NALO LITAPITA
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 333
- 90
Wakuu niko chuo kikuu ninasoma na dada fulani ambaye nimekuwa nikimpenda sana!wiki iliyopita nikamwambia nina mazungumzo na yeye akaniambia yuko bizze kidogo na akawa ameniambia tukutane ijumaa jioni tuongee.nikawa nimekubali lakini baadae nikakumbuka kuwa nilikuwa nisafiri Alhamis kwenda mkoa jirani ila ningerejea baada ya pasaka nikampigia nikamweleza akaniambia tuonane nikisharudi.baada ya kuwa nimerudi nikawasilia nae akaniambia tukutane jana saa kumi mna moja jioni mda ulipofika nikampigia hakupokea nikamtafuta saa mbili hivi akapokea akasema alikuwa amebanwa kidogo ila akaniambia tuonane jioni hiyo ilikuwa kama saa tatu hivi na kimvua kilikuwa kinanyesha tukaenda mahalifulani nikamueleza lakini akaniambia she is not feel me.nikajaribu kuongea nae lakini jibu likawa hivyo leo usiku huo nikampigia tukaongea na leo asubuhi pia nimempigia tumeongea lakini jibu ni hilo bado ila nikimpigia anarespond flesh tu nifanyeje wadau?