Ushauri wa haraka: Kuku wameanza kufa kwa kasi

Ushauri wa haraka: Kuku wameanza kufa kwa kasi

Sio kideri hiki kweli? Mara nyingi kinaambukiza kwa mfugaji km alikanyaga kinyesi cha kuku mwenye ugonjwa labda huko nje, then akaenda kwa kuku wake anapofuga, ikipuliza hewa tyuuh imoo.

Kanunue madukani dawa ya kideri, nzuri ile ya matone kutia kwenye macho.

Ufugaji wa kuku unahitaji uangalizi na matunzo mnoo.
Nashkru sana kwa ushauri, lakini nashkru wanaendelea vzr na wanaoumwa bado hawajaongezeka
amekufa 1 mwingine aliyekuwa na hali mbaya baada ya kuwapa dawa ya mafua makali ameanza kulicover kwa sasa.
 
Wanyweshe gongo...
Kabla hujanidhihaki wala kunitukana,muulze mfugaji mwenzio kwanza...

Narudia tena...wanyweshe gongo
Haya mkuu nitajitahidi nichanganye na K vant nasikia ni nzuri kwa minyoo
 
sijaona mahali ukizungumzia kama uliwahi kuwapa chanjo tatu za muhimu
Mkuu uko sahihi kabisa mpaka sasa sijawahi kuwapa chanjo yoyote.
zaidi nimekuwa nikiwapa virutubisho tu na ANTIBIOTIC BASI.

LAKINI WIKI IJAYO NITAANZA KUWAPA CHANJO HATAKAMA NI KWA KUCHELEWA BASI SINA JINSI.
 
"DAWA GANI NZURI YA MAFUA MAKALI YA KUKU."
jaribu kuwapa flueban pamoja na otc usiwape dawa za biadamu kwani zinawaletea kuku usugu
fanya usafi wa banda ,cheki maranda unayoweka kwenye banda yasiwe ya mbao zenye harufu kali ,banda liwe na hewa ya kutosha,safisha vyombo vya maji kwa sabuni kila siku na wape kuku maji safi
tumia v-rid kupuliza kwenye hewa na ndani ya mabanda kila wiki na kama unataka kujilinda zaidi weka sahemu ya kukanyaga dawa kabla ya kufika bandani
NASHUKRU SANA KAKA KWA USHAURI MZURI.

USAFI NAJITAHIDI SANA NA NATUMIA MAPUMBA YA MPUNGA NA NAYABADILI KILA BAADA YA MUDA MFUPI.

Kuhusu dawa binadamu nitaziepuka maana wakidiwa nilikuwa nimeanza kuwapa za mafua pia za binadamu, na Tylodox
 
kuku ukiwapa chanjo zote sawasawa ndani ya mwezi moja na badae kurudia zile zinazopaswa kurudiwa kila miezi mitatu ,banda likiwa vizuri ukazingatia USAFI vifo utasikia kwa majirani
Nitajitahidi kuzingatia haya mkuu, shukrani sana
 
Ukiwa na mifugo ya aina yoyote inatakiwa uwe na moyo wa chuma maana wakifika 100 unataka wawe 200
Mimi nashukuru niliwala sana yaani kila wiki kuku mara moja au mbili na mayai mpaka 30 yanalika kwenye familia

Ila ukisema uwafanye ndugu basi utakuwa kama watusi au wasukuma unakuwa na ng'ombe 500 halafu kila leo unagombana na wakulima

Kuna mzee alinionyesha mifugo yake akasema unamuona huyo yuko sawa na mwanangu wa form 4
Anamuona kama mwanae pia [emoji1]
Uko sahihi now nina vifaranga 112 lakini natamani wangekuwa zaidi.

lakini ndani ya mwezi naona kuku baada ya kuwanyanganya vifaranga ndani ya 2weeks walianza kutaga na kwa sas baadhi naona wameanza dalili za kuatamia.
 
Sidhani kama ni kideri
Kwani wangeharisha kinyesi cheupe na kijani.
Alivyo eleza; inaonekana hayo ni mafua ya ndege....kuna mtu amemuelekeza dawa zake hapo juu
Yaa ni kweli dalili na jinsi wanavyopumua inaonesha ni mafua si kideri
 
Mbna niliona km alisema wana harisha? Bas sikusoma vizuri, kweli hayo mafua ya ndege
Hawaharishi ni shida ya kupumua ambayo ni wazi ni mafua kabisa tena makali, akizidiwa anapumulia mdomo tu na pua limeziba makamasi
 
Mkuu uko sahihi kabisa mpaka sasa sijawahi kuwapa chanjo yoyote.
zaidi nimekuwa nikiwapa virutubisho tu na ANTIBIOTIC BASI.

LAKINI WIKI IJAYO NITAANZA KUWAPA CHANJO HATAKAMA NI KWA KUCHELEWA BASI SINA JINSI.
wape usijepata hasara ya mwaka
 
Hapo kwenye andiko lako naona umetaja chakula na dawa tu ambazo unazopaga kuku wako ila chanjo sijaziona umetaja hivyo kama haukuzingatia utalatibu wa chanjo tatzo ndio linaanzia hapo husiangaike kumtafuta mchawi
 
Hapo kwenye andiko lako naona umetaja chakula na dawa tu ambazo unazopaga kuku wako ila chanjo sijaziona umetaja hivyo kama haukuzingatia utalatibu wa chanjo tatzo ndio linaanzia hapo husiangaike kumtafuta mchawi
Ni kweli mkuu sijawahi kuwapa chanjo.

Lakini nikiwapa kwa muda huu si sawa itafanya kazi tu mkuu
 
Chanjo muhimu sana
Kuna ile ya 3 in one
Na kuna ya mara tatu kwa awamu,
 
Dah, nilifikisha Kuku 120 na bata Bukini, Perkins, mallard, Khakhi campbell na Indian Runners 100. Hahaaaa, huu ufugaji huu. Ulitokea ugonjwa alipokuja dr akaniambia ni typhoid wakapukutika kuku wengi na nimebaki na kuku 30 tu na bata wakawa wanakufa mwisho nikawapunguza kwa kuwauza na sasa wamebaki 28 tu. Jamaa Aliniambia sikutaka kuchanganya kuku na bata kwa maana mabata ndio walileta typhoid kwa kuku.
 
Back
Top Bottom