Ushauri wa bure kwa mtoto wa Bakhresa ambaye ni Mjumbe wa bodi ya TANESCO nchini kwa sasa

Ushauri wa bure kwa mtoto wa Bakhresa ambaye ni Mjumbe wa bodi ya TANESCO nchini kwa sasa

walidhani madudu yao yatafichika tena kama kipindi cha baba yao( 2015 kurudi nyuma) walivyotupiga kweli kweli na tukachakaa vilivyo kwa ulafi wao

Magu alitufumbua watanzania namna nchi ilivyoliwa walivyo hawana akili wanarudi tena na style zile zile za zamani wakidhani tumesahau
 
walidhani madudu yao yatafichika tena kama kipindi cha baba yao( 2015 kurudi nyuma) walivyotupiga kweli kweli na tukachakaa vilivyo kwa ulafi wao

Magu alitufumbua watanzania namna nchi ilivyoliwa walivyo hawana akili wanarudi tena na style zile zile za zamani wakidhani tumesahau
Mkuu Magufuli aliacha kafunua uozo wote serikalini
 
Africa yote haiaminiki asikudanganye mtu
Siku zinaenda kasi sana leo uko kwenye kasri na unaendesha Porsche halafu ghafla unajikuta una pingu na kesi ya uraia na uhujumu uchumi

Kesi haiishi mpaka anakuja kiongozi mwingine miaka 10
 
kwa kuwasaidia tu, mtoto wa bakhresa ambaye january makamba alimteua kuwa mjumbe wa bodi ya tanesco ni abubakar bakhresa.

jamaa ni msomi na very smart. binafsi bado nashangaa namna alivyojiingiza kwenye mtego wa january makamba. naungana na hoja ya mleta mada. ajitoe haraka kabla hajachafua image ya biashara yao.
 
Dogo awe makini hawa wezi wanatafuta kichaka cha kufichia ukwapuzi wao hii itapelekea kuharibu taswira yao kiutendaji
wewe bila shaka unazungumzia yusufu bakhresa. sio huyo.

mjumbe wa bodi ya tanesco ni abubakar bakhresa
IMG_20211122_233907.jpg
 
Fahamu katika bodi hiyo umechanganywa na watu wasio waaminifu kwa taifa hili, wana tuhuma za wazi kabisa za ubadhirifu wa mali za umma, akiwemo Waziri wako wa nishati.
Hizi tuhuma unazomtupia waziri wa nishati una ushahidi nazo wa kutosha? Au umeamua kumchafua tu?
 
Nakuomba uzingatie ushauri huu ninaokupatia kwa sasa, kwani una faida kwako binafsi na kwa kampuni yenu ambayo inajiendesha kwa uaminifu sana na ina jina zuri Nchini na nje ya nchi hii.

Kama hayati Magufuli hakuwatilia Shaka hakika nyie mna wema fulani wa kiwango cha juu kwa taifa hili, nakumbuka mpaka mlipewa eneo la kulima miwa ili mzalishe sukari kukidhi mapungufu ya sukari nchini, hiyo ni heshima unapaswa kuilinda ambayo mlipewa na kiongozi mkuu wa nchi.

January Makamba ni rafiki yako na urafiki wenu imefanya akuingize kwenye bodi ya Tanesco nchini.

Fahamu katika bodi hiyo umechanganywa na watu wasio waaminifu kwa taifa hili, wana tuhuma za wazi kabisa za ubadhirifu wa mali za umma, akiwemo Waziri wako wa nishati.

Kukubali kufanya kazi na hili kundi lenye tuhuma nzito inaonyesha na wewe kwa namna flani ni mtuhumiwa tarajiwa pindi mambo yatakapoharibika zaidi.

Watanzania wa leo sio wa Jana, wameamka, hivyo isijeonekana pesa inakwapuliwa nishati (Tanesco)kisha inaingizwa kwenye biashara yenu ya Bakheresa company kufanya mzunguko ili kujinufaisha.

Hali kadhalika mikataba ovu itakayoingiwa na wizara kwa lengo la kuhujumu taifa utahusika moja kwa moja bila kupepesa macho kama mjumbe wa bodi.

Hiki ninachokuambia ndio kitatokea baadae nchi hii ina mengi , mtaingia kwenye tuhuma za kutumika na wanasiasa,na hapo baadae huwezi jua mtawala atakua nani na atachukua hatua gani kuhusiana na ukwasi wenu.

Kaa tafakari na fikiria nje ya box, unaziona hizi kelele za wananchi ya kinachoendelea wizara ya nishati, ni dalili isio njema kwako.

Bakheresa asije akawa Seti Sing wa baadae au Rugemalila. JIUZURU UJUMBE WA BODI
Nina uhakika huyu mtoto wa Bakhresa akiona kuna mambo ya hovyo yanaendelea ataachia ngazi. Sidhani kama atakubali kuchafua jina la makampuni na jina la familia yao ili kuwafurahisha hao unaowaita marafiki zake.
 
Bado najiuliza sana kama kisiwa cha ukerewe ni sehemu ya Tanzania hii ya viwanda.
 
Back
Top Bottom