Ushauri wangu kuhusu wachezaji John Bocco, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni

Ushauri wangu kuhusu wachezaji John Bocco, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni

Kwani hawa wachezaji hua wanatoa rushwa kwa kocha ili awapange kikosi cha Kwanza?

Wanachoonyesha kwenye uwanja wa mazoezi ndicho hicho kinafanya kupangwa kwenye mchezo, hizo damu change unazosema zenye vipaji lukuki ni kwanini hazichezi?
Ni kwamba hawapendwi na kocha ama ?

Tuache ujuaji muacheni kocha afanye kazi yake kama hao wachezaji hawafai basi hao damu changa waonyeshe viwango waitwe timu ya taifa na sio kuitwa tu bali wakapiganie namba wawaweke benchi hao wazee kama wanaweza.
Kama nimekuelewa ni kwamba tuna makocha wababaishaji wasiojielewa
 
Ukweli sijaangalia ila naamini kama unaweza haijalishi umbo lako japo uwe unajiweza maana hata history wachezaji waliotokea kuwa wazuri na wafupi na wadogo kama Maradona, Messi mpaka kina Xavi vidogo tu Iniesta ila wanajuwa.
Ungeangalia hizo mechi ungenielewa kipi namaanisha ungeona jinsi hawa wachezaji wetu waliovyokuwa wana bembea kwenye migongo ya watu ungenielewa mtu anapiga kichwa mbele ya Job japo kajitahidi kuruka kwa uwezo wake wote ila kimo kimemhukumu.

Unaweza kuwa mfupi na ukawa mchezaji hatari sana ila inategemea nafasi gani unacheza, usibeze hata kidogo umbo lina maana kubwa sana kwenye mpira.
 
Mimi nakubaliana na wewe kuwa na centre back wenye miili mikubwa inasaidia au ku mix vimo inakuwa ngumu kuwa beki zote wafupi mtapata tabu mipira mirefu, sasa hapo ndio kocha anatakiwa kuonesha utalaamu wake kwa kujuwa mimi nacheza na watu warefu nitumie wachezaji gani waweze kukabiliana na hatari au sina chaguo ni hawa tu nifanye mbinu gani kupunguza makali ya vimo vyao, Kitu kimoja najuwa kuwa beki wa kati kuwa na kimo ni advantage kubwa na duniani kote mabeki wa kati warefu na ukiona beko mfupi basi juwa huyo ni special talent ila beki za pembeni ufupi sio shida sana. Sasa hapa inakuja suala la kuwakuza vijana physical kwa mazoezi na vyakula. Toka wakiwa wadogo unamwambia kabisa wewe beki na mwili wako huu hutafika mbali hamia kiungo au wewe mrefu rudi nyuma. VVD alikuwa forward akaambiwa nyuma kuna kufaa, Paul scholes alikuwa striker akaambiwa wewe mzuri lakini mbele sio sehemu yako rudi kati akaja kuwa bonge la kiungo. Huyu mtoto wa Liver Jones alikuwa winger kabadilishwa kiungo yuko juu. ni kuwa na makocha wazuri wa academy kuweka mambo sawa kabla too late.
 
Shomar kapombe n mdogo lakin Hana jipya tena hawez ongeza chochote ndo mwisho wa uwezo wake sijui Hawa makocha wetu yan n aibu Boko, nyon na mzamiru kuchezea timu ya taifa hasa Boko umri umemuacha Sana
Ishu ni kiwango kushuka siyo umri
Mbokani wa DRC amefunga goli karibu kila mechi za kufuzu amesaidia sana timu na ana umri sawa na kina Nyoni, Boko
 
Kwani hawa wachezaji hua wanatoa rushwa kwa kocha ili awapange kikosi cha Kwanza?

Wanachoonyesha kwenye uwanja wa mazoezi ndicho hicho kinafanya kupangwa kwenye mchezo, hizo damu change unazosema zenye vipaji lukuki ni kwanini hazichezi?

Ni kwamba hawapendwi na kocha ama?

Tuache ujuaji muacheni kocha afanye kazi yake kama hao wachezaji hawafai basi hao damu changa waonyeshe viwango waitwe timu ya taifa na sio kuitwa tu bali wakapiganie namba wawaweke benchi hao wazee kama wanaweza.

Kocha ndiye hajui ndiyo maana twafungwa

Hao damu changa Wana uwezo mkubwa ila hawachaguliwi timu ya Taifa
 
Ukweli sijaangalia ila naamini kama unaweza haijalishi umbo lako japo uwe unajiweza maana hata history wachezaji waliotokea kuwa wazuri na wafupi na wadogo kama Maradona, Messi mpaka kina Xavi vidogo tu Iniesta ila wanajuwa.
Ongeza Lorenzo Insigne, Marco Verrati, Ngoro Kante, Roberto Carlos, Zolla, Msuva, Ngassa, Marco Senna, Matthew Valbuena and too many to mation

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Ushauri Wangu Kuhusu Wachezaji John Bocco, Shomari Kapombe Na Erasto Nyoni

Wadau wa JF

Huu ndiyo ukweli hata kama unaumiza

Huu ndiyo ukweli wenye maslahi mapana kwa nchi letu

Wachezaji John Bocco na Shomari Kapombe na Erasto Nyoni uwezo wao uwanjani umepungua pakubwa sana kutokana na umri na sababu nyinginezo

Ni busara wachezaji hawa wakapumzishwa rasmi kuichezea Timu yetu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars)

Ni wakati muafaka wa kuanza kutumia damu changa zilizojaa vipaji lukuki

KaziIendelee
Naomba ni kujibu kiufundi
Kapombe namba yake bado hana mshindani na hajaisha Sana ila anahitajika kupumzika kidogo maana miaka hii mitatu katumika Sana
Bocco yeye ndio standing striker pekee nchi hii ila kinachomhukumu saivi ni injary nyingi , Bocco huyu akipumzika akarecovery vizuri atarudi moto Kama msimu uliopita

Erasto mnamlaumu bure timu ya taifa sijaona kosa lake
 
Ndio wakina nani hao?

Naombeni picha za watu hao niwajue na wanacheza timu ipi?
 
Hebu peleka huo Uyanga wako kwenu!
Eti wengine wameenda mbali hata kusema ongeza na Manula, hivi kuna golikipa maikini kama Manula Tanzania hii??? bila Manula ile mechi ya wacongo Dar tulikuwa tumepigwa 7 ! ni vizuri mashabki wa Yabga mkaacha chuki binafsi za kishabki na kushambulia watu binafs badala ya kushauri techinical terms!
Inafahamika muda wanaokaa kambin wachezaji wetu kiufupi hautoshi kujenga muunganiko mzuri hivyo sio jamba la kushangaza kama mchezaji atabakia akirukruka uwanjani ! Kitu kikubwa tunachokitegemea siku zote ni uwezo binafs wa wachezaji ambao kama akikutana na mazingira ya kukamiwa au kubanwa , ndo hali inakuwa hivi kama iliyomkuta staa wetu Samatta!
Hivyo ni vema kufocus mabo mtambuka yaliyotukwamisha badala ya kushambulia wachezaji! Huwezi kumuamulia mtu eti astafu kazi yake wakati hata club yake tu bado inamuhitaji!
 
Uliowataja wanafanana maumbo na kina kibabage? Au umeamua ubishe tu
Wewe unamjuwa kuna mtu alikuwa anaitwa Omar Hussen? au ulishawahi kumuona Juma Burhani labda hawa wa nchini utawajuwa wale kwenye TV unawaona wakubwa. Kwa hiyo huyo Kibabage ni mdogo kuliko Shakir. Hii sio basketball hao niliowataja kina Jordi Alba ni wachezaji wadogo sana kimaumbo. Kulikuwa vile vicheza vifupi Xavi na iniesta giant mwenyewe Yaya toure ikabidi akae bench ahame na team. ukiwa unajuwa mpira unajuwa tu Maradona alitesa dunia na ufupi wake.
 
Hizo nchi zenye wachezaji wenye maumbo makubwa kama congo na Cameroon walishawahi kuchukua kombe la dunia?

Bukayo Saka mchezaji mdogo kiumri na kiumbo ila angalia shughuli yake uwanjani na kunawakati Arsenal tulikuwa na shida ya left back ila huyu bwana mdogo pamoja na umbo lake dg alikuwa anacheza nafasi hiyo ya beki wa kushoto
 
Bukayo anamwili mdogo?
afu ni left au rightback
 
Back
Top Bottom