Ushauri wa bure kwa benki ya NBC kwenye udhamini wa ligi ya Tanzania

Ushauri wa bure kwa benki ya NBC kwenye udhamini wa ligi ya Tanzania

kocha Nabi

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2022
Posts
709
Reaction score
1,881
Habari wakuu,

Nikiwa kama mfanyabiashara ninayeanza kujikita katika hii tasnia huwa kuna hali inanijia kwa asilimia kubwa vitu ninavyokutana navyo huwa nahusisha sana na biashara.

Katika pilika zangu nikajikuta nachukia sana matangazo wanayofanya NBC kwenye udhamini wa ligi yaani hayaakisi na sehemu walipowekeza.

Kwanza kabisa ligi yetu ni ligi bora sana kwa afrika kwa sasa, lakini sijafahamu kama watu wa marketing kwa hii benki kama amekieka hiki kitu kwenye akili ama ni juu juu tu.
- Nilitegemea kuona matangazo yatakayovutia wateja ili wazidi kutumia bank yao kupitia hii league, na sio tu lile tangazo lao na majezi ya simba na yanga.

Sijajua sheria zao za mikataba ila

1. Nilitamani hata watu wanaotumia kadi ya nbc wawe na gate zao ukifika unamulika kadi unaingia bila bugudha na hii ingeendana na baadhi ya ofa kwa wanaonunua tiketi kupitia hii bank.

2. Nilitamani kama sheria zao zinaruhusu wachezaji wote wa ligi kuu mishahara wawe wanapokelea hii bank.

3. Nilitamani kuona kuna priority yoyote ile kwa mtu anayemiliki kadi ya nbc kwenye mambo yanayohusu ligi kuu na tim zake kama vile, kuwe na vituo maalum vya kuuza jersey kipindi cha kutambulisha jersey kwa wanaotumia kadi ya NBC pekee ili kuwaondolea msongamano na yamkini hata wakipata punguzo la bei itakuwa vyema.

4. Nilitamani kuona matangazo ambayo yatahusisha huduma zao i.e how easy they are, fast, simple, transparent and security. kwa kupitia hii hii platform ya ligi kuu ikiwezekana wanamodify kidogo kuleta umakini kwa walengwa. (japo hili lipo ila kwanza halisikiki ni kuimba tu visivyoeleweka)

Kama nilivyotangulia kusema hapo awali sijajua sheria zao na naongeza sifahamu kwa undani wao mipango waliyopanga ila hawajanifurahisha na promotion yao.
 
Back
Top Bottom