Ushauri wangu kwa Upinzani Tanzania: Epukeni kujibizana hadharani, wapuuzeni wapambe

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Mada inahusika.

Katika kipindi hiki kwenu kilichojaa fitina na majungu na nia ya dhati ya kutaka kusambaratishwa na watawala, umakini unahitajika sana.

Kwanza ukomavu wenu ni muhimu na mapitio yenu yawaunganishe kama kundi moja lenye common intrest

Tumieni uzoefu mlioupata kwenye UKAWA 2015 kutatua changamoto zenu, ikiwezekana undeni kamati ya ushauri ya utatuzi wa changamoto zenu. Tambueni ADUI yenu mkuu ni CCM.

Epukeni kujibizana hadharani ili kutowapa faida maadui zenu wakubwa katika kipindi hiki hasa CCM, baadhi ya wakurugenzi, baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa na POLISI.

Acheni kuwasikiliza wapambe nuksi. Hawa ni wachonganishi sikilizeni hoja na kutatua changamoto zenu kwa busara.

Fikirieni umoja wenu na namna ya kukabiliana na CCM. Puuzeni baadhi ya mambo yasiyo ya lazima kuyajibu au kutoa ufafanuzi na muwe na mwelekeo unaoeleweka (BE FOCUSED)

Ni hayo tu.

Kishada.
 
Ushauri mzuri ,vijana wa chadema wakiijua nidhamu hutaona haya yakitokea,na huko ndiko kwenye tatizo
 
Wewe nawe, ungekuwa unaijua nidhamu badala ya kushabikia ungeanza kwa kuwaokoa vijana wa lumumba. Wanapokubali kutumika na kutumikishwa wanaanzisha moto ambao muelekeo wake polisi na nyie hamtaweza kuuzima.
 
Mashabiki wengi wa chadema ni vichwa maji na viongozi wao hawana vision Wala misimamo
 
Ushauri mzuri, itawaepusha na mengi hasa kipindi hiki tunapokaribia uchaguzi mkuu
 
Mashabiki wengi wa chadema ni vichwa maji na viongozi wao hawana vision Wala misimamo
Mkuu jitahidi usichochee kuni kwenye moto wa nyumba ya Jirani. Kwa umoja wetu wote watu wa vyama tofauti. Tujifunze yatokanayo na huu ushauri. Ruksa kujadili na sio kukashifu.
 
Bora ukawapa ushauri familia yako kuliko kupoteza muda wako kuwashauri manyumbu.
 
Uhitaji rocket science kufahamu kuwa iwe kwa namna yoyote ile, CCM & DOLA zinaenda kutimiza lengo la ama kuifuta CHADEMA kwenye uso wa siasa za Upinzani au kuidhoofisha kabisa ibaki chama cha kawaida sana. Kwa hiyo CHADEMA hata ikichukua ushauri huu au isichukue bado kikombe cha CCM itakinywa tu.
Sasa hivi ni siasa za JINO kwa JINO, yani don't bow or kneel down maana CCM wanaendesha siasa za UBABE kwa msaada wa DOLA, hakuna reconciliation itayoiokoa CHADEMA.

Matendo ya CCM na DOLA yapo wazi, usishangae kuona Bunge lijalo kambi ya Upinzani ikiundwa na NCCR ya Mbatia. Huu ni mkakati.

Pichani ni Dr. Bashiru Ally
FB_IMG_1583487042212.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunafahamu usaliti unaoendelea. Ni vyema kutumia weledi wote kushughulika na hujuma kwa ustadi mkubwa.

Tunafahamu uwoga wa CCM dhidi ya Umoja wa Upinzani imara Bara na Zanzibar. Tunafhamu uwoga wa Mkuu na Mwenyekiti wa Chama Tawala wa kuaogopa kuangukiwa na jumba bovu kichama.

Tunafahamu baadhi ya wapinzani kutaka kutumiwa kuhujumu Upinzani wa kweli.

Tunafahamu njama za kutaka kutumia hadaa ya UZALENDO khujumu matunda ya umoja kwenye upinzani.

Hayo yote yashughulikiwe kwa umakini mkuibwa na vyama vya upinzani makini. Atakaye kwenda kinyume ashughulikiwe ipassavyo kwa uzito wa hoja na kwa wakati muafaka na sio propaganda.

Nikwambieni zidisheni umakini tu. Kuna watu wataadhirika si mda mrefu lakini shuruti kuwe na umakini na hatua muafaka.
 
Huo umakini na busara ni zero kabisa huko upinzani. Wanaropoka sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elewa mleta uzi ,anasisitza umoja ndani ya upinzani ,muache kuchambana hadharani ,ccm inaingiaje hapa wakati ndio mnadai adui yenu?,pathetic
Wewe nawe, ungekuwa unaijua nidhamu badala ya kushabikia ungeanza kwa kuwaokoa vijana wa lumumba. Wanapokubali kutumika na kutumikishwa wanaanzisha moto ambao muelekeo wake polisi na nyie hamtaweza kuuzima.
 
Mkuu jitahidi usichochee kuni kwenye moto wa nyumba ya Jirani. Kwa umoja wetu wote watu wa vyama tofauti. Tujifunze yatokanayo na huu ushauri. Ruksa kujadili na sio kukashifu.

Mkuu huu ushauri wako nauunga mkono, nimewashauri cdm kama chama wasijibu lolote hasa kwa huyo Mbatia au mwingine yoyote wa mwelekeo huo. Maana lengo hasa ni kuwatoa cdm kwenye taswira safi, wao wajikite kudai tume huru ya uchaguzi, wataishia kuona kauli kama za leo za kina Bashiru. Hao wapinzani design ya kina Mbatia waachwe watapewa moto wao huku mitandaoni. Uzuri ni kuwa wapinzani hasa Cdm hawajamjibu chochote Mbatia au mwingine mwenye uelekeo huo, maana chama kinachotafutwa hapo ni cdm zaidi.
 
Elewa mleta uzi ,anasisitza umoja ndani ya upinzani ,muache kuchambana hadharani ,ccm inaingiaje hapa wakati ndio mnadai adui yenu?,pathetic

Tutajie chama cha upinzani cha kweli kilichochambana na kingine. Inaeleweka hizi chokochoko mlengwa ni cdm. Uzuri ni kuwa sasa hivi watu wanauelewa mpana hivyo wanajua kila kinachoendelea.
 
Uhitaji rocket science kufahamu kuwa iwe kwa namna yoyote ile, CCM & DOLA zinaenda kutimiza lengo la ama kuifuta CHADEMA kwenye uso wa siasa za Upinzani au kuidhoofisha kabisa ibaki chama cha kawaida sana. Kwa hiyo CHADEMA hata ikichukua ushauri huu au isichukue bado kikombe cha CCM itakinywa tu.
Sasa hivi ni siasa za JINO kwa JINO, yani don't bow or kneel down maana CCM wanaendesha siasa za UBABE kwa msaada wa DOLA, hakuna reconciliation itayoiokoa CHADEMA.

Matendo ya CCM na DOLA yapo wazi, usishangae kuona Bunge lijalo kambi ya Upinzani ikiundwa na NCCR ya Mbatia. Huu ni mkakati.

Pichani ni Dr. Bashiru Ally
View attachment 1378702

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu uko sahihi ile mbaya, ila uzuri sasa hivi bila tume huru ya uchaguzi wapinzani wa kweli hatutashiriki, na kelele za tume huru ya uchaguzi ni kama zote. Kwa sasa inadhidi kudhihirika ni chama gani huwa kinashinda kwa kura, na kipi huwa kinanajisi box la kura ili kitangazwe washindi. Mfano halisi ni huyo katibu mkuu, alichokuwa anatapika hapo kwenye press conference. Wapinzani wa kweli waendelee kushikilia hapo hapo kwenye kudai tume huru ya uchaguzi, ukweli unazidi kusogea peupe. Hao wapinzani walioamua kumsujudia shetani ili wapate fahari ya dunia hii, waendelee kwa raha zao wananchi wanaojitambua wako wa kutosha.
 
Mkuu huu ushauri wako nauunga mkono, nimewashauri cdm kama chama wasijibu lolote hasa kwa huyo Mbatia au mwingine yoyote wa mwelekeo huo. Maana lengo hasa ni kuwatoa cdm kwenye taswira safi, wao wajikite kudai tume huru ya uchaguzi, wataishia kuona kauli kama za leo za kina Bashiru. Hao wapinzani design ya kina Mbatia waachwe watapewa moto wao huku mitandaoni. Uzuri ni kuwa wapinzani hasa Cdm hawajamjibu chochote Mbatia au mwingine mwenye uelekeo huo, maana chama kinachotafutwa hapo ni cdm zaidi.
Mkuu umenielewa Sana.
 
Back
Top Bottom