cassavaleaves
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 2,169
- 2,540
Wanabodi,
Mimi ni mkazi wa Jimbo la Kawe, Mbunge wetu, Mhe. Askofu Josephat Gwajima, japo ni Mbunge mchapakazi ila ni mtu wa ahadi nyingi ambazo hazijatekelezwa.
Japo alipanga kuzitekeleza awamu ijayo, lakini kukatokea bahati mbaya, mdomo umeponza kichwa!, ameteleza na kuanguka kwenye tope, hivyo amevuliwa nguo!.
Ukivuliwa nguo, Chutama!.
Hivyo imetokea amevuliwa nguo hadharani na kubaki mtupu!, uchi wa mnyama!. Dawa pekee ya kumnusuru na aibu na kumtunzia kaji dignity kadogo alichobakiwa nacho, Mbunge wetu wa Kawe na MNEC wa CCM, Baba Askofu Dr. Josephat Gwajima, ni kuchutama tuu!, kujisetiri!.
Miongoni mwa sifa zake kuu za pekee, Askofu Gwajima, ni mzee wa kuliamsha dude!, na hua analiamshia kanisani kwake katika ibada za Jumapili.
Kuna vitu fulani mimi navijua lakini sivisemi, hivyo namshauri mbunge wangu, Askofu Gwajima, this time around, asiliamshe DUDE!, na badala yake aendeshe tuu ibada yake kama kawaida as of nothing happened!, atanishukuru!
Najua kuna wengi wangetamani kumuona akiliamsha DUDE, sii busara kuliamsha DUDE this time around kwasababu fulani!.
Kuna type fulani ya watu ni impulsive, ukimprovoke, anaprovokika, analipuka!, lakini kumbe hawajui kuwa kumbe sometimes kunyamaza kimya ni jibu kubwa na zuri kuliko kulipuka!.
Hadithi ya Kuoga Mtoni na Nguo Kutokomea!
Kuna simulizi ya watu wawili waliokuwa wanaoga mtoni.
Kuogo mtoni ni unavua nguo zote unabaki kama ulivyozaliwa.
Kumbe yule jamaa anayeoga ni kichaa! kijiji kizima wanamjua huwa anatembea hivyo kama alivyo zaliwa!.
Mara yule jamaa akachoropoka kwenye maji hapo mtoni, akaenda kuzichukua nguo zote za yule jamaa!.
Ungekuwa wewe ungeamua nini?.
1. Kwasababu wewe ni fighter, huwezi kuacha mtu akuchezee, hivyo utaamua kutoka kwenye maji na kumkimbiza mwizi wako kuokoa nguo zako ambazo ni haki yako?
2. Kuchutama, na kuziachia nguo ziende!, japo utaonekana zoba, jinga, hujui kupigania haki yako, utachekwa na kudharaulika jitu lioga, linashindwa kukimbiza mwizi!.
Uamuzi huu wa kuchutama ndio uamuzi sahihi na wa busara!.
Je tumchagize Askofu Gwajima aliamshe DUDE au achutame?.
Paskali
Mkuu Pascal: Nani kavuliwa nguo hasa? Rais kashindwa kabisa kupangua hoja! Na ameleta maswali mengi mno. Tukubali Serikali imekuwa na kama wiki mbili ngumu hivi karibuni, na yote ni kauli za Rais.
Angekaa kimya kwa hili Rais na kuonyesha amempuuza Gwajima mengi yasingezungumzwa. Hebu angalia swala la wanaharakati kutoka Kenya, hili lilikuwa sana sana la Mkurugenzi wa Uhamiaji, mbona nchi hii imerudisha watu wengi makwao! Kuna kuwapa masaa 12 au 48, na kuna kuwarudishia mipakani, na pia kuwapeleka Mahakamani. Lakini kuwarudisha kwa kuwapiga, na halafu Rais anatoka kwenye Kadamnasi bila aibu na kulizungumzia, hii inafikirisha sana Mkuu, inaonekana kuongoza nchi kwa kufuata utawala wa Sheria ni ngumu mno! Na ugonjwa huu unaanzia ofisi kuu ya nchi!
Kwa kifupi ni Serikali ndio inabidi ichutame!