Ushauri wakuu.anasema hana feeling na mimi

Ushauri wakuu.anasema hana feeling na mimi

NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
333
Reaction score
90
Wakuu niko chuo kikuu ninasoma na dada fulani ambaye nimekuwa nikimpenda sana!wiki iliyopita nikamwambia nina mazungumzo na yeye akaniambia yuko bizze kidogo na akawa ameniambia tukutane ijumaa jioni tuongee.nikawa nimekubali lakini baadae nikakumbuka kuwa nilikuwa nisafiri Alhamis kwenda mkoa jirani ila ningerejea baada ya pasaka nikampigia nikamweleza akaniambia tuonane nikisharudi.baada ya kuwa nimerudi nikawasilia nae akaniambia tukutane jana saa kumi mna moja jioni mda ulipofika nikampigia hakupokea nikamtafuta saa mbili hivi akapokea akasema alikuwa amebanwa kidogo ila akaniambia tuonane jioni hiyo ilikuwa kama saa tatu hivi na kimvua kilikuwa kinanyesha tukaenda mahalifulani nikamueleza lakini akaniambia she is not feel me.nikajaribu kuongea nae lakini jibu likawa hivyo leo usiku huo nikampigia tukaongea na leo asubuhi pia nimempigia tumeongea lakini jibu ni hilo bado ila nikimpigia anarespond flesh tu nifanyeje wadau?
 
Sasa wewe ulitaka AKUTUKANE???? Achana naye haku feel au unataka umnunue? Buy her and you will see at the end.
 
tumia nguvu ya hela sasa dogo . mkono mtupu haulambwi. akiruka na hiyo tumia nguvu za kijeshi.
 
Bora uachane nae, and raise your gpa and work hard to succeed, hajakukomoa kukwambia hivyo as hata yeye ambaye ana feelings kwake nae hampendi na huyo nae ni hivyo hivyo as mzunguko wa love feelings unaendelea, unapopendwa wewe hupapendi na usipopendwa na wewe unapapenda, its tough to date a college girl kama na wewe hupo college as financial freedom wewe huna and woman needs to be protected socially and financially from their man
 
Amesha toa jibu, give the sister some space please.

niliwahi ambiwa NAOMBA TUWE KAMA KAKA NA DADA, nikamwambia poa. Tukaendelea na mawasiliano ya kawaida na outing za hapa na pale. Siku moja alinikuta na msichana mwingine kwenye pozi ambalo siyo, jioni yake akaja rum analalamika na tukamalizana siku hiyo. Kuanzia hapo nikaendelea kufaidi taratibu. Kijana anatakiwe aende taratibu,asiwe na pupa. Kama unataka kuonja tu,we kula kona kwani wako wengi
 
bora amekuwa muwazi kwako.vile vile mpe muda,maybe baadae atakupenda huyo.
 
Kwa nnavowajua wadada hata hnamaana hiyo!! maana yake ongeza bidii zaid kwny kuomba,upo hapo?
 
Namba unayopiga haipatikani tafadhari jaribu baadae.
 
We mmwagie mapesa,ikishndikana tumia mbinu za kijeshi kama alvoshauri mdau mmoja hapo juu.
 
Kuna uwezekana wa mambo mawili hapo; la kwanza huyo Dada ana busara na tayari ana mtu wake hivyo hataki kuwachanganya au kukupotezea muda, kama ni hivyo, ana busara na ni mke mzuri mtarajiwa, maana mwingine angekukubalia ili afaidi Boom lako. Jambo la pili, anaweza kuwa anataka kukusoma kama kweli una nia ya dhati. Kwa hili la pili utahitajika kuwa mvumilivu na kuendelea kubisha hodi kwa muda mrefu ili kujiridhisha bila mashaka kwamba ni kweli hutakiwi. Lakini angalia usiwe kero kwake, huku kwa nchi za wenzetu kama mtu hakutaki akaendelea kumlazimisha ni kosa kisheria; na vile vile ukumbuke kilichokupeleka chuo....Elimu Kwanza.
 
Wakuu niko chuo kikuu ninasoma na dada fulani ambaye nimekuwa nikimpenda sana!wiki iliyopita nikamwambia nina mazungumzo na yeye akaniambia yuko bizze kidogo na akawa ameniambia tukutane ijumaa jioni tuongee.nikawa nimekubali lakini baadae nikakumbuka kuwa nilikuwa nisafiri Alhamis kwenda mkoa jirani ila ningerejea baada ya pasaka nikampigia nikamweleza akaniambia tuonane nikisharudi.baada ya kuwa nimerudi nikawasilia nae akaniambia tukutane jana saa kumi mna moja jioni mda ulipofika nikampigia hakupokea nikamtafuta saa mbili hivi akapokea akasema alikuwa amebanwa kidogo ila akaniambia tuonane jioni hiyo ilikuwa kama saa tatu hivi na kimvua kilikuwa kinanyesha tukaenda mahalifulani nikamueleza lakini akaniambia she is not feel me.nikajaribu kuongea nae lakini jibu likawa hivyo leo usiku huo nikampigia tukaongea na leo asubuhi pia nimempigia tumeongea lakini jibu ni hilo bado ila nikimpigia anarespond flesh tu nifanyeje wadau?

tukushauri nn tena na wakati mtu keshakuambia aku fill,achana nae tafuta ingine.
 
Ukiendelea utakua kero. Umesha mpa ujumbe we piga kimya tu sasa. Akibadili mawazo atakutafuta yeye.
 
mazee, nimeambiwaga hivyo..nikasepa..ila mawasiliano nao bado yapo..text simu kama kawaida..wengine wana watoto wao..wameolewa ..bado wanawasiliana na mimi..hapo ndo nakopata kigugumizi kuhusu mabinti..undefined..
 
Back
Top Bottom