Ushauri wa Bure: Ukijikwaa ukaanguka, usiangalie tu pale ulipoangukia, bali angalia pale ulipojikwaa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Chadema ilijikwaa, ikaanguka, ikaangalia tuu pale ilipoangukia, ikainuka, ikaendelea na safari, bila kuangalia ilipojikwa, sasa imejikwaa tena pale pale, Ila bado haijaanguka, hivyo huu ni ushauri wa bure wa kuisaidia this time around, isianguke!.

Mtu unapokuwa umejaaliwa uwezo wa kuona mabaya fulani kupitia kitu kinachoitwa precognition kuwa yatawatokea watu fulani, usipowaambia, halafu yakatokea, utaumia sana kwa a guilty conscious kuwa I saw it coming but you did nothing to help out!. Lakini ukiona jambo baya kinakuja, ukiwaambia, unaweza kuzuia, ila ukiwaambia, wakapuuza, yakija kutokea ya kutokea, angalau hupati a guilt conscious ya dhamira yako kukusuta maana uliwaambia!.

Hivyo hili ni Bandiko la kujitolea kutoa msaada wa bure kabisa
kwa Chadema kwa kuwaelimisha kuhusu kitu kinachoitwa karma ni nini na kinafanyaje kazi "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Japo Wana Macho, Hawaoni!
Japo watu wote wana macho, wengi wana macho ya nje tuu yanayoona vitu vya nje, lakini hawana jicho la ndani (jicho la roho) kuona vitu visivyoonekanika kwa macho ya kawaida, hivyo wanasemwa kuwa wana macho lakini hawaoni.

Japo Wana Masikio, Hawasikii!
Vivyo hivyo kwa masikio, watu wengi wana masikio na wanasikia, ila masikio yao ni masikio ya nje, yanayosikia sauti za nje tuu, lakini hawana sikio la ndani (sikio la roho) kuweza kusikia sauti za ndani "voices from within" hivyo wanasemwa kuwa wana masikio lakini hawasikii.

Jicho la Ndani na Sikio la Ndani
Kila kiumbe anacho ila tumetofautiana sana uwezo wa kutambua, mfano kuna wanyama wana uwezo mkubwa zaidi ya binadamu kutambua hatari. Mfano mbwa anapotumia pua kunusa, amini usiamini, anachonusa sio harufu bali ni sauti ya ndani. Hivyo wale mbwa wanusa mizigo airports au wale panya watengua mabomu, ni wanatumia jicho la ndani na sikio la ndani.

Kwa vile sio watu wote wamejaliwa uwezo wa kutumia jicho la ndani kuona hatari iliyo mbele yetu sisi tuliojaaliwa jicho hilo, na sikio hilo tukiona kitu na tukisikia kitu cha hatari kinakuja kutokea ni vizuri tukasaidia.

Kila tukio, linatokea kwa sababu, everything happens for a reason, hivyo likitokea jambo baya lolote, wengi huishia kwenye kuliangalia tukio tuu la nini kilichotokea na matokeo yake tuu, lakini hawajiulizi the underlying causes za kilichopelekea tukio hilo kutokea, the reasos behind the underlying causes and the consequences.

Hata wengi wakijikwaa na kuanguka, huinuka kujifuta vumbi na kuendelea na safari yao, huwa hawarudi kuangalia wamejikwaa wapi, ili wakipita tena njia hiyo, wasije wakajikwaa tena pale pale na wakaanguka tena vile vile.

Kwenye ile dhana ya usaliti wa ule "Waraka wa Mabadiliko", Chadema ilijikwaa mahali kwenye issue ya kumtiimua Zitto, na kiukweli imekula bakora za karma za kutosha, na wahusika wakuu wametandikwa bakora zao, Chadema ikaangukia, na wahusika wakaanguka, kisha wakasimama na kuendelea na safari yake bila ya kuangalia walipojikwaa bali walipoangukia. Ni Kwa nini Chadema wakijikwaa wakaanguka, wakainuka wakaangalia tuu walipoangukia na sio walipo jikwaa, kwasababu Chadema wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii.

Sasa kwenye hili la Halima Mdee, Chadema, imejikwaa tena pale pale ilipojikwa kwenye issue ya kumtumua Zitto, safari hii Chadema bado haijaanguka na bakora za karma bado hazijaanza kutembea.

Kwa vile Zitto alikimbilia mahakamani akashindwa, Chadema wakashangilia ushindi huo, nashukuru mimi niliwaeleza humu kuwaelimisha kuhusu karma, na nikawaambia the consequences ya matendo, hivyo kwenye hili la Halima Mdee, nae amekimbilia mahakamani, ikitokea na Halima akashindwa kama alivyoshindwa Zitto, hivyo Chadema wakafanikiwa kuwatimua rasmi hao wanaowaita Covid 19, naomba mimi niwe mtu wa kwanza kuwaambia the consequences will be very devastating, kwenye karma ya Zitto, angalau someone survived miraculously, I'm not sure kwenye hili, if anyone will!. Kwa kuchelea this, nimejitolea kuishauri Chadema the right thing to do na kuepuka adhabu ya karma.

Dhana ya Usaliti
Sijui ni wanachama wangapi wa Chadema waliusoma ule Waraka wa Mabadiliko, ukiwa ni msomaji mzuri wa maandishi ya mtu fulani, unajikuta unapata skills zinazoitwa graphology, ambapo ukisoma andiko fulani unamjua mwandishi ni nani, Waraka ule wa Mabadiliko sio kazi ya Zitto ile, mimi najua ni kazi ya Nani!.

Contents za Waraka huo ni hoja za ukweli tuu, na sio kweli kuwa lengo la waraka ule ni kufanya Mapinduzi ya uongozi wa juu, waraka ule ulikuwa ni waraka wa kuunda kitu kinachoitwa "a winning coalition" na kuitumia hiyo winning coalition kushinda nafasi zote za uongozi wa juu ndani ya Chadema kwenye uchaguzi wa ndani.

Kwanini Chadema Itandikwe na Karma?.
Karma inataka haki bin haki.
Kwa mujibu wa katiba ya Chadema, CC ya Chadema inauwezo tuu wa kumsimamisha NKM lakini sio mamlaka yake ya nidhamu, hivyo CC ya Chadema haikuwa na uwezo wa kumfukuza Zitto. Mamlaka halali ya nidhamu ya NKM ni Baraza Kuu na mamlaka ya Rufaa ni Mkutano Mkuu. CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Zitto?. Bakora za karma zimeshughulikia.

The same same scenario ya kutumbuliwa kwa Zitto, imejirudia katika kutimuliwa kwa Halima Mdee, CC ya Chadema ina uwezo wa kumsimamisha tuu Mwenyekiti wa Bawacha, lakini sio mamlaka yake halali ya nidhamu. Mamlaka halali ya nidhamu ya Halima Mdee ni Baraza Kuu na mamlaka yake ya Rufaa ni Mkutano Mkuu. CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Mdee?. Bakora za karma zitashughulikia!.

A Way Forward
  1. Kitu muhimu cha kwanza kwa Chadema kufanya ni kutengua maamuzi yote kuwahusu hao wabunge 19 kuwa bado ni wanachama halali wa Chadema na kuwakubalia waendelee na ubunge wao.
  2. Baada ya kurejeshewa uanachama wao, wafute kesi iliyopo mahakamani
  3. Chadema kufanya a due process, uteuzi wao ulifanyikaje. Ikijiridhisha kuna jinai then waripoti rasmi polisi.
  4. Kule wathibitishe jinai ya forgery imefanywa na polisi kufanya uchunguzi wa kijinai na ikithibitishwa tuu jinai hiyo, then ni NEC ndio watakao watengua ubunge wao.
  5. Process ya mashitaka ya ndani ifanyike kwa mujibu wa katiba ya Chadema.
  6. Only ring leaders ndio waadhibiwe kwa kulazimishwa kuomba msamaha, na kuvuliwa vyeo vyote wabaki wanachama wa kawaida.
  7. Na wakosaji hao wakishupaza shingo zao then watimuliwe kwa haki na sio kwa kutumia a Kangaroo Court kama mwanzo.
  8. Hili likifanyika, Chadema itakuwa imewatendea haki wanachama wake.
  9. Adhabu ya bakora za karma ninazoziona hazitakuja, hazita itandika Chadema, Chadema itakuwa salama na viongozi wake watakuwa salama.
  10. Chadema will prosper again, uchaguzi wa 2025 watashinda baadhi ya majimbo.
Mwenye macho na aone Mwenye masikio na asikie!.

Jumamosi Njema

Paskali.
 
Mkuu Paskali, huwa naheshimu mawazo yako mara nyingi lakini katika hili bado unaendelea kuji misdirect kwa utashi usiojulikana.

Siasa ni utashi na wa watu waliojiunga na nia moja kuendeleza kile wanacho amini.
Liangalie suala la kina Mdee kwa jicho tofauti na utaona mambo haramu ambayo kila mpenda ukweli lazima atakosa kuyaunga mkono.
Usiliangalie suala la Mdee kama la CHADEMA peke yake, lakini ni suala la Utawala Bora.

Kwanza kabisa ni FORGERY ya kuwapeleka kina Mdee bungeni, pengine Paskali unaliona ni la kirahisi rahisi tu.
CHADEMA are on record kuwa hawaja wapelekea majina NEC , ya hao kina Mdee na wenzake 18!
Kama State Machinnery ikishirikiana na Bunge(hii ni mihimili miwili) kufanya kazi kwa kutumia fake documents, basi kuna tatizo kubwa sana .
Kama leo Dola likiamua kwa kushirikiana na Bunge kufanya lolote kwa kughushi nyaraka, hapo kuna basic contradiction katika uendeshaji wa dola.

Pili, kwa akina Mdee kukubali ubunge kwa matamanio ya kipato, huku wakijua chama chao hakiridhiki na hilo, huo ni usaliti!
Hao ni watu wa kununuliwa, wataaminika vipi?

Tujue kwa uhakika kuwa kitendo cha NEC kiliasisiwa na nani kupeleka majina ya kina Mdee na wezake 18?
Bunge kuwapa kina Mdee & Co ubunge on un authentic documents hakiungwi mkono, si na CHADEMA tu bali hata tunaolingalia swala kwa nje.

Na hapo karma itatenda kama inavyopaswa.
 
Wanabodi,
Heading imekaa vibaya the proper heading ni hii

"Ushauri wa Bure: Ukijikwaa Ukaanguka, Usiangalie Tuu Pale Ulipoangukia, Bali Angalia Pale Ulipo Jikwaa!.

Chadema ilijikwaa, ikaanguka, ikaangalia tuu pale ilipoangukia, ikainuka, ikaendelea na safari, bila kuangalia ilipojikwa, sasa imejikwaa tena pale pale, Ila bado haijaanguka, hivyo huu ni ushauri wa bure wa kuisaidia this time around, isianguke!.

Mtu unapokuwa umejaaliwa uwezo wa kuona mabaya fulani kupitia kitu kinachoitwa precognition kuwa yatawatokea watu fulani, usipowaambia, halafu yakatokea, utaumia sana. Lakini ukiwaambia, unaweza kuzuia, ila ukiwaambia, wakapuuza, yakija kutokea ya kutokea, dhamira yako haitakusuta maana uliwaambia.

Hivyo hili ni Bandiko la kujitolea kutoa msaada wa bure kabisa

kwa Chadema kwa kuwaelimisha kuhusu kitu kinachoitwa karma ni nini na kinafanyaje kazi.

Japo watu wote wana macho, wengi wana macho ya nje tuu yanayoona vitu vya nje, lakini hawana jicho la ndani (jicho la roho) kuona vitu visivyoonekanika kwa macho ya kawaida, hivyo wanasemwa kuwa wana macho lakini hawaoni.

Vivyo hivyo kwa masikio, watu wengi wana masikio na wanasikia, ila masikio yao ni masikio ya nje, yanayosikia sauti za nje tuu, lakini hawana sikio la ndani (sikio la roho) kuweza kusikia sauti za ndani "voices from within" hivyo wanasemwa kuwa wana masikio lakini hawasikii.

Jicho la ndani na sikio la ndani, kila kiumbe anacho ila tumetofautiana sana uwezo wa kutambua, mfano kuna wanyama wana uwezo mkubwa zaidi ya binadamu kutambua hatari. Mfano mbwa anapotumia pua kunusa, amini usiamini, anachonusa sio harufu bali ni sauti ya ndani. Hivyo wale mbwa wanusa mizigo airports au wale panya watengua mabomu, ni wanatumia jicho la ndani na sikio la ndani.

Kwa vile sio watu wote wamejaliwa uwezo wa kutumia jicho la ndani kuona hatari iliyo mbele yetu sisi tuliojaaliwa jicho hilo, na sikio hilo tukiona kitu na tukisikia kitu cha hatari kinakuja kutokea ni vizuri tukasaidia.

Kila tukio, linatokea kwa sababu, everything happens for a reason, hivyo likitokea jambo baya lolote, wengi huishia kwenye kuliangalia tukio tuu la nini kilichotokea na matokeo yake tuu, lakini hawajiulizi the underlying causes za kilichopelekea tukio hilo kutokea, the reasos behind the underlying causes and the consequences.

Hata wengi wakijikwaa na kuanguka, huinuka kujifuta vumbi na kuendelea na safari yao, huwa hawarudi kuangalia wamejikwaa wapi, ili wakipita tena njia hiyo, wasije wakajikwaa tena pale pale na wakaanguka tena vile vile.

Kwenye ile dhana ya usaliti wa ule "Waraka wa Mabadiliko", Chadema ilijikwaa mahali kwenye issue ya kumtiimua Zitto, na kiukweli imekula bakora za karma za kutosha, na wahusika wakuu wametandikwa bakora zao, Chadema ikaangukia, na wahusika wakaanguka, kisha wakasimama na kuendelea na safari yake bila ya kuangalia walipojikwaa bali walipoangukia. Ni Kwa nini Chadema wakijikwaa wakaanguka, wakainuka wakaangalia tuu walipoangukia na sio walipo jikwaa, kwasababu Chadema wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii.

Sasa kwenye hili la Halima Mdee, Chadema, imejikwaa tena pale pale ilipojikwa kwenye issue ya kumtumua Zitto, safari hii Chadema bado haijaanguka na bakora za karma bado hazijaanza kutembea.

Kwa vile Zitto alikimbilia mahakamani akashindwa, Chadema wakashangilia ushindi huo, nashukuru mimi niliwaeleza humu kuwaelimisha kuhusu karma, na nikawaambia the consequences ya matendo, hivyo kwenye hili la Halima Mdee, nae amekimbilia mahakamani, ikitokea na Halima akashindwa kama alivyoshindwa Zitto, hivyo Chadema wakafanikiwa kuwatimua rasmi hao wanaowaita Covid 19, naomba mimi niwe mtu wa kwanza kuwaambia the consequences will be very devastating, kwenye karma ya Zitto, angalau someone survived miraculously, I'm not sure kwenye hili, if anyone will!. Kwa kuchelea this, nimejitolea kuishauri Chadema the right thing to do na kuepuka adhabu ya karma.

Dhana ya Usaliti

Sijui ni wanachama wangapi wa Chadema waliusoma ule Waraka wa Mabadiliko, ukiwa ni msomaji mzuri wa maandishi ya mtu fulani, unajikuta unapata skills zinazoitwa graphology, ambapo ukisoma andiko fulani unamjua mwandishi ni nani, Waraka ule wa Mabadiliko sio kazi ya Zitto ile, mimi najua ni kazi ya Nani!.

Contents za Waraka huo ni hoja za ukweli tuu, na sio kweli kuwa lengo la waraka ule ni kufanya Mapinduzi ya uongozi wa juu, waraka ule ulikuwa ni waraka wa kuunda kitu kinachoitwa "a winning coalition" na kuitumia hiyo winning coalition kushinda nafasi zote za uongozi wa juu ndani ya Chadema kwenye uchaguzi wa ndani.

Kwanini Chadema Itandikwe na Karma?.

Karma inataka haki bin haki.

Kwa mujibu wa katiba ya Chadema, CC ya Chadema inauwezo tuu wa kumsimamisha NKM lakini sio mamlaka yake ya nidhamu, hivyo CC ya Chadema haikuwa na uwezo wa kumfukuza Zitto. Mamlaka halali ya nidhamu ya NKM ni Baraza Kuu na mamlaka ya Rufaa ni Mkutano Mkuu. CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Zitto?. Bakora za karma zimeshughulikia.

The same same scenario ya kutumbuliwa kwa Zitto, imejirudia katika kutimuliwa kwa Halima Mdee, CC ya Chadema ina uwezo wa kumsimamisha tuu Mwenyekiti wa Bawacha, lakini sio mamlaka yake halali ya nidhamu. Mamlaka halali ya nidhamu ya Halima Mdee ni Baraza Kuu na mamlaka yake ya Rufaa ni Mkutano Mkuu. CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Mdee?. Bakora za karma zitashughulikia!.

A Way Forward

Kitu muhimu cha kwanza kwa Chadema kufanya ni kutengua maamuzi yote kuwahusu hao wabunge 19 kuwa bado ni wanachama halali wa Chadema na kuwakubalia waendelee na ubunge wao.
Baada ya kurejeshewa uanachama wao, wafute kesi iliyopo mahakamani
Chadema kufanya a due process, uteuzi wao ulifanyikaje. Ikijiridhisha kuna jinai then waripoti rasmi polisi.
Kule wathibitishe jinai ya forgery imefanywa na polisi kufanya uchunguzi wa kijinai na ikithibitishwa tuu jinai hiyo, then ni NEC ndio watakao watengua ubunge wao.
Process ya mashitaka ya ndani ifanyike kwa mujibu wa katiba ya Chadema.
Only ring leaders ndio waadhibiwe kwa kulazimishwa kuomba msamaha, na kuvuliwa vyeo vyote wabaki wanachama wa kawaida.
Na wakosaji hao wakishupaza shingo zao then watimuliwe kwa haki na sio kwa kutumia a Kangaroo Court kama mwanzo.
Hili likifanyika, Chadema itakuwa imewatendea haki wanachama wake.
Adhabu ya bakora za karma ninazoziona hazitakuja, hazita itandika Chadema, Chadema itakuwa salama na viongozi wake watakuwa salama.
Chadema will prosper again, uchaguzi wa 2025 watashinda baadhi ya majimbo.
Mwenye macho na atazame ushauri huu, na mwenye masikio asikie.

Nawatakia Jumamosi Njema

Paskali.

Kada wa CCM aliyeambulia kura Moja ya wajumbe pale kawe
 
Makamanda, karibuni kwa maoni. Mkumbuke tu hii mada imeletwa humu jukwaani na Mwandishi na mchambuzi wetu nguli! Kada wetu wa ccm! Na pia Mtia nia wetu wa ubunge kule Kawe mwaka 2020 kupitia ccm!

NB: Kejeli na matusi hayakubaliki. Changia kwa staha! Toa maoni yako kuendana na mada iliyopo mezani. Maana inaweza kuwa anaitakia mema Chadema. Na asingependa kuona ikianguka kupitia hiki anachokiita karma.
 
Pascal alishauza mwili, na roho kwa lile shetani la kijani. Lile shetani linahitaji kafara ambayo hutolewa kwa mfumo wa sifa na mapambio yasiostahili kutolewa. Pia kafara zake hutolewa kwa kuwaponda wale wanaolipinga, hata kama hakipo chenye kustahili kupondwa.

Utaandika maandiko marefu, maneno mengi, ila kila mmoja anatambua unachokipigania. Ni matamanio yako kupata kiti kwenye meza ya shetani la kijani, ili na wewe ule na kunywa damu inayokamuliwa kutoka kwa walalahoi wa nchi hii. Njaa yako imehama kutoka tumboni, imepanda kichwani.

Haulitumikii taifa, hauwazi maslahi ya nchi. Unalitumikia tumbo lako, na umeweka mbele maslahi ya shetani aliekununua.

Shame on you Pascal!
 
Mkuu Pascal Mayalla naona umeenda kuwatibua chawa waliokuwa wamejificha kwenye kichwa cha mwendawazimu. Kichwa cha mwenda wazimu namaanisha 👉 (swala la masai wa mchongo wa ngorongoro) Sasa basi kwa vile chawa hao umewatibua inabidi na wewe uwahi kunyoa nywele ili wasije kukishambulia kichwa chako kwa hasira. BTW umeandika fact tupu. Ubarikiwe sana.
 
Attachments

  • images (32).jpeg
    images (32).jpeg
    30 KB · Views: 10
Mkuu Paskali, huwa naheshimu mawazo yako mara nyingi lakini katika hili bado unaendelea kuji misdirect kwa utashi usiojulikana.
Mkuu Jidu La Mabambasi , asante sana kwa kujiheshimu, na mimi pia sio tuu nakuheshimu, bali nawaheshimu members wote jf na hata madogo humu wakinitukana, mimi nawamwagia thanks.
Siasa ni utashi na wa watu waliojiunga na nia moja kuendeleza kile wanacho amini.
Liangalie suala la kina Mdee kwa jicho tofauti na utaona mambo haramu ambayo kila mpenda ukweli lazima atakosa kuyaunga mkono.
Usiliangalie suala la Mdee kama la CHADEMA peke yake, lakini ni suala la Utawala Bora.
Mimi interest yangu ni moja tuu, watendewe haki, kama ni kuhumiwa, wahukumiwe kwa haki.
Kwanza kabisa ni FORGERY ya kuwapeleka kina Mdee bungeni, pengine Paskali unaliona ni la kirahisi rahisi tu.
CHADEMA are on record kuwa hawaja wapelekea majina NEC , ya hao kina Mdee na wenzake 19!
Kama Chadema wanajijua hawajapeleka majina, hii inamaanisha kuna forgery imefanyika, forgery ni kosa la jinai, kwanini Chadema hawakuripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike?. Kama Chadema wangeripoti polisi, Chadema wangekuwa served na nakala halisi ya barua yao ya uteuzi kutoka Chadema, Chadema ndio wangethibisha ni fake NEC wangebatilisha uteuzi wao. Kwanini Chadema iwatimue wanachama wake kienyeji enyeji bila kufanya a due process kuuthibisha forgery na katika kuwatimua, kwanini Chadema iwatimue wanachama wake bila kufuata Katiba sheria taratibu na kanuni zake yenyewe walizojiwekea?.
Kama State Machinnery ikishirikiana na Bunge(hii ni mihimili miwili) kufanya kazi kwa kutumia faked dicuments, basi kuna tatizo kubwa sana .
Kama leo Dola likiamua kwa kushirikiana na Bunge kufanya lolote kwa kughushi nyaraka, hapo kuna basic contradiction katika uendeshaji wa dola.
This is a challenge.
Pili, kwa akina Mdee kukubali ubunge kwa matamanio ya kipato, huku wakijua chama chao hakiridhiki na hilo, huo ni usaliti!
Hao ni watu wa kununuliwa, wataaminika vipi?
Hii ni changamoto kati ya morality and the business of politics. Ubunge ni politics and fursa at the same time.
Tujue kwa uhakika kuwa kitendo cha NEC kiliasisiwa na nani kupeleka majina ya kina Mdee na wezake 19?
Hapa ndipo kulihitajika a due process to establish the truth. Mimi niliisikia sauti, voices from within kuhusu hili na nikaliketa humu, Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?
Bunge kuwapa kina Mdee & Co ubunge on un authentic documents hakiungwi mkono, si na CHADEMA tu bali hata tunaolingalia swala kwa nje.

Na hapo karma itatenda kama inavyopaswa.
Barua ya uteuzi wa wabunge hao 19 iliyotoka NEC kwenda kwa Spika it's authentic bonafide genuine letters.
P
 
You must possess the high level of IQ kuielewa siasa ya nchi hii,ugumu ni kwamba mabo nyeti ya kisiasa kama haya yana mkono wa Dark side deep state, hawa deep state wamegawanyika wapo mpaka upinzani na wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, sisi huku juu tunapangiwa ajenda za kujadili kutuchanganya,hivi inahitaji elim ya kiasi kujua kuwa suala hili lina mafungamano thabiti baina ya CDM na serikali?kweli jmn hamuoni?Pasco yupo mbele ya hili kifikra, anachokijua pasko cc wengine tutakuja kukiona after 2025.
 
Huwa unakuja na thread zako kuonesha kama vile una jambo jipya, lakini kwa msomaji aliyekuzoea, na anayejitambua upstairs, ataona bado unazunguka pale pale.

Thread zako nyingi kuizungumzia Chadema na hao covid huwa unakuja na allegations pekee, unatoa shutuma lakini kwa makusudi huwataji kwa majina unaowalaumu, ili tu uwalinde rafiki zako wasaliti waliowahi kufukuzwa Chadema.

Nikwambie kitu, kama kweli unakiamini unachoandika kuhusu kuwatetea hao unaodai wameonewa, wataje kwa majina wale waliowaonea, na uoneshe kwa ushahidi ni kwa vipi walihusika kwenye huo uonevu, lakini kinyume na hapo, wacha kuchezea akili za watu bro.

Mfano, unauzungumzia ule waraka wa 2014 uliowaondoa kina Zitto na wenzake, unadai "mashetani yako" yanakwambia aliyeuandika unamfahamu, ok, tutajie kwa jina huyo muhusika utuwekee na ushahidi wa namna alivyohusika kuandika ule waraka ili tuamini kweli kina Zitto walionewa.

Nakushangaa unaposema hao wasaliti wanaonewa wakati hatua za kinidhamu wanazochukuliwa ni zile zilizowalea wao ndani ya chama chao miaka yote, wamekuwa wakizifahamu, na wengine wameshaona namna zilivyotumika kuwaadhibu waliowatangulia, sasa kama walikubaliana nazo miaka yote hizo taratibu, iweje leo zikifuatwa dhidi yao ionekane wanaonewa?
 
You must possess the high level of IQ kuielewa siasa ya nchi hii,ugumu ni kwamba mabo nyeti ya kisiasa kama haya yana mkono wa Dark side deep state, hawa deep state wamegawanyika wapo mpaka upinzani na wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, sisi huku juu tunapangiwa ajenda za kujadili kutuchanganya,hivi inahitaji elim ya kiasi kujua kuwa suala hili lina mafungamano thabiti baina ya CDM na serikali?kweli jmn hamuoni?Pasco yupo mbele ya hili kifikra, anachokijua pasko cc wengine tutakuja kukiona after 2025.
Robots wa sampuli yako ndio Paskali anawapenda.
 
Huwa unakuja na thread zako kuonesha kama vile una jambo jipya, lakini kwa msomaji aliyekuzoea, na anayejitambua upstairs, ataona bado unazunguka pale pale.

Thread zako nyingi kuizungumzia Chadema na hao covid huwa uunakuja na allegations tu, unatoa shutuma lakini kwa makusudi huwataji kwa majina unaowalaumu, ili tu uwalinde wasaliti waliowahi kufukuzwa Chadema.

Nikwambie kitu, kama kweli unakiamini unachoandika kuhusu kuwatetea hao unaodai wameonewa, wataje kwa majina wale waliowaonea, na uoneshe kwa ushahidi kwa vipi walihusika kwenye huo uonevu, lakini kinyume na hapo, wacha kuchezea akili za watu bro.

Mfano, unaouzungumzia ule waraka wa 2014 uliowaondoa kina Zitto na wenzake, unadai "mashetani yako" yanakwambia aliyeuandika unamfahamu, ok, tutajie kwa jina huyo muhusika utuwekee na ushahidi wa namna alivyohusika kuandika ule waraka ili tuamini kweli kina Zitto walionewa.
Hata siku moja usiiruhusu njaa ikupande kichwani 😁 😁 😁 .
 
You must possess the high level of IQ kuielewa siasa ya nchi hii,ugumu ni kwamba mabo nyeti ya kisiasa kama haya yana mkono wa Dark side deep state, hawa deep state wamegawanyika wapo mpaka upinzani na wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, sisi huku juu tunapangiwa ajenda za kujadili kutuchanganya,hivi inahitaji elim ya kiasi kujua kuwa suala hili lina mafungamano thabiti baina ya CDM na serikali?kweli jmn hamuoni?Pasco yupo mbele ya hili kifikra, anachokijua pasko cc wengine tutakuja kukiona after 2025.
Ni Kweli akili hiyo hako nayo pekeake.

Tunachomtaka akae ktk nafasi yake ya uandishi.
K
ATIBA ya CDM inayo mapungufu kadha wa kadha.

Aache kuwa KADA kuepuka conflict of interest.

Tujadili Kwa mustakabali wa vizazi vijavyo.Amen
 
Ndugu Pascal nilishakwambia Ili uwe HURU Kujadili CDM lazima urudishe kadi ya CCM kwanza.

Kama Bado upo Chama kile Usitumie UBONGO wako kufikiria maana hauhitajiki. Kule ni kusifu na MAPAMBIO baasss😀😀😀😀
Mkuu Rabbon, kwa umri wangu nilionao sasa, nina haki ya kujiita mwalimu, hivyo nawafundisha tujifunze kusikiliza hoja ya mtoa hoja na sio kumjadili mtoa hoja.

Bandiko hili ni kuwasaidia wenzetu Chadema, huwa wanajikwaa na kuanguka na kuangalia walipoangukia tuu na sio walipo jikwaa, hivyo katika kuendelea na safari, kupitia njia ile Ile, wakapita pale pale walipojikwaa mwanzo, na sasa wamejikwaa tena pale pale na sasa wanapepesuka, bado hawajaanguka, hivyo nawasaidia wasianguke.

Walipomtimua Zitto Kabwe kwa maonevu, wao Chadema wenyewe hawana jicho la roho kuona nini kimewakuta, kiukweli wamekula bakora za karma za kutosha tuu.

Sasa wamemtimua Mdee, kwa mtindo ule ule, hapa nawasaidia kuepuka adhabu ya bakora za karma.
P
 
Mkuu Jidu La Mabambasi , asante sana kwa kujiheshimu, na mimi pia sio tuu nakuheshimu, bali nawaheshimu members wote jf na hata madogo humu wakinitukana, mimi nawamwagia thanks.

Mimi interest yangu ni moja tuu, watendewe haki, kama ni kuhumiwa, wahukumiwe kwa haki.

Kama Chadema wanajijua hawajapeleka majina, hii inamaanisha kuna forgery imefanyika, forgery ni kosa la jinai, kwanini Chadema hawakuripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike?. Kama Chadema wangeripoti polisi, Chadema wangekuwa served na nakala halisi ya barua yao ya uteuzi kutoka Chadema, Chadema ndio wangethibisha ni fake NEC wangebatilisha uteuzi wao. Kwanini Chadema iwatimue wanachama wake kienyeji enyeji bila kufanya a due process kuuthibisha forgery na katika kuwatimua, kwanini Chadema iwatimue wanachama wake bila kufuata Katiba sheria taratibu na kanuni zake yenyewe walizojiwekea?.

This is a challenge.

Hii ni changamoto kati ya morality and the business of politics. Ubunge ni politics and fursa at the same time.

Hapa ndipo kulihitajika a due process to establish the truth. Mimi niliisikia sauti, voices from within kuhusu hili na nikaliketa humu, Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?

Barua ya uteuzi wa wabunge hao 19 iliyotoka NEC kwenda kwa Spika it's authentic bonafide genuine letters.
P

Nimecheka kwa nguvu, eti kama kuna forgery CDM wangeripoti polisi, waripoti kwa polisi hawa wasiojua hata PGO inafanyaje kazi? Iripoti kwa polisi iliyotumika moja kwa moja kunajisi uchaguzi mkuu? Ni matukio mangapi ya kura za wizi yaliripotiwa kwenye vituo mbalimbali wakati wa uchaguzi wa 2020, na polisi hawakuchukua hatua zozote na ushahidi wa hayo upo.

Bro ni bora ukae kimya maana tumekupuuza kama tulivyolipuuza box la kura. Ni kweli CDM kama chama wanaweza kushiriki uchaguzi, lakini sioni sisi tunaijitambua kuwa na muda wa kushiriki huo uchaguzi. Kwa ujumla kwa sasa Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Tegemea idadi ndogo sana ya wapiga kwenye chaguzi zijazo.
 
Back
Top Bottom