Ushauri wa Bure kwa Waziri Ummy Mwalimu kuhusu NHIF

Umeongea point muhimu sana wakifuata hu ushauri NHIF watafanikiwa maana vituo vingine kupima maralia tu elfu 20 na NHIF wanalipa

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Kwani bodi ya NHIF ina compose kina nani (kwa majina) ?

Mwenye kujua tafadhali atuletee hapa hiyo taarifa.

Na Mwenyekiti wa hiyo board ni nani ?

Je bado ni Bibi wa Sensa ?

Au kwa sasa ni nani?
 
Mimi ninafanya kazi za ukaguzi. Kati ya mentality mbaya sana yetu wakaguzi Ni KUTAFUTA MAKOSA.

Kupambania kutafuta PERFECTIONISM wakati wa UKAGUZI.

Mimi nipo pia kituo cha Afya, na huwa najishughulisha sana na UJAZAJI wa fomu za Bima.

Hakuna watu wapuuzi Kama watu wa Bima.

Kiuhalisia, FRAUDS ipo kwasababu both NHIF na Watoa Huduma wanachofanya Ni KUTAFUTANA na KUVIZIANA.

Hata ujaze vizuri vipi hizo forms za BIMA lazima watatafuta makosa na watakukata pesa.

Imagine, unapeleka CLAIMS za 2M wanakata 1.2M wanakulipa laki 8???

Makosa yenyewe utaambiwa:

  • Tulipigia simu mgonjwa kasema Huduma zilizoandikwa siyo kweli.
  • Mgonjwa uliye-claim anakaguliwa kuanzia Mapokezi, Dispensing, Leja ya Daktari mpaka Maabara Kama hayupo hiyo kesi. Ujue hawalipi.
  • Sometimes, unaambiwa tu Kwa level ya Kituo cha Afya ilivyo dawa fulani hukutakiwa kutoa kwanini ulitoa?
  • Mara mtu aliyetoa dawa hakutakiwa kutoa.
Ujinga kibao ilimradi wasilipe tu.

Na hata kama wakipata, imagine Paracetamol NHIF wanalipa Tsh 20 kwa kidonge. Sasa private wao watakuwa wananuaje??
2.Review bei za dawa na gharama za upasuaji

---kuna dawa zinanunuliwa kwa pesa ndogo sana ila NHIF wanalipa karibu mara 3 mpaka 4 ingawa kuna baadhi mna punja .
Sidhani kama unajua unachozungumza hapa.
NHIF imejaa Watumishi VILAZA kupindukia kwasababu wanalipana mishahara ya KUTISHA kabisa. Akili Hakuna Ni michongo mingi ndio maana mfuko unafilisika na mhanga mkubwa Ni WATOA HUDUMA na WANACHAMA.

Sasa hivi, watoa Huduma wakiona mteja wa NHIF wanaugua kabisa.

Wamejitahidi mpaka kuanzisha madirisha ya wateja wa NHIF pekee ili kujaribu kupunguza hizi drama za hao wapuuzi lakini wapi.

Ndio maana Hakuna hospital serious Kama Aghakhana watachukua hivi vikadi vya kibwege vya NHIF.
Kwenye Afya za watu biashara itolewa na NHIF kama mfuko wa Taifa kisiwe ndio chanzo cha Kutajirika watu huku huduma zinazorota .
In short, NHIF sasa hivi Ni takataka kabisa
 
Hongera mkuu kwa Uchambuzi mzuri na wa msaada kwa Taifa
 
Hao wanaokufanyia vipimo ukiwa na kadi yako ya NHIF washukuru sana, mtindo uliopo Sasa hivi vituo vingi vinaminya vipimo na dawa ambavyo ulipaswa kufanyiwa.
 
Hivi nauliza.mbona huwa nikienda naambiwa ni sign form kabla ya kuhudumiwa.hivi hapa haiwezekan wakajaza madawa nisiyopew!? Na kwanin isiwe wanafunga kama balance sheet kuzuia kuongezwa dawa
Hairuhusiw ku sign kabla hujapewa huduma japo hata usipo sign haibadirishi wao kuongeza dawa ama vipimo
 
Hao wanaokufanyia vipimo ukiwa na kadi yako ya NHIF washukuru sana, mtindo uliopo Sasa hivi vituo vingi vinaminya vipimo na dawa ambavyo ulipaswa kufanyiwa.
mfuko huu umeharibika sana
 
Mim sijajua ila kuna baadh ya huduma naonaga bora nikalipe tu kuliko kwenda kunyanyasika na kadi ya bima.inangawa tunachangia kila mwez
 
Mim sijajua ila kuna baadh ya huduma naonaga bora nikalipe tu kuliko kwenda kunyanyasika na kadi ya bima.inangawa tunachangia kila mwez
Of course, NHIF inadhiofika kila siku. Maana NHIF wenyewe wanasumbua kwa VIJISABABU visivyokuwepo.
 
Kwanini zisijengwe hospitali ambazo ni za serikali specifically zikawa zinaendeshwa na bima ya NHIF badala ya kuhangaika na mahospitali private.

Yani mfano badala ya NSSF kujenga majengo useless kila kona ya mji wangejenga hospitali ambazo jengo hadi wahudumu ni wa NHIF wenyewe tu. Kusiwe na muingiliano wa maslahi.
 
Wanasemaga siasa ndio maisha yao !!
 
Hiyo ndio dawa pekee !!
 
Ummy yuko sahihi katika hili,
Hakuna maana ya kuwa na Ada ya kumuona daktari, usichanganye ada ya kumuona daktari na allowance
Kwamba kumuona daktari ni kuingia kumuangalia na kutoka nje ? au kuna mambo mengine kama kupokea maelezo yako ,kujua kutokana na maelezo yako vipimo vipi au matibabu yapi utahitaji , kuna Ushauri pia na haya ndiyo yanafanya kuwe na pesa ya kumuona Daktari .
 
Kutoa maelezo ya vipimo au matibabu yapi utahitaji ndio sehemu ya kazi ya Daktari, ndio maana analipwa Mshahara kwa kazi hiyo. Kama ni extra kazi anazofanya ndio maana kuna EDA, On call allowances etc, hii kitu inaitwa malipo ya kumuona Daktari inafanya Watanzania wengi wasiende kucheki Afya zao, yaani Mtu alipie kumuona Daktari then alipie matibabu, doesn't make sense
 
Hivi unalipia kumuona daktari akiwa uchi au amevaa nguo??
 
Kwa sisi tunaojua mfuko wa Bima ulikotoka, uongozi wa sasa ni bora zaidi na umepunguza fraud kiasi kikubwa. Usingekuwa uongozi wa sasa haya yote usingeyasikia.

Fraud kwa NHIF zinafanywa na

1. Vituo vya afya na hapa hasa ni private, public si sana.
3. Wagonjwa na watumishi wa afya. Mgonjwa anaweza akawa anataka maziwa ya mtoto, akaenda hospitali kwa kushirikiana na watumishi wa afya wakatengeneza ugonjwa mkubwa ambao dawa zake hazikuwepo hospitali. Labda mgonjwa anaandikiwa dawa zenye thamani ya laki 5 lakini hazipo hospitali. Akipewa form 2c (ambazo zimefungiwa kwa sasa) na kwenda kuchukua dawa pharmacy, kule wanaweza kubaliana kumpa maziwa au pesa au chochote alichonacho kilichopo pharmacy. Hapa hapakuwa na uaminifu kati ya Vituo vya Afya, Pharmacy binafsi, Watumishi wa Afya, na wagonjwa. Wizi huu umefanyika sana Dar es salaam.
3. Watumishi wa NHIF wenyewe. Hawa wengi wao waliondolewa au kuzuiwa. Mfano huko nyuma vibali vya CT scan kwa siku vilikuwa vinatolewa kama elfu moja, lakini chini ya uongozi mpya wa sasa vibali vya NHIF vikapungua ha kufikia around 500 per day. Kazi ya nani? Mkurugenzi wa sasa. Pale NHIF watumishi wao walikuwa wanapiga deal kwa kuwaongeza wategemezi kwenye kadi za principal member bila kuwa na uhusiano. Haya mambo yameenda kwa muda hadi uongozi wa sasa ulipokuja kurekebisha.
4. Serikali kuingiza siasa kwenye mfuko. Mfano kuanzisha vifurushi ni wazo zuri sana, maana kunaongeza wigo. Shida ni aina ya watu wanaofungua vifurushi ni wale wanaoumwa. Wanaenda kula pesa za mfuko. Lakini pia serikali inaposema mfuko utakufa unatumia kiasi ABC kutibu magonjwa sugu wawe wanatuambia wanakusanya kiasi gani na walitaka mfuko uwe unatibu magonjwa gani.

Siasa ikiondoka, uongozi wa sasa wa NHIF utatosha kabisa kusukuma gurudumu la NHIF.
 
Reactions: RNA
sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…