Zegreaty
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 2,504
- 3,188
Mkuu kwanza pole na maswahibu yale uliyopitia kulingana na mahojiano yako, ila kwamasikitiko sana with all due respect mkuu unaonekana huja recover bado honest kabisa,sasa hapo aliepaswa kuchutama ni nani? Hebu tueleze kidadavuzi kosa la Gwajima ni lipi? Tunakubaliana kabisa Gwaji ni mmoja wa watu wa hovyo tulionao lakini haiondoi ukweli kua alischokisema sio kitu cha hovyo hata kidogo ni mtetea maslahi pekee ndio atapingana na Gwaji, Je mlitaka atoe mfano wa nani juu ya kupotea? Mbona viongozi wakigusiwa kuhusu kupotea watu wanatoa mifano ile watu walioenda kwa waganga huko hatusikii mkitoa milio hawawagusi walengwa husika? Au wewe binafsi unafurahishwa na mambo haya mkuu unaona sawa na unaona wewe uko salama kwakua ni mwanasisiemu? Mkuu huo ndio uzalendo manaohubiri kwa Taifa letu? Vifo nakupotea kwa watu wanaowakosoa mnaona ni sahihi kwaajili ya maslahi yenu? Taifa mnadhani mna haki miliki yakufanya lolote? Mwisho wa siku sote njia yetu ni moja na Mungu hadhihakiwiWanabodi,
Mimi ni mkazi wa Jimbo la Kawe, Mbunge wetu, Mhe. Askofu Josephat Gwajima, japo ni Mbunge mchapakazi ila ni mtu wa ahadi nyingi ambazo hazijatekelezwa.
Japo alipanga kuzitekeleza awamu ijayo, lakini kukatokea bahati mbaya, mdomo umeponza kichwa!, ameteleza na kuanguka kwenye tope, hivyo amevuliwa nguo!.
Ukivuliwa nguo, Chutama!.
Hivyo imetokea amevuliwa nguo hadharani na kubaki mtupu!, uchi wa mnyama!. Dawa pekee ya kumnusuru na aibu na kumtunzia kaji dignity kadogo alichobakiwa nacho, Mbunge wetu wa Kawe na MNEC wa CCM, Baba Askofu Dr. Josephat Gwajima, ni kuchutama tuu!, kujisetiri!.
Miongoni mwa sifa zake kuu za pekee, Askofu Gwajima, ni mzee wa kuliamsha dude!, na hua analiamshia kanisani kwake katika ibada za Jumapili.
Kuna vitu fulani mimi navijua lakini sivisemi, hivyo namshauri mbunge wangu, Askofu Gwajima, this time around, asiliamshe DUDE!, na badala yake aendeshe tuu ibada yake kama kawaida as of nothing happened!, atanishukuru!
Najua kuna wengi wangetamani kumuona akiliamsha DUDE, sii busara kuliamsha DUDE this time around kwasababu fulani!.
Kuna type fulani ya watu ni impulsive, ukimprovoke, anaprovokika, analipuka!, lakini kumbe hawajui kuwa kumbe sometimes kunyamaza kimya ni jibu kubwa na zuri kuliko kulipuka!.
Hadithi ya Kuoga Mtoni na Nguo Kutokomea!
Kuna simulizi ya watu wawili waliokuwa wanaoga mtoni.
Kuogo mtoni ni unavua nguo zote unabaki kama ulivyozaliwa.
Kumbe yule jamaa anayeoga ni kichaa! kijiji kizima wanamjua huwa anatembea hivyo kama alivyo zaliwa!.
Mara yule jamaa akachoropoka kwenye maji hapo mtoni, akaenda kuzichukua nguo zote za yule jamaa!.
Ungekuwa wewe ungeamua nini?.
1. Kwasababu wewe ni fighter, huwezi kuacha mtu akuchezee, hivyo utaamua kutoka kwenye maji na kumkimbiza mwizi wako kuokoa nguo zako ambazo ni haki yako?
2. Kuchutama, na kuziachia nguo ziende!, japo utaonekana zoba, jinga, hujui kupigania haki yako, utachekwa na kudharaulika jitu lioga, linashindwa kukimbiza mwizi!.
Uamuzi huu wa kuchutama ndio uamuzi sahihi na wa busara!.
Je tumchagize Askofu Gwajima aliamshe DUDE au achutame?.
Paskali
Mika 6:8
*"Bwana amekuambia ni nini kizuri, na anachotaka kwako ni hiki: kutenda haki, kupenda fadhili, na kutembea kwa unyofu na Mungu wako.
Qur’an 49:9
"Ikiwa makundi mawili ya Waumini yanapigana, basi yapatanishi kati yao. Ikiwa kundi moja linadhulumu lingine, basi mpiganeni na lile linalodhulumu."
. Hadith ya Nabii (S.A.W)
"Mwenye kuyakumbatia miongoni mwenu uovu, anapaswa kuubadilisha kwa mkono wake (kiungu); kama hana uwezo, basi kwa lugha yake; na kama hana uwezo, basi kwa moyo wake – na hiyo ndiyo imani dhaifu zaidi."*
(Sahih Muslim – inasisitiza wajibu wa kila mtu kupinga uovu kwa njia anayoweza.
Efeso 5:11
"Wala msiushirikiane katika matendo ya giza yasiyo na matunda; bali, msiwaadhibu."
(Wakristu wanatakiwa kukataa na kukemea mambo ya uovu.)
Sasa Mkuu kama dini zote zinakataa uovu nyie ni nani hadi muone anaepinga Uovu amefanya makosa? Muda utaongea na kila mtu atalipia uovu wake mbele za Mungu.