Ushauri wa bure kwa Askofu Gwajima: Ukivuliwa nguo, ukabaki utupu! Ustaarabu ni kuchutama!

Very diplomatic language kwa mfia chama kama wewe (kulinda mapenzi yako ya CCM).

Kwa lugha nyingine unalaani na kukubaliana na Gwajima vitendo vya senseless killings anavyokemea inatosha sasa.

Hakuna mtanzania mwenye akili timamu au mwanachama wa CCM timamu anayeweza kufurahia utekaji!

Kukemea utekaji ni jambo muhimu na kutumia hekima katika kukemea ni jambo muhimu zaidi.

Kukemea au kuzungumzia jambo kwa namna ambayo linaweza kuamsha hisa hasi na zinazoweza kuzua taharuki, kuumiza walengwa na wahanga sio jambo jema.

Unless uwe umedhamiria mambo mawili kukemea pamoja na kuinua machafuko
 
Wamechutama sana waramba makalio kwa miaka zaidi ya 60...
Matokeo yake ni:
Deni kukua
Ufisadi kukua
Wizi serikalini kukua
Kipande cha barabara kutoka ubungo hadi mbezi kinajengwa tokea 2012 hadi leo 2025 ujenzi unaendelea hapohapo.

Sad
 
Hii ni kutaka kujiosha tu kama shabiki ndaki-ndaki wa Samia na mfia chama wa CCM.

JF haiwezi kulaumu msimamo wako unajulikana kwenye jukwaa piga ua CCM ipo damuni kwako.

Walau unakiri senseless killings is enough, kupata kauli hiyo kwa mfia chama cha mapinduzi kama wewe; Sisi wengine tunapinduka na kauli yako ya kuwa hata wewe kada unaona senseless killings inatosha.

Maelezo mengine ya propaganda baki nayo, ukiwa kama mwachachama wa CCM ambae unajulikana humu. Hiko chama kwako ni kama damu.
 
Labda si Gwajiboy huyu ninaemjua...
Unakumbuka Ile vita na Makonda,alishauriwa hivi hivi na alipo kishika kipaza sauti!akalimsha mpaka mjomba Magu akamkubali 100%....
Swali je aliyoyasema yapo au hayapo....
Naziona media na watu Watson miminika kanisani kwake...
 
Pasko hifadhi maneno kaka yangu ..... HAUIJUI KESHO..... Usimchukie MTU KISA LEO MBAYA KESHO ANAWEZA KUKUFAA
 
Ndugu yangu Paskali Mayala hv unadhani tutaogopa hadi lini,kumbuka ndugu zetu wanazidi kuteketea na ss tumekaa kimya kana kwamba wanaootezwa ni panya ,mbwa ,mbuzi ,fisi yaani utadhani sio wanadamu wenzetu au watanzania wenzetu na sijui kwa nn watanzania tuko wabinafsi kwa kiwango cha juu hivyo.
 
Naunga mkono hoja, Gwajima apotezee tu muhimu ujumbe wake umefika.
 
Mkuu PM kuna mambo mengine sio lazima kutoa neno kwa ukubwa wako.
Haeleweki anataka nini, uko uzi wake mmoja anadai kwa mikataba yake na makampuni kadhaa ilivunjwa baada ya kumuuliza swali Jiwe, na kwamba hakutekwa kwa vile yeye na jiwe walikuwa kabila moja.

Lakini baadaye akadai Jiwe hahusiki ila Wapambe wake! unawezaje kumuelewa huyu mtu? Kwahiyo mbona Wapambe hawakumteka au nao walikuwa kabila moja?
 
Sio kwa ubaya ila aeleweki kabisa na kwa bahati mbaya yawezekana yeye hajalijua hilo. PM ana heshima yake ila anapambana sana kuishusha kwa mambo kama haya.
 
Kuchutama ndo lugha gani? Hivi Kuna mtu yeyote alisema chochote, na kuharibu dignity ya Gwajima?
 
Gwajima akae kimya kwasababu gani hivi paschal tayari baada ya kufikia umri huo unataka uturudishe nyuma tuishi kama watu wa zama za kizamanj dawa ya mtu muuaji nikumsema hadharani bila kuficha uovu wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…