Ushauri wa bure kwa abiria wa Bodaboda; Usipande bodaboda kama...

Ushauri wa bure kwa abiria wa Bodaboda; Usipande bodaboda kama...

Nawashauri bodaboda hasa kipndi hichi cha mvua wawe wanawasha taa na ikifikq saa 12 jioni pia hii ni rahisi hata kama mtu anagari amuone mapema hua nashangaa sana kuna mvua kubwa na mtu anaendeshq boda hivo hivo bila ya taa yyte inakua ngumu kumdetect mtu hasa aliwa anatokea ubavuni mwako
 
huwezi amini gari niliendesha kwa kuangalia youtube nikaingia road mazima, then nikaenda driving school kupata cheti na maelekezo muhimu, piki piki nimeanza kufundishwa na baba yangu mdogo nikiwa shule ya msingi 2005 huko, akaja rafiki nikiwa nimemaliza form 6, nikiwa chuo nikafundishwa na watu watatu tofauti ila mpaka leo sijui kuendesha pikipiki na sinaga shobo nazo nikifikiria risk zake tu.
 
Namba 1 hiyo muhimu sana aisee mie usafiri wangu ni pikipiki yaani naendesha mwenyewe kwenda kwenye shughuli zangu ila hawa bodaboda ambao wameamua kung'oa side mirror ni moja ya changamoto kubwa sana aisee ajali muda wowote usipokuwa makini anakusababishia na wapo wenge sana ila na huwezi kukuta boda anayejiheshimu kang'oa side mirror
Mtindo wa kung'oa side mirror wenyewe wanaita kujilipua
 
wale wadada wanaopanda miguu wanaweka yote upande mmoja..hatari sana, nilishuhudia mdada kadumbukia mtaroni boda hajaanguka baada ya kukunja kona kali......bahati mbaya boda alivyoona hivyo akakimbia kamuacha abiria wake kwenye mtaro
 
Siku ya ajari hutoijua japo precautions Ni muhimu Sanaa...

Yes,
Mimi Ni muhanga wa hizi ajar muda huu napo andika ndio nimeanza kujaribu kusimamia mguu (mazoezi ya kukanyagia mguu)

Hofu, woga kwenye kukanyagia japo Nina CRUTCHES Ila mdogo mdogo with time ntazoea..

NB.
Sito panda tena USAFIR WA BODABODA
Pole mkuu. Get well soon.
 
1. Usipande bodaboda isiyokuwa na vioo vya pembeni (saiti mira) – side mirror
Pikipiki ambayo haina vioo vya pembeni, dereva haoni gari linalokuja nyuma au hata akitaka kupinda, haoni nyuma hivyo uwezekano wa kugongwa ni mkubwa sana; ni suala la muda tu wala haijalishi uzoefu. Kama unajali uhai wako na familia yako, zingatia sana hii
Ukiona boda boda haina hivi vioo chukua tahadhari kwani wengi wao ni walevi wa visungura na pombe nyingine za bei rahisi. Akishakunywa pombe akakutana na mwanga wa jua mchana au taa za gari usiku zikapiga kwenye hivi vioo halafu ukarudi kumpiga usoni mwendeshaji anapata wenge hasa ukizingatia ashatandika visungura kadhaa. Kwa hiyo suluhisho la boda boda wengi walevi ni kuondoa hivyo vioo .
 
Kama huna ulazima wa kupanda boda boda ie kama unapoenda waweza fika ndani ya dk 15 au 20 basi wewe tembea tu kwa mguu. Usikae kumfurahisha mtu au kuogopa kuitwa bahili.
 
Kama unatumia Bodaboda hasa maeneo ya MJINI pitia hapa!

1. Usipande bodaboda isiyokuwa na vioo vya pembeni (saiti mira) – side mirror
Pikipiki ambayo haina vioo vya pembeni, dereva haoni gari linalokuja nyuma au hata akitaka kupinda, haoni nyuma hivyo uwezekano wa kugongwa ni mkubwa sana; ni suala la muda tu wala haijalishi uzoefu. Kama unajali uhai wako na familia yako, zingatia sana hii

2. Usipande pikipiki ambayo dereva hajavaa Kofia/helmet
Ile kofia inakioo kinachozuia wadudu wanaoingia machoni na hata vumbi anapopishana na magari makubwa; Fikiria boda anakimbia KMS 70, halafu wadudu wamuingie machoni; ushukuru sana Mungu kama hutaishia kwenye mtaro au hata kugongwa...

Ushauri: Vile vioo vya pembeni vyote viwili havizidi shs 10,000 hivyo kama una bodaboda wako, unaweza kumnunulia/kumkopesha. Kofia ngumu ya kawaida ni kwenye shs 20,000=

Mwisho: Ukiona pikipiki ipo ovyo ovyo (haina sifa), ujue na muendeshaji yuko hivyo hivyo, uamuzi ni wako!
3. Mwendesha hiyo bodaboda ana kiduku kichwani/hachani nywele!

4. Bodaboda imefanyiwa maboresho ya kihuni, na hivyo kutoa mlio mkubwa na usio wa kawaida.

5. Mwendesha bodaboda amevaa kifulana, kikaptula, na miguuni amevaa kandambili/yeboyebo!! halafu anakaa upande wakati wa kuendesha hiyo bodaboda, huku ananing'iniza kandambili/yeboyebo yake ya mguu wa kushoto.



Narudia tena! Ogopa sana!!
 
Kuna vijiwe vina boda wazoefu na wakongwe. Panda hizo. Usipande za madereva wapya au watoto watoto
 
Back
Top Bottom