Ushauri wa haraka: Kuku wameanza kufa kwa kasi

Ushauri wa haraka: Kuku wameanza kufa kwa kasi

Umuhimu pia kuzingatia na chanjo za kuku,hata mm nilipoteza kuku kadha mwanzoni,lakini nikajitahidi kua zingatia chanjo kwenye dawa Mimi leva,amprolin-300,limoxin WS,na ultraxide(hi ni ya utitiri,)sema Mimi nachanganya kwenye maji zikiwa zote
shukran sana
 
Nashukru sana kaka kwa ushauri wako.

Kuna muda unahisi kuku wamekuwa ndugu zako so ukipoteza hata 1 unafeel maumivu na unabakia kuwaza hatma ya wengine waliobakia.
Hakika mkuu maumivu yakupoteza kuku huwa inauma sana sema ndio hvyo

tunapenda ufugaji inabidi tupambane na changamoto hzo hazikwepeki
 
Dawa nzuri ya mafua kwa kuku ni kuwachanganyia PILIPILI kwenye maji yao ya kunywa. Ikiwa kuna mmoja kazidiwa sana mpake pilipili kwenye mdomo wake, hii dawa ni siku moja tu kesho yake wote wanapona. Hii ndo dawa nayotumia kwa kuku wangu
Pia tuzingatie sana na madawa ya kienyeji yaliyotuzunguka majumbani
Mfano:Mwarobain unatwangatwanga unaloweka kwenye maji huu ni dawa nzuri kuzuia kuku kuharisha
Alovera ,mlonge hizi z inasaidia sana kuzuia kideri,mafua,
Dawa za kienyeji ni nzuri tuzingatie pia
 
Wanyweshe gongo...
Kabla hujanidhihaki wala kunitukana,muulze mfugaji mwenzio kwanza...

Narudia tena...wanyweshe gongo
Ndugu nami ni mfugaji. Nauliza kwa kila lita ya maji inahitajika kiasi gani cha gongo na je gongo ile namba moja au uliyopozwa makari
 
Dawa nzuri ya mafua kwa kuku ni kuwachanganyia PILIPILI kwenye maji yao ya kunywa. Ikiwa kuna mmoja kazidiwa sana mpake pilipili kwenye mdomo wake, hii dawa ni siku moja tu kesho yake wote wanapona. Hii ndo dawa nayotumia kwa kuku wangu
Kuku anaekoloma ni ugonjwa gani
 
Usiweke utani kwenye mambo ya maendeleo.
Watu tumetumia gongo miaka nenda rudi kutibu kuku we unasema utani?! Anyway, endeleeni na hayo madawa yenu ya wazungu muone kama mtatoboa. Miafrika sijui tupoje!😠
 
Naomba kujua chanjo gani ya kwanza wanatakiwa kupatiwa kuku wa kienyeji mara tu wanapofika bandani?
 
Back
Top Bottom