Ushauri wangu kwa Mama Samia kuhusu matumizi ya fedha za DP World!

Ushauri wangu kwa Mama Samia kuhusu matumizi ya fedha za DP World!

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Utangulizi:
Kwakuwa Mwenyezi Mungu ameamua kutujaalia Watanzania kwa kutuletea hii neema ya uwekezaji ya DP World; neema ambayo imekuja kipindi ambacho nawe alishaamua kukujaalia neema ya uongozi.........endelea kushirikiana na viongozi wenzako kutuhimiza kuishikilia neema hii.

Kwakuwa Mwenyezi Mungu amejaalia mamilioni ya Watanzania, I mean Watanzania kama Watanzania huku mtaani, wameelewa na wapo pamoja nawe kabisa kabisa tena kwa 100%......pigeni kazi mama!

Kwakuwa kamanda Kwile aliwahi kusema, "Solve the problem or leave the problem. But do not live with the problem." Sisi Watanzania tumekuelewa sana Jemedari wetu wewe. Kuliko kuya'leave' matatizo lukuki na makubwa pale bandarini ya wizi, uvivu, uhujumu uchumi, urasimu n.k. yaendelee kutusibu kimwili na kisaikolojia; umeuvaa ujasiri wa kuyatatua maana bila shaka, kwa jinsi ulivyojawa na upendo, umeona kabisa kama hujasolve hilo tatizo hapo bandarini hadi muda wako unaisha you will never be able to live your life again..........mama Watanzania tunasema songeni mbeleee!!

Kwakuwa anayeitwa 'askofu' Mwamakula, kwa kukusudia au kutokukusudia, amewaonyesha Watanzania wote wenye akili na nia njema na nchi hii ni vipi hawana hoja hao wapingaji, sisi Watanzania wenye akili na uchungu kuliko huyo Mwamakula, tunasema ikiwezekana kazi na DP World ianze hata saa 10 alasiri ya leo.

Kwakuwa familia za lissu na mbowe, sina uhakika sana na ya Dr slaa ingawa nae sina imani nae, ziko Marekani na zina uraia wa huko; Watanzania tunasema wakikukaribia watandike vibao, la tufanye sisi wenyewe! Shwayn!!!

Kwenye mada:
Mama, Mtanzania mimi nakushauri yafuatayo kuhusu mapato makubwa ya DP World yatakayopatikana. Na hiki nakusihi kiwe kitu cha kwanza kufanya mara baada ya muamala wa kwanza kusoma;

Jenga njia mbili mbili katika barabara zote kuu ili kupunguza ajali zinazoshamiri kila leo kutokana na magari kugongana. Utaokoa maisha ya Watanzania wengi sana yakiwemo na ya kina lissu, mbowe, mwamakula na slaa. Kuwawezesha kuongeza speed ili kufika kwa haraka maeneo mbalimbali kukutukana na kuendelea kukuzushia, hilo litakuwa juu yao kuamua.....naamini halitokusumbua kama ambavyo halikusumbui sasa hivi wanapofanya kwa speed ya sgr.
 
Nauliza hiviii, ndiyo tunataka maendeleo kwa muandiko huu?

Hawa ndio raia wenyewe au kuna wengine?
 
Nauliza hiviii, ndiyo tunataka maendeleo kwa muandiko huu?

Hawa ndio raia wenyewe au kuna wengine?
Mwandiko ndo huohuo na raia wenyewe ndo haohao mkuu na maendeleo tunayahitaji kuliko kawaida.......na tutayapata!

Halafu sijasema kuwa DP World ni Mungu mkuu😄😄😄
 
Mnataka vya bure bila kushughulisha akili, kubuni na kufanya kazi. Mnafikiri waarabu ni wajinga sana katika dunia hii mpaka wasahau kwao waje wakupe pesa za bure bure.

Maumivu yanakuja muda si mrefu. Ndipo mtajua kuwa pesa hazidondoki kama mvua badi hutafutwa kwa jasho na damu.
 
Mnataka vya bure bila kushughulisha akili, kubuni na kufanya kazi. Mnafikiri waarabu ni wajinga sana katika dunia hii mpaka wasahau kwao waje wakupe pesa za bure bure.

Maumivu yanakuja muda si mrefu. Ndipo mtajua kuwa pesa hazidondoki kama mvua badi hutafutwa kwa jasho na damu.
Hilo kina Mama Samia walilijua kabla hujazaliwa. We komaa na marobota yako ya pamba huko, ukibeba mwenyewe gunia moja hadi jingine kupeleka gulioni ukiamini wakibeba wengine watakuibia.
 
Yeah, nimesoma yale makubaliono yanayofananishwa na mkataba!
Mkataba ni nini?

Kinachopelekwa bungeni kuwa ratified ni makubaliano au mkataba?

Umesoma full instruments of powers za Tanzania?
 
Back
Top Bottom