Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Kwa hapa amm sina cha kuchangia.Acha nikomae kulea wanangu na wazaz wangu japo sina maisha.
Lakin kitu nilichojifunza kwa wazaz wangu ni hiki "mambo yao ni yao binafsi has kama ni mabaya".
Sijawahi kushuhudia baba na mama wakigombana wala kuzozana hadharani toka nizaliwe mpaka sasa at 30s.
Nina uhakika wanapishana hilo sipingi maana wao ni wanadam lakin hawajawah kupitiwa kiasi kwamba vijana wqo tukashuhudia tofaut zao hadharani.
NADHANI NI BUSARA NA HEKIMA NA ZAID KUOMBA MUNGU ATUSAIDIE KUYAMUDU HAYA.
 
So kama aliambiwa nakuondoka na hiyo suruali ndio amsuse mtoto wake ...hahaa dahh so sad"....... kwahiyo kinachotaka kumrejesha kwa mtoto sasa hivi ni nini " !?, zile hasira sasa hivi zimeisha !?, now ndio anatambua kuwa diamond ni mwanae !?

Umeshawahi jiuliza swali !?, kama diamond asingekuwa hivi alivyo leo baba yake angeendelea kumlilia lilia !?

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji16][emoji16]mkuu umewaza mbali sana, diamond angekuwa maskini asingemlilia. Kimsing, wanaume tunakusea sana ugomvi wa mapenzi ya wawili kuhusisha watoto.. yan unagombana na utamu wako halafu unampotezea na mtoto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona YouTube mzazi ana busara sana kaongea mengi huku akimtakia mafanikio na nyota ing'are. Kasema suala la kumwalika harusini ni lake yeye Diamond cha msingi anapenda aone diamond anaoa na sio kugeuza nyumba daguro!!. Sijawahi kununua kazi ya Diamond na sio shabiki wa miziki yote ya Tz isipokuwa miziki ya OTTU JAZ BAND. Kijana nimemdharau sana kwani sisi wakristu tunafundishwa samehe saba mara sabini

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo busara imekuja baada ya kijana kufanikiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NA AKIJALIBU KUTOA MSAADA KWA BABAKE NDIO MWISHO WAKE UTASKIA YA KANUMBA
 
Ana tamani sana Ku msaidia lakin ndo akijifanya kujalibu kumsaidia ndo mwisho wake labda apande degrees tena ndipo abadilishiwe miiko
 
Mi naona wacha amfundishe tu ili iwe fundisho kwa sisi ma BABA VITOMBI i mean yaani ukipata hela wewe upo bize na vimada mzigo wa familia umemuachia mkeo anapasuka kichwa kuwaza familia ile nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona YouTube mzazi ana busara sana kaongea mengi huku akimtakia mafanikio na nyota ing'are. Kasema suala la kumwalika harusini ni lake yeye Diamond cha msingi anapenda aone diamond anaoa na sio kugeuza nyumba daguro!!. Sijawahi kununua kazi ya Diamond na sio shabiki wa miziki yote ya Tz isipokuwa miziki ya OTTU JAZ BAND. Kijana nimemdharau sana kwani sisi wakristu tunafundishwa samehe saba mara sabini

Sent using Jamii Forums mobile app
aisee a riff wapi iyo? Kwa madiba nini?
 
Hao watoto tu kawatelekeza, sembuse baba

Sent using Jamii Forums mobile app

Mmnh sizani!
Wanawake wenyewe alozaa nao wale wangeshaenda mahakamani!
Wale wameshampinga mizinga ya kimataifa kwa hiyo wako vizuri na ujasiri wa kudai hawana!
Wengine wameng’ang’ania magorofa ya Dai hapo utasema Dai hawatunzi?!
Sizani kabisa kwa hilo!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naandika nikiamini kwa namna moja au nyingine ushauri huu utamfikia huyu kijana Diamond. Yeyote asiye na maelewano na wazazi/mzazi wake pia inamuhusu. Na wazazi wanaotelekeza vizazi vyao pia wanaweza kujifunza jambo.

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda namna Diamond anavyojituma katika kazi pamoja na ubunifu katika muziki na biashara ya muziki. Pia amekuwa mstari wa mbele kusaidia vijana wenzake, hususan waliotoka katika hali duni kimaisha kama ilivyokuwa kwake, kupata maendeleo kupitia sanaa. Tumeshuhudia hali kadhalika mara kadhaa akirudi maskani Tandale na kuwasaidia wakazi wa huko, kidogo alicho jaaliwa, na mengine mengi mazuri.

Yapo pia mambo kadhaa ambayo sifurahishwi nayo kuhusu yeye, lakini nitalizungumzia hili la kumtelekeza Baba yake. Nimeona mahojiano ambayo baba Diamond amefanya na online TV moja. Ni wazi kwamba huyu mzee alitibuana na demu wake Sandra - mama Diamond, akatimka nyumbani na kutelekeza familia. Anasema wakati huo Diamond alikuwa na akili yake nzuri tu, hivyo huenda Diamond aliathirika sana kisaikolojia kwa Baba yake kutokomea kusikojulikana na kuwaacha yeye na mama yake hawana hata unga robo. Kutokana na maelezo yake aliyotoa na mazingira ya nyumbani kwake, huyu mzee ana hali ngumu. Baba Diamond sasa hivi anafanya biashara ya kukopa viatu vya mtumba Ilala, anarudi kwake magomeni anaviosha na kung'arisha kisha anatembeza mtaani, yaani Mmachinga typical. Anapoumwa kwa mfano, anakuwa hana hata fedha ya matibabu, hivyo kugeuka ombaomba. Kutokana na maelezo ya Mzee mwenyewe, majirani na mdogo wake Diamond anayeishi na baba yake, Diamond kufika kwa mzee wake ni tokea yuko na Wema!

Kilichonifanya kuandika huu uzi ni kwamba Baba Diamond ameomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya. Tena amesema kwa uchungu kabisa, kwamba hata Mwenyezi Mungu husamehe. Kwa nini , yeye asisamehewe?. Binafsi naona imefika wakati Diamond akunjue moyo wake na kumsaidia Baba yake. Katika Qur'an, ipo wazi kabisa, kwamba baada ya Mwenyezi Mungu, wanafuata wazazi. "Be grateful to Me and to your parents; to Me is the [final] destination." (Quran 31:14). Mzee Abdul alikosea kumtelekeza mtoto Diamond, haijalishi walitibuana nini na mama Diamond. Diamond hajui nini hasa kilitokea. Mzee ameomba msamaha, anapaswa kusamehewa na maisha yaendelee.

Diamond rudisha maelewano na umsaidie baba yako. Amejutia na ameomba msamaha. Kwa sasa haikupunguzii chochote kumsaidia mzee wako aishi maisha ya kawaida, ya angalau ajue familia yake itakula nini jioni. Utakuwa na amani, Itakuongezea heshima katika jamii, na zaidi utapata credit kwenye daftari lako la Akhera. Maisha yenyewe ndiyo haya. Ukiishi sana 80. Ukiishi zaidi ya 80 ni maumivu tu, uwe na hela au huna. Akifa huyu mzee katika hali hii, Diamond utaaibika Duniani na akhera.
Any fool with a dick can make a baby but it take a real father to take care of his children.. Huyo sio baba ni sperm donor
 
wakati mwingine hawa wazee wanaboa sana, ila kwa kuwa hamuyajui yalimo kiundani mnaweza mshutumu kijana wa watu na kumuona mzee kama innocent, hivi diamond anashindwa kuchukua walau M.20 akampatia baba yake, ama kibiashara cha maana hapo mjini yote haya anaweza ila akikumbuka jinsi mshua alivyokuwa mdwanzi anaonelea acha ashike adabu. me kwa upande wangu naamini diamond ana hakili timamu tena sana za kujua na kuthamini, sema hata hawa wazazi nao wachunguzwe kwa jicho la tatu, jamani kuna wazazi wana maudhi zaidi ya ibilisi.. huyo mshua kwa namna moja ama nyingine siwezi mtetea maana hata chanzo cha watoto wa mitaani walio wengi wao ni kuwa na wazazi wanaotelekeza familia zao kama ilivyo kwa huyu mzee..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdingi kinachomuua ni vidole na midomo ya watu lakini yule mzee kwa vigezo vyetu vya kitanzania yupo njema sema anaonekana ana matatizo kwa kuwa mwanae ana jina kubwa na fedha za kutosha yaani ana uwezo mkubwa wa kuendesha maisha yake. Mzee ana nyumba Magomeni Kagera na wapangaji juu na huenda hata wale wanaomwona Diamond hamsaidii wazazi wao wana maisha mabovu kuliko Diamond.
Mzee anaonekana NJAA imetawala maisha YAKE,,NYUMBA yenyewe mvua ikinyesha Kama MWEMBE? choo cha GHOROFA.,,Yule anaishi kwenye BANDA sio NYUMBA,,, mzee tumemsikia kwa KAULI YAKE,,,anatembeza VIATU... na ana matatizo ya MIGUU,, anapaswa KUSAIDIWA,,,yule DIAMOND ,,ANA ROHO NGUMU SN,, hivi siku MUNGU akimchukuwa yule MZEE ,,DIAMOND atashiriki MSIBA? na atashiriki kama MTOTO,,AU NDUGU? au JIRANI? msidanganywe na MAFANIKIO....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom