neutral , kipind kile alisaidia sanaaaa. mbona ni hatari hiyo yaan nasubiri nione kutatokea nn!! Sasa
 
microphone.png
yooooooooooo
Papirrrr yooooooo
 
Napenda kumpa ushauri mdogo wangu Ally Salehe Kiba aende akaombe kusainishwa WCB kiroho safi ili akuze mziki wake bila ya hivyo natabiri baada ya miaka miwili ijayo hatoweza tena kumkaribia Diamond level zake bali atakuwa level za Rayvanny na Harmonize


Hawa madogo tangu waingie WCB mafanikio wameyapata mapema sana kulinganishwa na wenzao waliotoka pamoja kama vile Neddy Music na madogo wengine


Hata Rich Mavoko tulikuwa tushamsahau ila tangu aingie WCB show zimekuwa za kucheba na thamani yake imepanda maradufu


Si Mavoko tu hata Khadija Kopa alivyoshirikishwa kwenye wimbo wa Nasema nawe jina lake lilitajwa kwenye tuzo za Afrimma ingawaje hakuweza kuibuka kidedea


Ommy Dimpoz ,Yamoto band ,V money walllivyokuwa karibu na Dai majina yao yaling'aa sana ila tazama sasa ukaribu umepungua wapo wapi?



Huu ni ushauri tu najua utamfikia tu taka asitake akipuuzia shauri zake kwa maana ataenda na maji


Mimi ya kwangu ndio hayo kwa siku ya leo akiweza apokee ushauri wangu akijifanya mjuaji na kichwa ngumu shauri zake ila baadaye asije akasema hakushauriwa.
Kwa hiyo WCB wanamhujumu Kiba?
 
Back
Top Bottom