Ushauri wa Gerald Hando kuhusu tiktok ni mwiba kwa uhuru

Ushauri wa Gerald Hando kuhusu tiktok ni mwiba kwa uhuru

Mimi mnieleweshe, ukijiunga huko tiktok content zinakuja zenyewe au hadi uzifollow/subscribe? Nashindwa kuliweka hili sawa sababu sina hiyo tiktok.

Maana mimi naona ukiacha JF mitandao mingine yote ina costumize content anazopendelea kuzifatilia mhusika.

Mfano, mimi ukiingia insta yangu feeds nyingi utakazoscrow zinahusisha urembo, mapishi, na decorations. Ukibonyeza explore utakuta contents zile zile, hata mtoto akishika simu akafungua insta atakutana na yale yale tu unless kama anajua kusearch pages/reels mpya. So as youtube, Quora nafollow pages za Academics na story za mahusiano pia travelling.
 
Elimu inapaswa kutolewa kuhusu mitandao ya kijamii maana mitandao mingi ni customized unachokipenda ndio unachokiona
 
Nilikiwa sijawahi ingia huo mtandao ..majuzi kuna video nilikuwa natafuta ikabidi nidownload huo mtandao wa tiktok ..duuh nilichokiona na kinaochoendelea kule ni hatari kwa ustawi wa kizazi cha vijana...
Mambo nayoona kwenye hizo live videos ndio balaa ..kwanza ni matusi muda wote kutukanana, mara mabinti kukaa nusu uchi na vijana kuanza kushawishi binti apandieshe nguo au avue waone chup*etc ..wapo wachache wanaoutumia vizuri kuonyesha biashara zao lakini wengi ni balaaaaaa.. ndio maana serikali ya Kenya pia etc zinashawishishi na wananchi kufunga huu mtandao ni hatari aisee..maana ni fully kijiwe cha ufuksa
 
kule tiko tok
vitu pekee unavyoweza kuviona muda wote:
1.Watu wana shindana kwa ukubwa, kuonyeshana, kutingisha matako.
2.Ushoga na usagaji ni elimu nyingine ya bure inayopatikana bila mipaka
3.Kama social media zingine, watu wako bize kujadili mambo ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia.


UNAJUA VIJANA WA LEO NDIO WAZEE WA KESHO.
 
TikTok na Twitter ni mitandao hatari sana kwa watoto na Rika zingine. Explicit contents zimeshamiri kupita maelezo. Leo hii serikali imefunga vituo vya porno kiasi Cha kwamba ili upate access inabd uwe na VPN. Ila kwa hio mitandao ni hatari sana. Nafuu Instagram wanajitahd sana kudhibiti hizo contents
 
Huyo jamaa pamoja na hiyo redio inayomtumikisha ndo wanapaswa kufungiwa
 
Asubuhi nilikuwa nasikiliza redio ambapo hawa ndugu zetu walikuwa wanajadili suala la dawa za kulevya ambapo waathirika na wanaotuhumiwa watapimwa. Katika kuelezea hilo mmoja wa watangazaji, Gerald Hando akasema jambo liende kwa wizara na TCRA.

Jambo lake ni kuwa Tiktok inaharibu vijana na watoto. Kwa hoja yake ni kuwa marekani inajaribu kuzuia tiktok sio tu kwa masuala ya taarifa binafsi lakini pia kulinda watoto.

Mimi napata shida na namna yoyote inayojiweka mbele kupinga teknolojia badala ya kutafuta namna bora za kutumia digital kukuza demokrasia.

Kama ambavyo baadhi ya mitandao imezuiwa nchini, naona kabisa tunaenda kuzuia mitandao mingi zaidi kwa sababu hizi zinazotolewa na wadau ambazo hazina mashiko.

Nawasilisha.
Sasa wmarekani ndio vinara wa ushoga Leo wanapinga tiktok ! Nadhani wameona Tu mchina kawapiga gap na mtandao huu Leo Una wafuasi wengi
 
Back
Top Bottom