Mimi ninafanya kazi za ukaguzi. Kati ya mentality mbaya sana yetu wakaguzi Ni KUTAFUTA MAKOSA.
Kupambania kutafuta PERFECTIONISM wakati wa UKAGUZI.
Mimi nipo pia kituo cha Afya, na huwa najishughulisha sana na UJAZAJI wa fomu za Bima.
Hakuna watu wapuuzi Kama watu wa Bima.
Kiuhalisia, FRAUDS ipo kwasababu both NHIF na Watoa Huduma wanachofanya Ni KUTAFUTANA na KUVIZIANA.
Hata ujaze vizuri vipi hizo forms za BIMA lazima watatafuta makosa na watakukata pesa.
Imagine, unapeleka CLAIMS za 2M wanakata 1.2M wanakulipa laki 8???
Makosa yenyewe utaambiwa:
- Tulipigia simu mgonjwa kasema Huduma zilizoandikwa siyo kweli.
- Mgonjwa uliye-claim anakaguliwa kuanzia Mapokezi, Dispensing, Leja ya Daktari mpaka Maabara Kama hayupo hiyo kesi. Ujue hawalipi.
- Sometimes, unaambiwa tu Kwa level ya Kituo cha Afya ilivyo dawa fulani hukutakiwa kutoa kwanini ulitoa?
- Mara mtu aliyetoa dawa hakutakiwa kutoa.
Ujinga kibao ilimradi wasilipe tu.
Na hata kama wakipata, imagine Paracetamol NHIF wanalipa Tsh 20 kwa kidonge. Sasa private wao watakuwa wananuaje??
Sidhani kama unajua unachozungumza hapa.
NHIF imejaa Watumishi VILAZA kupindukia kwasababu wanalipana mishahara ya KUTISHA kabisa. Akili Hakuna Ni michongo mingi ndio maana mfuko unafilisika na mhanga mkubwa Ni WATOA HUDUMA na WANACHAMA.
Sasa hivi, watoa Huduma wakiona mteja wa NHIF wanaugua kabisa.
Wamejitahidi mpaka kuanzisha madirisha ya wateja wa NHIF pekee ili kujaribu kupunguza hizi drama za hao wapuuzi lakini wapi.
Ndio maana Hakuna hospital serious Kama Aghakhana watachukua hivi vikadi vya kibwege vya NHIF.
In short, NHIF sasa hivi Ni takataka kabisa