Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kenya sasa hivi kuna sintofahamu. Tume ya Uchaguzi imegawanyika, na imetoa tamko rasmi kwamba haiwezi kutoa guarantee uchaguzi ukifanyika wiki hii utakuwa huru na haki. Kamishna mmoja wa Tume hii alishatoa maelezo kwamba tume inapokea maelekezo "kutoka juu". Kwa sasa Uhuru anataka kulazimisha uchaguzi ufanyike, badala ya yeye kuachia uraisi kwa Spika wa Bunge kulingana na katiba ya Kenya, iwapo uchaguzi hautafanyika ndani ya siku 60 baada ya kubatilishwa.
Uhuru anasahau kwamba akilazimisha uchaguzi, matokeo yake yatapelekwa tena Mahakamani na kuna uwezekano mkubwa uchaguzi wa marudio kubatilishwa tena na Mahakama! Juzi hapa Uhuru alitoa mwito kwa raia wa Kenya kuiombea amani. Lakini je, suluhisho la Kenya ni kuiombea amani? Amani ili nani awe Raisi wa Kenya, Uhuru? Odinga?
Ukweli ni kwamba kwa hali iliyofikia Kenya kwa sasa, ushindi wa uraisi kwa Uhuru au Odinga hautakuwa ushindi kwa Kenya. Kenya imegawanyika mno kwa sasa, na ukiangalia kwa makini utaona kwamba ukabila ni chanzo kikubwa cha mgawanyiko wa kisiasa uliopo. Wajaluo hawatakubali kamwe ushindi wa Uhuru, na Wakikuyu hawatakubali kamwe ushindi wa Odinga.
Ushauri ninaotoa kwa Wakenya ni kwamba, wakataeni wote Uhuru na Odinga. Tafuteni raisi kutoka makabila madogo nchini Kenya ambayo hayajafungamana na Wakikuyu au Wajaluo. Hilo ndilo suluhisho pekee litakaloleta amani nchini Kenya kwa sasa.