Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nmeitumia na kuku wako poa tuu till now ...Tatu ni One niliona YOU TUBE baadhi wanaisifu wengine wanasema ni bomu hakuna kitu, je umewahi kuitumia?
Dawa nzuri ya kuku hasa wenye kideriWanyweshe gongo...
Kabla hujanidhihaki wala kunitukana,muulze mfugaji mwenzio kwanza...
Narudia tena...wanyweshe gongo
Kuna mjinga hajui,halafu anadai et napotoshaDawa nzuri ya kuku hasa wenye kideri
Kama hujui kaa kimya,kwanza unaonekana hata kuku hunaGongo tena!! acheni kabisa mizaha kwenye mifugo alafu akili ya kuambiwa changanya na zako sio kila unaweza kupokea kikawa kitu sahii kwako
kuku wa kienyeji hawakai ndani,hasa vifaranga ,usipoangalia vitakufa vyoteHabari wadau wa JF
Mwezi wa 2 mwanzoni nilianza kufuga kuku wa kienyeji pure.
Nikanunua Jogoo 2
Mitetea 14.
Mitete 2 walipata shida kidogo nikawala nikabakia nao 12.
Mwezi wa 3 mwanzoni wakaanza kutaga na kuanzia mwezi wa 3 baadhi wakaanza kuatamia, kuku wa mwisho katotoa leo trh 7/6/2023
Nina vifaranga makundi 4
1. miezi mitatu vifaranga 9.
2. Mwezi na nusu vifaranga 45
3. mwezi 1 vifaranga 35
4. Wiki 3 vifaranga 11
5. siku 1 vifanga 6.
Jumla nilikuwa na vifaranga wapatao 106 na waliongezeka leo kufanya jumla ya 112.
KATIKA VIFARANGA WOTE NILIKUWA SIJAWAHI KUPOTEZA KIFARANGA KWA SABABU YA UGONJWA AU KUUMWA.
Isipokuwa nilipoteza vifaranga 6 kwa kudonolewa na kuku wengine ambao siyo mama yao.
LEO ASBH NIMEAMKA NAONA KUKU 1 NI MNYONGE HALI MACHO HAYAONI VIZURI.
Baada ya kumchunguza vzr nikajuwa ana mafua makali sana na anapumua kwa shida.
Nilivyoanza kumpa matibabu kumfanyia dressing na kuondoa utando mweupe ndani ya jicho kwa kutumia maji ya vuguvugu na chumvi akazidiwa gafla na kuanza kukata roho.
Ni kifaranga wa mwezi na nusu.
KUKU WANGU WANAKAA NDANI MUDA WOTE LABDA MARA MOJA MOJA NAWATOA KUOTA JUA.
Kuku wakubwa wanashinda Nje kwenye Fensi na eneo la kutosha kama ekari 5.
CHAKULA CHAO HUWA NACHANGANYA
1. Mahindi yaliyobarazwa
2. pumba za mahindi.
3. Dagaa
4. Pumba za alizeti.
5. Maharage yaliyobarazwa mara chache.
Dawa ambazo,nimewahi kuwapa za vitaminic na madini ni
1. Neochikis
2. Premix layers
3. D.TC
4. Oxfarm
5. Alovera kila baada ya wiki mbili.
KUKU 12 WA KIENYEJI WALITAGA MAYAI ZAIDI YA 250.
DAWA GANI NZURI YA MAFUA MAKALI YA KUKU.
Nahofia na wengine vifaranga wataendelea kufa kwa kasi hii.
Hakikisha wamepona kwanza kwa kuwapa antibiotics kama vile OTC ,ndipo uwape chanjo bila hivyo watakufa zaidi.Ni kweli mkuu sijawahi kuwapa chanjo.
Lakini nikiwapa kwa muda huu si sawa itafanya kazi tu mkuu
Pilipili kichaa au jamii ya pilipili zote kamaDawa nzuri ya mafua kwa kuku ni kuwachanganyia PILIPILI kwenye maji yao ya kunywa. Ikiwa kuna mmoja kazidiwa sana mpake pilipili kwenye mdomo wake, hii dawa ni siku moja tu kesho yake wote wanapona. Hii ndo dawa nayotumia kwa kuku wangu