Ushauri wa Bure: Ukijikwaa ukaanguka, usiangalie tu pale ulipoangukia, bali angalia pale ulipojikwaa

Ushauri wa Bure: Ukijikwaa ukaanguka, usiangalie tu pale ulipoangukia, bali angalia pale ulipojikwaa

Mbona Hujamtaja mhuni mwenzio ******** kwenye bandiko lako?eti alikua mtetezi wa wanyonge🤣🤣✌️✌️
 
Mkuu John7371, kwanza, nimefarijika sana kujua na wewe ni miongoni mwa watu wenye uwezo wa kufanya critical thinking and critical analysis. Watu wenye uwezo huo ni wachache hata humu jf, kwasababu, ili mtu awe na uwezo huo wa critical thinking na critical analysis ni lazima mtu huyo awe, bright and brilliant with good brain and intelligent mind.

Mimi nina bahati tuu kuzaliwa kwenye familia ambayo both parents, Baba na Mama ni watu wa 'Idara' hivyo nimezaliwa with security conscious hivyo kuonekana kama ofisa kipenyo na kwa vile wazazi ni huko, watu wanaamini mwana wa nyoka ni nyoka.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, kwetu tumezaliwa 8, we can't all be nyokas wengine ni mijusi.

Hizi the voices from within ni kweli kabisa nazisikia sauti na sio tips from deep state!. Karma nimeisoma nilipoishi New Delhi, India hivyo kuna vitu vinavyosabisha bad karma naviona vikifanywa, kazi yangu it's just to warn kuhusu karma, halafu bakora za karma zikishuka najua hizi ni bakora za karma. Mfano baada ya ushindi wa JPM, ile 2015, nilipandisha uzi huu, Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake! mtu wa deep state hawezi kupandisha bandiko kama hilo.

Na hata sasa watu wasio na jicho la roho wanaanza kumchagiza Samia kugombea 2025, mimi nimeunga mkono ya 2025 twende na Nagombea mwanamke, ila nikasema sio lazima awe Samia!, Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake! halafu nikasikia sauti hii Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, Sauti Imeshauri Mama Amkabidhi Kwanza Dr. Mwinyi, Urais wa JMT, Ndipo Aje Mwanamke!, mtu wa deep state, hawezi kuandika kitu kama hii!.
Hivyo rest assured mimi sii sehemu ya deep state, ila niko vizuri kwenye intels na hao deep state, kuna vitu tunaviweka humu, vinawasaidia kama hii kitu Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya? ... mwisho wa siku, jamaa walikula kichwa!, sasa ni mlango wazi! TOKA GEREZANI MPAKA BUNGENI-Nusrat hanje.only idiot won't recognize the key role played by dikteta uchwara
 
Wanabodi,
.
  1. Hili likifanyika, Chadema itakuwa imewatendea haki wanachama wake.
  2. Adhabu ya bakora za karma ninazoziona hazitakuja, hazita itandika Chadema, Chadema itakuwa salama na viongozi wake watakuwa salama.
  3. Chadema will prosper again, uchaguzi wa 2025 watashinda baadhi ya majimbo.
Mwenye macho na aone Mwenye masikio na asikie!.

Jumamosi Njema

Paskali.
Hivi hiyo "laana' au "karma" huwapata tu watu kwa kuwa tu fulani wewe Pascal Mayalla umsema, au..?

CHADEMA ni karma gani inayowatandika kwa mfano...?
Mkuu The Palm Beach, karma is the law of cause & effects kwa kuhukumiwa kwa matendo yako, ukitenda mema, unalipwa mema, na ukitenda uovu unaafhibiwa!.

The biggest toll ya karma ni kifo.

Kila binadamu kuna mazuri yake na mabaya yake, akitenda mema anabarikiwa, akitenda maovu analaaniwa. Kila kitu kinachomtokea binadamu hapa duniani ni matokeo ya matendo yake.

Kwa upande wa Chama, pia kuna karma za taasisi na karma za viongozi wa taasisi ambazo ndio watoa maamuzi. Taasisi inapotoa maamuzi ya dhulma, taasisi inaadhibiwa na watoa maamuzi nao wanaadhibiwa individually!, wakati wale wanao dhulumiwa karma ikiwafidia kwa kuwabariki.

Angalia baadhi ya viongozi wa Chedema waliofukuzwa bila kutendewa haki, baada ya kutimuliwa Chadema au kujitoa Chadema, angalia walikuja kuwa wapi?.

Angalia ma sterling wa matukio haya kilikuja kuwakuta nini?.

Angalia hali ya sasa ya Chadema kama Chama kikuu cha upinzani huku bara, amini nakuambia mwisho wa siku, Chadema itafanikiwa kuwatimua hawa makamanda mabinti 19 lakini machozi yao jasho na damu walioigharimikia Chadema, hayatapotea bure!, there is a price to pay and Chadema will pay dearly!.

Kwa vile Chadema inayo katiba yake na imeweka taratibu za haki kabisa kushughilikia nidhamu, zikiwemo mamlaka tofauti tofauti za nidhamu kwa viongozi tofauti tofauti, kwanini hazifuatwi?.

Mfano wakati wa kumtimua Zitto, Zitto alikuwa NKM, kwa mujibu wa katiba ya Chadema, mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu na mamlaka yake ya rufaa ni Mkutano Mkuu, mamlaka ya CC ya Chadema ni kumsimamisha tuu na sio kusikiliza shauri lake!, sasa hiyo CC ya Chadema ilimtumua Zitto kwa mamlaka gani?. Angalia Zitto baada ya kutimuliwa alikuwaje na angalia yule sterling wa kutimuliwa Zitto nini kilikuja kumkuta?.

Angalia Kitila Mkumbo baada ya kutimuliwa Chadema alikuja kuwa nani?.
Angalia Juliana Shonza baada ya kutumiwa Chadema alikuja kuwa nani

Hivyo kiukweli kabisa karma ipo and it acts upon us kwa matendo yetu!.

P.
 
Wanabodi,

Chadema ilijikwaa, ikaanguka, ikaangalia tuu pale ilipoangukia, ikainuka, ikaendelea na safari, bila kuangalia ilipojikwa, sasa imejikwaa tena pale pale, Ila bado haijaanguka, hivyo huu ni ushauri wa bure wa kuisaidia this time around, isianguke!.
A Way Forward
  1. Kitu muhimu cha kwanza kwa Chadema kufanya ni kutengua maamuzi yote kuwahusu hao wabunge 19 kuwa bado ni wanachama halali wa Chadema na kuwakubalia waendelee na ubunge wao.
  2. Baada ya kurejeshewa uanachama wao, wafute kesi iliyopo mahakamani
  3. Chadema kufanya a due process, uteuzi wao ulifanyikaje. Ikijiridhisha kuna jinai then waripoti rasmi polisi.
  4. Kule wathibitishe jinai ya forgery imefanywa na polisi kufanya uchunguzi wa kijinai na ikithibitishwa tuu jinai hiyo, then ni NEC ndio watakao watengua ubunge wao.
  5. Process ya mashitaka ya ndani ifanyike kwa mujibu wa katiba ya Chadema.
  6. Only ring leaders ndio waadhibiwe kwa kulazimishwa kuomba msamaha, na kuvuliwa vyeo vyote wabaki wanachama wa kawaida.
  7. Na wakosaji hao wakishupaza shingo zao then watimuliwe kwa haki na sio kwa kutumia a Kangaroo Court kama mwanzo.
  8. Hili likifanyika, Chadema itakuwa imewatendea haki wanachama wake.
  9. Adhabu ya bakora za karma ninazoziona hazitakuja, hazita itandika Chadema, Chadema itakuwa salama na viongozi wake watakuwa salama.
  10. Chadema will prosper again, uchaguzi wa 2025 watashinda baadhi ya majimbo.
Mwenye macho na aone Mwenye masikio na asikie!.

Jumamosi Njema

Paskali.
Hatimaye Chadema sasa wamefunguka macho, they are now doing the right thing na sasa ushauri huu wa bandiko hili ndio unakwenda kufanyika.
Update
Hatimaye Chadema wameacha kushupaza shingo na wamekubali matokeo!, kwa kuufuata ushauri wa bandiko hili CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Nimepokea taarifa, hii kutokea twitwani
Kisha nikasoma na bandiko hili humu JF Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Chadema wameufuata ushauri wa bandiko hili, waneacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo ya uchaguzi wa 2020!, sasa wameacha kushupaza shingo, wameyatambua matokeo kimya kimya!, wamewasamehe mashujaa hawa kimya kimya msamaha ambao utatangazwa rasmi siku ya Jumatano tarehe 8 Machi na Mwenyekiti wa Chadema, mbele ya Rais Samia!.

Iliwa kusemwa kuwa hakuna mkate mgumu wowote mbele ya chai!, tayari Chadema imeisha anza kupokea ruzuku hivyo sasa ita survive!. Na ile kesi ya kina Halima Mdee na wale 19 iliyopo mahakamani itafutwa!.

Hongera sana Chadema, for doing the right thing!, mtabarikiwa, viongozi wenu watabarikiwa, chama chenu kitabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa!.
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki CCM kwa kukubali reconciliation
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Nani asiyejua kuwa Covid 19 ni Magufuli Project na kibaraka wake mtiifu Ndugai.???EBU tuwe wakweli
 
Back
Top Bottom