Mimi nakubaliana na wewe kuwa na centre back wenye miili mikubwa inasaidia au ku mix vimo inakuwa ngumu kuwa beki zote wafupi mtapata tabu mipira mirefu, sasa hapo ndio kocha anatakiwa kuonesha utalaamu wake kwa kujuwa mimi nacheza na watu warefu nitumie wachezaji gani waweze kukabiliana na hatari au sina chaguo ni hawa tu nifanye mbinu gani kupunguza makali ya vimo vyao, Kitu kimoja najuwa kuwa beki wa kati kuwa na kimo ni advantage kubwa na duniani kote mabeki wa kati warefu na ukiona beko mfupi basi juwa huyo ni special talent ila beki za pembeni ufupi sio shida sana. Sasa hapa inakuja suala la kuwakuza vijana physical kwa mazoezi na vyakula. Toka wakiwa wadogo unamwambia kabisa wewe beki na mwili wako huu hutafika mbali hamia kiungo au wewe mrefu rudi nyuma. VVD alikuwa forward akaambiwa nyuma kuna kufaa, Paul scholes alikuwa striker akaambiwa wewe mzuri lakini mbele sio sehemu yako rudi kati akaja kuwa bonge la kiungo. Huyu mtoto wa Liver Jones alikuwa winger kabadilishwa kiungo yuko juu. ni kuwa na makocha wazuri wa academy kuweka mambo sawa kabla too late.