Ushauri wangu kuhusu wachezaji John Bocco, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni

Ushauri wangu kuhusu wachezaji John Bocco, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Ushauri Wangu Kuhusu Wachezaji John Bocco, Shomari Kapombe Na Erasto Nyoni

Wadau wa JF

Huu ndiyo ukweli hata kama unaumiza

Huu ndiyo ukweli wenye maslahi mapana kwa nchi yetu

Wachezaji John Bocco na Shomari Kapombe na Erasto Nyoni uwezo wao uwanjani umepungua pakubwa sana kutokana na umri na sababu nyinginezo

Ni busara wachezaji hawa wakapumzishwa rasmi kuichezea Timu yetu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars)

Ni wakati muafaka wa kuanza kutumia damu changa zilizojaa vipaji lukuki

KaziIendelee
 
Shomar kapombe n mdogo lakin Hana jipya tena hawez ongeza chochote ndo mwisho wa uwezo wake sijui Hawa makocha wetu yan n aibu Boko, nyon na mzamiru kuchezea timu ya taifa hasa Boko umri umemuacha Sana
 
Kwani hawa wachezaji hua wanatoa rushwa kwa kocha ili awapange kikosi cha Kwanza?

Wanachoonyesha kwenye uwanja wa mazoezi ndicho hicho kinafanya kupangwa kwenye mchezo, hizo damu change unazosema zenye vipaji lukuki ni kwanini hazichezi?

Ni kwamba hawapendwi na kocha ama?

Tuache ujuaji muacheni kocha afanye kazi yake kama hao wachezaji hawafai basi hao damu changa waonyeshe viwango waitwe timu ya taifa na sio kuitwa tu bali wakapiganie namba wawaweke benchi hao wazee kama wanaweza.
 
Shomar kapombe n mdogo lakin Hana jipya tena hawez ongeza chochote ndo mwisho wa uwezo wake sijui Hawa makocha wetu yan n aibu Boko, nyon na mzamiru kuchezea timu ya taifa hasa Boko umri umemuacha Sana
Hivi utakwenda kucheza na mijibaba kama Dr Congo, Togo, Mali n.k kisha ukatumia beki kama kibwana Shomari au kibabage pekee? Hata kama wana vipaji vikubwa ila maumbo yatawahukumu.
 
Uliangalia mechi ya stars na Dr Congo kule kwao na hapa nyumbani?
Ukweli sijaangalia ila naamini kama unaweza haijalishi umbo lako japo uwe unajiweza maana hata history wachezaji waliotokea kuwa wazuri na wafupi na wadogo kama Maradona, Messi mpaka kina Xavi vidogo tu Iniesta ila wanajuwa.
 
Back
Top Bottom