Ushauri wangu Kwa wale wanaotaka kuagiza magari kipindi hiki

Ndivyo inavyokua nimeshangaa namna mleta uzi alivyozunguka na burungutu la hela.
 
Nimeagiza kupitia SBT Japan...njia ya kuagiza mwenyewe bado inanipiga chenga mkuu
Next time agiza mwenyewe haina ugumu mkuu ukikwama nitakupa namba ya sales manager wa kule Japan ninazo namba zao, na namba ya meneja wa branch ya Dar (mtu poa sana) utaenda kuhakiki invoice yako. Ingawa wadada na staff wa pale Samora watakukata sana jicho kwa kuwanyima ridhiki.
 
Poapoa mkuu nashukuru Kwa ushauri wako.... barikiwa sana
 
Mkuu hii ikichoka nitainunua mimi 😁 ile DUN nimeikosa.
 
Ikifika tu chuma tunaibless kaka PureView zeiss congratulations sana.

Kusema kweli issue mbili kubwa, dollar na kupanda kwa gharama za shipping, mtu unaweza amua kwanza kukausha na gari lako kwa muda.
 
Ikifika tu chuma tunaibless kaka PureView zeiss congratulations sana.

Kusema kweli issue mbili kubwa, dollar na kupanda kwa gharama za shipping, mtu unaweza amua kwanza kukausha na gari lako kwa muda.
Ni kweli kabisaa mkuu maana Kwa hii Hali ya uchumi ni Bora utulie Tu gari yako bila kuuza
 
👍
 
Be forward ukilipa kwa Card au paypal unalipa kwa TSH, so inategemea nawe unanua wap
 
Ukinunua befoward ukalipa kwa Card ama Paypal unalipa kwa Tzs.
 
Ndio ungewaambia SBT Japan wakupe account namba ya huko JP unatuma hela kutoka akaunti yako kwenda kwao, hutasikia habari ya uhaba wa $ maanake zitaenda kama Yen.
Ukinunua gari kwa yen utapasuka vibaya sana,,
Ndo mana watu wanapenda kulipa kwa dola, ila siku hizi nimesikia be forward wana option ya kulipa kwa debit card ambayo ina deduct moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako kwa rate ya dola ya bot kwa siku hiyo.
 
Kampuni nyingi za nje wataanza kufungua account za TT ila rate ya dollar itakuwa kubwa Sana ili wasipate harasa nahisi dola moja itafika Hadi Tsh 3000 kama unataka kutumia TT
 
Sio rocket science. Siku ingine waambie SBT Japan wakupe invoice halafu nenda nayo kwenye bank yako waambie nataka kuwalipa hawa sbt nanunua gari invoice hii hapa. Bank yako watatuma hizo hela.
Nilikua nasubiri ufike kwenye maelekezo haya, Naomba kukutaarifu kuwa benki za kibongo zinakataa kufanya hivi. Zinakubali endapo unanunua kitu kwa kutumia currency nyingine na sio US dollar. Juzi nilienda CRDB tena ya Kigamboni tu, jamaa walinifanyia transaction ya GBP easy ila nikawauliza ingekua US dolla ningepata huduma?? walisema kwa US dollar haiwezekani, KUNA UHABA WA USD.

In summary ni rahisi kununua gari UK kwa paundi (na paundi imechangamka sana rate yake 1pound ni sawa na 3700 TZS selling rate kwa board) Ni ngumu kununua gari Japan kwa Us dollars ha wao hawaitaki hela yao YEN, hii syndicate ya madolari itatukaanga sana. Unaweza uza gari yako uliyo nayo halafu ukashindwa kuagiza gari utakayo itaka ukaishia kula hela. Hivyo kama una gari yako na haikusumbui iko vizuri, huu sio muda mzuri wa kuiuza, unaweza usimiliki gari tena.

Addition. Jana Enhance auto wawakilishi wao kwa Tanzania walinipigia sim kuna gari nili INQUIRE kwenye site yao, nikawauliza hili swali naweza lipa hii gari kwa Local tzs kwenye akaunti yenu? wakasema hawapokei local tzs, wanachotaka ni mtu uwe na DOLARI mkononi ukawapatie, au ukadeposit DOLARI, That's it ni ngumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…